mpaka leo hii ni takribani siku nne toka kibanda hiki cha kukaa abiria wanaosubiria usafirikianguke na hakuna taratibu zozote zilizochukuliwa juu yake mpaka wakati huu.sasa sijui ndio wanasubiria mpaka JK atoe kauli yake ndio kiweze kufanyiwa kazi??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Pesa hazikutengwa kwa kazi ya ukarabati wa kibanda kwa mwaka huu wa fedha. Kitabidi kisubiri mwaka ujao wa fedha.
    Utawala.

    ReplyDelete
  2. Eti mpaka JK atoe kauli! Jamani, kazi ya HALAMSHAURI YA JIJI ni nini? Hakuna wanaosimamia vituo vya mabasi?

    ReplyDelete
  3. Sio siku nne zaidi ya wiki mbili sasa wanataka mpaka mtu afe hapo ndo waunde tume jamani tutafika kweli

    Amir

    ReplyDelete
  4. Haya ndio matatizo ya nchi yetu,viongozi wahusika wapo lakini hawafuatilii matatizo ya wananchi kwa karibu zaidi,kazi yao kulumbana bungeni na kufikia mpaka kushiriki kuzindua pombe !!!ni aibu sana kwa taifa letu,halmashauri ya jiji kazi yao kutuma wanamgambo kwenda kunyanyasa wafanya biashara wadogo walala hoi na kuwadhulumu bidhaa zao,huduma kama hizi za kukarabati mji hazipo,hapo utasikia wanasubiri kuanzisha tume ya kushughulikia ukarabati wa banda hilo,pia wananchi nasi tumezidi kujisahau katika anasa,mabonanza kila kukicha na kuiga timu za Ulaya hizo ndio zetu,na hii inatufanya tuwe wavivu wa kufikiri na hata kufuatilia au kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili nchi yetu,Kweli Tanzania tuna safari ndefu na kwa staili hii sijui kama tutafika,
    mdau Ugabuni.

    ReplyDelete
  5. aibu!aibu!aibu!

    ReplyDelete
  6. Ni kweli mdau anavyosema hapo juu,kwenye mabonanza,kuzindua pombe,na kila kukicha bia mpya zinazinduliwa,viongozi na wananchi wako bussy kuserebuka,mambo kama haya watu wanayaona na hawajali,hiyo ni sawa tu,tusema tangu banda hilo lianguke hakuna kiongozi wa jiji au manispaa aliyepita hapo na akaona,pia wananchi nao si wameona ,lakini hakuna anayejali.Haijulikani mwisho wa nchi yetu utakuwa wapi ??NI AIBU TUPU.Lakini starehe ni kama kazi,nguvu na muda wa starehe tunao sana kuliko kujali matatizo yanayotukabili siku hadi siku.

    ReplyDelete
  7. Huu ndio ugonjwa mkubwa wa watanzania. Tumezoea kila kitu kufanywa na serikali. Na ndiyo maana naombea ujamaa na kujitegemea uishe na tuanze ubepari; kwani banda hilo lingekuwa na mtu binafsi asingekubali likae siku zote hizo bila kufanyiwa ukarabati. Kuna mifano mingi sana Tanzania ya kuonyesha jinsi tulivyo na tabia ya kutojali vitu vya umma. Viwanda vya morogoro ,Mwanza, Tanga na sehemu nyingi nchini tumeviua kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa na uchungu navyo.ukiacha serikali kuu ,serikali za wilaya ,kata zipo mbele sana kukusanya kodi au ushuru kwa wananchi lakini ili kuendeleza shughuli za kimaemdeleo,lakini inapokuja ktk utoaji huduma zipo nyuma. Wananchi inabidi wawe wakali kwa kuhakikisha kuwa viongozi wote wanaozembea katika sehemu zao hawachaguliwi tena hata kama watamwaga pesa wakati wa pilika za uchaguzi.
    Kalenga Boy

    ReplyDelete
  8. hao wanadeka sana wangekua huku niliko yaani watu wangejiangusha hapo wanasema wamevunjika mgongo na wanasue city. Wanalipwa hapo kishenzi...Yaani hapo ulaji sana tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2011

    Ankal, hicho kituo kinaitwa "Morocco Hoteli" sio "Mikumi". Mikumi ni kituo cha pili toka hapo kama unaelekea Buguruni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...