![]() |
| Marehemu Sheikh Yahaya Hussein enzi za uhai wake |
Habari ambazo zimeingia chumba chetu cha habari sasa hivi zinasema kwamba mnajimu maarufu Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia.
Mtoto wa marehemu, Hassan Yahya Hussein, kaithibitishia Globu ya Jamii sasa hivi kwamba baba yake amefariki dunia mnamo saa nne asubuhi ya leo nyumbani kwake Mwembe Chai jijini Dar es salaam. Alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo.
Hassan amesema mipango ya mazishi yanafanyika hapo hapo Mwembe Chai, na kwamba maziko yanatarajiwa kufanbyika kesho hapo nyumbani kwa marehemu.
Globu ya Jamii inatoa mkono wa Rambirambi kwa wafiwa.
Mola Aiweke Roho ya Marehemu mahali pema peponi
-Amina



Poleni kwa msiba. marehemu astarehe kwa amani peponi. Amina.
ReplyDeleteMungu ailaze roho ya Marehemu Sheikh Yahya mahali pema peponi, Amen
ReplyDeleteIna lillah wainallilah rajiun. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi Amin
ReplyDeleteM.Omary
INNALILLA WA INNA ILAIHI RAAJIUUN.... KWAKE MWENYE EZ MUNGU , NA NI KWAKE TU NDIO MAREJEO YETU, InshaALLAh Mola wetu Mlezi AMSAMEHE MADHAMBI YAKE! AMNG'ARISHIE KABURI LAKE NA AMJAALIE QAULI THABIT HUKO AENDAKO KATIKA MAPUMZIKO YAKE! Poleni sana wafiwa ...TUTAMISS VITUKO VYAKE ....
ReplyDeletePole wadau kwa msiba huo wa Mnajimu wetu mashuhuri.
ReplyDeleteYako mengi ya kukumbuka ya sheikh huyu. Kila mtu atamkumbuka kwa namna yake. mimi binafsi namkumbuka kama miongoni mwa watu wa mwanzo kuwa na TV pale maeneo ya Magomeni. Mwaka 1986 tulikwenda kutazama fainali za kombe la dunia nyumbani kwake. Alifahamu fika kuwa majirani zake walipenda soka na hawakuwa na TV. Hivyo alitoa TV yake nje na kuiweka juu na sisi kina nanhii tukapata uhondo. Nakumbuka nilitazama pambano kati ya Argentina na ujerumani. wakati huo nikiwa darasa la sita paleeeeeee shule ya msingi mzimuni.
Mungu amrehem!
Hussein Kitta
RIP, Sheikh!
ReplyDeletePoleni kwa msiba mzito,Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.
ReplyDeleteAmen
M.Said
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi na pia awape nguvu familia yake yote kwa wakati huu mgumu. Amina
ReplyDeleteInnalillahi Waiina Ilayhi Rajiuun Mungu amlaze pema peponi
ReplyDeleteMbona Shehe na m/kiti wa CCM mzee mwinyimvua wamefariki siku moja na tena eneo moja hapo mwembe chai? na taarifa zikafikia blogu kwa wakati mmoja na zikawekwa humu ndani kwa wakati mmoja zikiongozana? Huenda walikuwa ni marafiki walioshibana sana kiasi kwamba msiba wa mmoja ulimpa mwenziwe majonzi yasiyovumilika na hivyo kumsababishia mauti. Pole nyingi kwa wafiwa wote. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake na libarikiwe...AMEN.
ReplyDeletepoleni sana kwa msiba.mungu wape moyo wa subira.
ReplyDeleteR.I.P.....alitabiri?
ReplyDeletePole sana Sheikh wetu Yahya. Hakika ni pengo umetuachia. Tulikutegemea kwenye mambo mengi ya kimaisha. Lakini kwa vile kazi ya mola haina makosa hatuna budi kukubali matokeo. Tunaamini mikoba yako ulimwachia kijana wako ili kazi yetu iendelee.
ReplyDeleteINALLAH WAINALILLAH RAJIUN!
Duh, shekh umekwenda? Nani atamtabiria JK tena? Mbona hukuweza kutabiri kifo chako?
ReplyDeletemaneno ya mtani wako hayo! Ukalale pema peponi mnajimu wetu. Tutakumiss hasa wakati wa kampein.
Huyo anayesema mbona wamekufa pamoja na mwenyekiti wa ccm??kweli ndugu unauliza swali la kijinga!!hayo ni mapenzi ya mungu...mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.amen
ReplyDeletemlinzi wa kikwete rip
ReplyDeleteInna lillahi wainna ilaihi rajiun poleni sana. M'mungu ailaze roho ya marehemu wote pepon amiin.M'mungu awape mioyo ya subra wale wote waliofikwa na msiba huu.kila nafsi itaonja mauti na sisi tupo njiani.
ReplyDeleteS.mahboob
Kaiandaliye ssm na watejawako makao!
ReplyDeletePoleni sana wanafamilia. Kweli ameacha pengo ambayo haiwezi kuzibwa. Hatutasahau matabiri yake ambayo tulingonjea kwa hamu mno.
ReplyDeleteMungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
ndiyo alitabiri alisema mwenzi wa tano kutatokea jambo kubwa watu watege masikio.kweli tarehe mbili osama kauwawa na tarehe 20 yeye mwenyewe kafa
ReplyDeleteKila nafsi itaonja mauti, Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. AMINA.
