Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akipokewa na Mwenyeji wake ambae ni Rais wa Taasisi inayoshughulika na utoaji wa huduma za kibinadamu ya Project C.U.R.E. nchini Marekani Daktari Douglas Jackson (kushoto)alipohudhuria katika hafla iliyoandaliwa baada ya kumaliza ziara ya kikazi Arizona hivi karibuni.katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mwanaidi Maajar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mke wa muanzilishi wa Project C.U.R.E. Daktari AnnaMarie Jackson baada ya Mama Kikwete kumpa zawadi moja ya vazi la asili la mwanamke wa kitanzania (kanga) na kumvalisha katika hafla ya kuagana huko Arizona. Taasisi hii inafanyakazi katika nchi 120 Duniani, huwa inautaratibu wa kumchagua mke wa Rais mmoja kutoka nchi ambazo zinahitaji kusaidiwa na kumfanya HARAMBEE kwaajili ya kuchangia vifaa mbalimbali vya afya pamoja na madawa. Project C.U.R.E. imeshachangia wake 6 wa Marais duniani akiwemo Mama Salma Kikwete ambae katika nchi za Afrika ni wapili kuchangiwa akitanguliwa na GHANA.
Mandhali ya Mlima Arizona unavyoonekana.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Du! Asante kwa habari na picha lakini hakuna mlima unaoitwa mlima Arizona. Mlima gani huo jamani wakati ni ka-kichuguu tu hako?

    ReplyDelete
  2. Washington Consensus hiyo. Yetu macho.

    ReplyDelete
  3. Good job mama kikwete!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...