Home
Unlabelled
KITUO CHA DALADALA MAGOMENI MIKUMI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Pesa hazikutengwa kwa kazi ya ukarabati wa kibanda kwa mwaka huu wa fedha. Kitabidi kisubiri mwaka ujao wa fedha.
ReplyDeleteUtawala.
Eti mpaka JK atoe kauli! Jamani, kazi ya HALAMSHAURI YA JIJI ni nini? Hakuna wanaosimamia vituo vya mabasi?
ReplyDeleteSio siku nne zaidi ya wiki mbili sasa wanataka mpaka mtu afe hapo ndo waunde tume jamani tutafika kweli
ReplyDeleteAmir
Haya ndio matatizo ya nchi yetu,viongozi wahusika wapo lakini hawafuatilii matatizo ya wananchi kwa karibu zaidi,kazi yao kulumbana bungeni na kufikia mpaka kushiriki kuzindua pombe !!!ni aibu sana kwa taifa letu,halmashauri ya jiji kazi yao kutuma wanamgambo kwenda kunyanyasa wafanya biashara wadogo walala hoi na kuwadhulumu bidhaa zao,huduma kama hizi za kukarabati mji hazipo,hapo utasikia wanasubiri kuanzisha tume ya kushughulikia ukarabati wa banda hilo,pia wananchi nasi tumezidi kujisahau katika anasa,mabonanza kila kukicha na kuiga timu za Ulaya hizo ndio zetu,na hii inatufanya tuwe wavivu wa kufikiri na hata kufuatilia au kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili nchi yetu,Kweli Tanzania tuna safari ndefu na kwa staili hii sijui kama tutafika,
ReplyDeletemdau Ugabuni.
aibu!aibu!aibu!
ReplyDeleteNi kweli mdau anavyosema hapo juu,kwenye mabonanza,kuzindua pombe,na kila kukicha bia mpya zinazinduliwa,viongozi na wananchi wako bussy kuserebuka,mambo kama haya watu wanayaona na hawajali,hiyo ni sawa tu,tusema tangu banda hilo lianguke hakuna kiongozi wa jiji au manispaa aliyepita hapo na akaona,pia wananchi nao si wameona ,lakini hakuna anayejali.Haijulikani mwisho wa nchi yetu utakuwa wapi ??NI AIBU TUPU.Lakini starehe ni kama kazi,nguvu na muda wa starehe tunao sana kuliko kujali matatizo yanayotukabili siku hadi siku.
ReplyDeleteHuu ndio ugonjwa mkubwa wa watanzania. Tumezoea kila kitu kufanywa na serikali. Na ndiyo maana naombea ujamaa na kujitegemea uishe na tuanze ubepari; kwani banda hilo lingekuwa na mtu binafsi asingekubali likae siku zote hizo bila kufanyiwa ukarabati. Kuna mifano mingi sana Tanzania ya kuonyesha jinsi tulivyo na tabia ya kutojali vitu vya umma. Viwanda vya morogoro ,Mwanza, Tanga na sehemu nyingi nchini tumeviua kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa na uchungu navyo.ukiacha serikali kuu ,serikali za wilaya ,kata zipo mbele sana kukusanya kodi au ushuru kwa wananchi lakini ili kuendeleza shughuli za kimaemdeleo,lakini inapokuja ktk utoaji huduma zipo nyuma. Wananchi inabidi wawe wakali kwa kuhakikisha kuwa viongozi wote wanaozembea katika sehemu zao hawachaguliwi tena hata kama watamwaga pesa wakati wa pilika za uchaguzi.
ReplyDeleteKalenga Boy
hao wanadeka sana wangekua huku niliko yaani watu wangejiangusha hapo wanasema wamevunjika mgongo na wanasue city. Wanalipwa hapo kishenzi...Yaani hapo ulaji sana tu.
ReplyDeleteAnkal, hicho kituo kinaitwa "Morocco Hoteli" sio "Mikumi". Mikumi ni kituo cha pili toka hapo kama unaelekea Buguruni.
ReplyDelete