ReplyDeletemwenyezi mungu amuadhibu kutokana shirki zake,na wala allah hatawasamehe waliomshirikisha yeye na kitu chochote,bali husamehe madhambi yasioya shirki kwa amtakae,atakumbukwa kwa unajimu uchawi na kuupoteza uislamu kwa utabiri wake na shirki zake,watu wakadhania uislamu ni uchawi uchawi tu na dini ya majini,rejeeni kwenye tauhidi enyi wenye kumuombea rehma mtu kama huyu,allah avunje vunje juhudi zake na wala asibiraki historia yake,twamuomba mungu asitujaalie kama kifo katika hali yake,amin
ReplyDeleteNaomba mtofautishe "Bwana Yesu" na "Allah". Mbona mnachanganya mada?
ReplyDeleteSiku chache baada ya mtabiri mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussein wa Dar es Salaam kutangaza katika vyombo vya habari kuwa mwana CCM atakayejitokeza kuchuana na Rais Jakaya Kikwete katika kinyang’anyiro cha kugombea urais mwaka huu, atakufa ghafla, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ Ubungo ametoa masharti matatu kwa mtabiri huyo vinginevyo naye atakufa ghafla.
ReplyDeleteKatika mahubiri kanisani hapo jana, Mchungaji Kiongozi, Gwajima alisema demokrasia ya Tanzania imo hatarini endapo mtu mmoja ataachiwa kuamua hatma ya taifa kinyume na mapenzi ya Mungu asiyekuwa na upendeleo kwa mtu yeyote.
“Baada ya kuendelea kutenda kazi zake zikiwa ni chukizo machoni mwa Mungu, leo ninatoa hukumu kutoka kwa Bwana, nanyi nyote mtachuja kuwa ni upi utabiri wa kweli kati ya Sheikh Yahaya na Mungu. Ninamwagiza Sheikh Yahaya afanye mambo matatu la sivyo naye atakufa ghafla kama alivyowatishia Watanzania wenzake,” alisema.
Sharti la kwanza alisema ni Sheikh Yahaya kwenda katika kanisa hilo la Glory of Christ na kuonana na mchungaji Gwajima yeye mwenyewe ili amwongoze kwa sala ya toba, kisha ampokee Yesu katika maisha yake.
Sharti la pili, Sheikh Yahaya ameamriwa kuanzia sasa aachane na utabiri wake ambao kwa miaka mingi alisema umewaumiza watu wengine wasiokuwa na hatia na kuwafaidisha wengine wachache kwa njia za giza.
Na sharti la tatu, Sheikh Yahaya ametakiwa, baada ya kuokoka, arudi katika vyombo vya habari kwa nguvu ileile aliyoitumia kutangaza utabiri wake wa mtu kufa ghafla na sasa awatangazie Watanzania mabaya yake yote aliyokwishayafanya kwa watu wa taifa hili hadi siku ya mwisho alipolazimika kuokoka.
Akifafanua juu ya masharti hayo, Mchungaji Gwajima alisema kimsingi yeye anamkubali Rais Jakaya Kikwete kuwa kiongozi wa taifa hili ila kinachomkera ni Sheikh Yahaya kuwatisha watu wengine wasitumie haki yao ya msingi katika kuikuza demokrasia hapa nchini.
Alipohojiwa kwa njia ya simu, Sheikh Yahaya ambaye alisema yuko nje ya jiji la Dar es Salaam kwa siku ya jana, alisema katika kipindi cha miaka 40 ya utabiri wake umekuwa sahihi siku zote na umaarufu wake ni wa kimataifa.
“Kamwe sitakwenda katika kanisa hilo, pia siko tayari kufuata sharti hata moja kutoka kwa mchungaji huyo.
Nimeanza utabiri kabla ya yeye kuwa shemasi wa kanisa hivyo endapo nitakufa najua ni siku zangu zimefikia mwisho wala si vinginevyo,” Sheikh Yahaya alisema.
Akitoa mifano ya utabiri wake ambao aliosisitiza kuwa sahihi mara zote, alitabiri msiba wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa kwa maelezo kwamba taifa litapata msiba mkubwa. Pia alisema aliwahi kutabiri kifo cha kiongozi mashuhuri ambaye kifo chake kingewakutanisha watu wa mataifa mbalimbali, dini, rangi na vyama mbalimbali vya siasa na kwamba kiongozi huyo alikuwa hayati Mwalimu Nyerere.
“Je, sikutabiri kuwa ndani ya CCM utazuka mtafaruku na kusababisha ufa ndani ya chama hicho kitu ambacho ninyi waandishi mmekishuhudia hivi karibuni?
Mimi siwezi kuongea kashfa yoyote dhidi ya mchungaji huyo bali ninachosema akipenda apeleke malalamiko yake Ikulu, kwani nako huko wapo watu wa kumjibu waliozishuhudia kazi zangu kwa miaka yote,” alitamba Sheikh Yahaya.
Alisema alitarajia kiongozi huyo wa kanisa aempe mwaliko rasmi waonane mahali popote siyo hapo kanisani ili waelezane masula ya nyota kwa undani badala ya ‘kumtisha’.
CHANZO: NIPASHE
Utabiri na Uchungaji ni vitu viwili tofauti kabisa.Utabiri hauna dini ni kipaji.
ReplyDeleteHivi wewe unaetoa kauli chafu kumkashifu mtu aliefariki kweli unaijui dini vizuri wewe, soma biblia soma masahafu vinasema nini pale unapopata habari za mtu kupatwa na mauti. Unahukumu kabla hujahukumiwa nani aliekuambia kuwa wewe ni mwema na huna dhambi mbele za Mwenyezi Mungu? tubu kwa mola wako akuondolee roho ya shetani iliyonayo.
ReplyDeleteRIP Shekh Yahaya Hussein.
Mdau