SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMETILIANA SAINI NA SERIKALI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA MAKUBALIANO YA MRADI MKUBWA WA MATENGENEZO YA KITUO CHA MATANGAZO YA MASAFA MAFUPI (SHORT WAVE) KILICHOPO DOLE PAMOJA NA STUDIO ZA SAUTI YA TANZANIA ZANZIBAR ZILIOPO RAHALEO MJINI ZANZIBAR

MAKUBALIANO YA MRADI HUO UTAKAOGHARIMU ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MBILI NUKTA NNE, KWA UPANDE WA ZANZIBAR UMETIWA SAINI NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI , UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO DK ALI MWINYIKAI NA KWA UPANDE WA CHINA UMETIWA SAINI NA MAKAMO WA RAIS WA KAMPUNI YA INTERNATIONAL ECONOMIC AND TECHNOLOGICAL TRADE AND INDUSTRIAL BWANA ZIONG ZUOSEIN

KWA MUJIBU WA MAKUBALIANO YA MKATABA HUO YALIYOTIWA SAINI KATIKA MAJENGO YA WIZARA YA HABARI , UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO , SERIKALI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA ITAGHARAMIA UWEKAJI WA MITAMBO MIPYA YA MASAFA MAFUPI KATIKA KITUO CHA KURUSHIA MATANGAZO KILIOPO DOLE , UWEKAJI WA ANTENA NA VIPOZA HEWA KATIA STUDIO ZA RAHALEO NA DOLE .

MATENGENEZO HAYO YANATARAJIWA KUANZA MAPEMA MWEZI JULAI MWAKA HUU NA YATACHUKUA MUDA WA MIEZI MITANO.

IMETO0LEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...