Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti, inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Profesa Amandina Lihamba, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mara baada ya kufungua Warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti, inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25.
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua warsha hiyo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki baada ya kufungua rasmi warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti, inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2011

    Doctor Manya mzee wa Geology nakuona hapo umekula 'Pause' pembeni mwa "Rasta'.Ni mimi classmate wako PCM Sengerema High school 1990-1992 na Mlimani Bsc(Geology) 1994-1997..!!Nikipata muda nitakuja kukuona hapo Idarani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...