Rais Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja wa Wizara, na Naibu Makatibu Wakuu 10 wa Wizara mbalimbali. Aidha, Rais Kikwete amemhamisha Naibu Katibu Mkuu mmoja kutoka Wizara moja kwenda nyingine.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo wa maofisa hao waandamizi wa Serikali unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011, na wataapishwa Jumamosi wiki hii, Aprili 30, saa sita mchana.
Taarifa hiyo inasema kuwa katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bwana Job D. Masima kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Aidha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemhamisha Injinia Mbogo Futakamba aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji kwenda Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Taarifa hiyo inasema kuwa Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni kama ifuatavyo: · Bwana Aphayo Kidata ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kidata alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. · Bwana Hab Mkwizu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mkwizu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri. ·
Bwana Charles Amos Pallangyo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Pallangyo alikuwa Mkurugenzi wa Uratibu – Ofisi ya Waziri Mkuu. · Bibi Mwamini Juma Malemi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya hapo alikuwa Msaidizi wa Makamu wa Rais katika masuala ya Maendeleo ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Wananchi. ·
Injinia Mussa Ibrahim Iyombe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi na JKT. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Usafiri katika Wizara ya Ujenzi. · Injinia Dkt. John Stanslaus Ndunguru ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi katika wizara hiyo hiyo ya Ujenzi. ·
Bwana John Thomas James Mngodo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi. Kabla ya uteuzi wake alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula. · Bibi Anna T. Maembe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Kabla ya uteuzi wake, Bibi Maembe alikuwa Mkurugenzi wa Mazingira na Habari wa NEMC. ·
Bibi Sihaba Nkinga ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Uchukuzi. · Injinia Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya Petroli.


Hongereni sana viongozi wetu Serikali. Nakupongeza Bw. Mrindoko kwa kuwa juhudi na uchapakazi wako umekufanya uaminiwe na wakuu wa Serikali. Mungu awabariki nyote.
ReplyDeleteHongera sana Bw. Mrindoko. Mungu azidi kukusimamia na kukupigania. Utaratibu na unyenyekevu wako umekukuza wengine waige.
ReplyDeleteMdau....
KOR
Naona wakiristo wengi kuliko waislamu
ReplyDelete"KATIBU MKUU WA MANAIBU KATIBU WAKUU" Yaani bongo yetu vyeo vingine nashindwa hata kuvielewa,ni mtiririko usioeleweka na hii ndiyo inachangia kutumika kwa pesa za serikali hovyo wakati tunalia kuwa nchi yetu masikini,Sasa jopo loote hili la viongozi lina umuhimu gani ??na hata hayo maendeleo hatuyaoni,watendaji wengi maendeleo madogo,maisha ya mtanzania yanazidi kuwa duni tu,kwa ushauri wangu ningependa vyeo vingine visivyo na umuhimu wowote vifutwe ili kubana matimizi na kuweza kuboresha maisha ya mtanzania.
ReplyDeletemtoa maoni Dar.
Anony 04:55:00 PM
ReplyDeleteTanzania haina dini. Tafadhali usituletee hiyo habari yako ya kuleta chuki za kidini, watanzania wahatadanganyika kwa hili kamwe.
Ni kweli mdau anavyosema hivi vyeo vya ajabu ajabu hata mimi sioni sababu ya kuwa navyo hii ni kufuja tu pesa za serikali wakati maisha ya mtanzania yanazidi kuwa duni,tuna kuwa na mlolongo mkubwa wa vyeo wakati maendeleo hayaonekani,hata mimi nashauri baadhi ya vyeo kama hivi vifutwe ili kubana matumizi.
ReplyDelete