
Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo (kulia) akipokea ufunguo wa gari moja lenye thamani ya shilingi milioni 82 za kitanzania kutoka kwa Mkuu wa sekta ya Miundombinu katika jumuiya ya Ulaya ( EU Head of Infrastructure) Mr. Adam Grodzicki (mwenye miwani) kwaajili ya kusaidia sekta ya usafiri katika Wizara ya Uchukuzi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo akijaribu kuwasha gari moja aina ya TOYOTA Land Cruiser Station Wagon lenye thamani ya shilingi milioni 82 za kitanzania kutoka kwa Msimamizi mkuu wa Sekta ya Miundombinu katika Jumuiya ya Ulaya (EU Head of Infrastructure)Mr. Adam Grodzicki (kulia )kwa ajili ya kusaidia sekta ya usafiri katika Wizara ya Ujenzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Gari lililokabidhiwa kwa Wizara ya Uchukuzi leo.
Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO


Mhandisi Omar habari za kazi?.Hizi gharama za hili 'kruza mkonga' kwanini(badala yake) serikali isingeomba hata lori mbili za kuzolea taka jijini Daresalaam.Hili suala la usafi jijini Dar linaweza lisikuhusu moja kwa moja lakini ninachotaka kusema hapa ni kwamba jijini la Daresalaam ni chafu sana.Nyie mnaokaa huko kwenye majiji masafi wenzetu wanafanyaje huko(kila mtu aje na wazo lake)..
ReplyDeletemaana Dar ukiweka mapipa ya takataka kila kona ya jiji yanaibiwa!!
David V
Tatizo kubwa la waTZ ni utamaduni. Utamaduni wetu hautufundishi kufanya kitu kwa hiyari. Kila kitu lazima tusukumwe ndio tufanye. Chukulia wewe mwenyewe nyumbani kwako. Shughuli za usafi zote zinafanywa na mama watoto au dada wa kazi. Ukienda ofisini usafi wa maeneo unafanywa na mfanyakazi wa sehemu ya usafi. Kama usafi haukufanywa na watu waliopangiwa hiyo kazi basi haufanywi na mtu mwengine. Miji yetu tumewapangia manispaa zifanye usafi wa mji, wakiwa hawa wafanyakazi hawakufanya hiyo kazi basi mji unakuwa mchafu. Nchi za wenzetu usafi wa mjini ni jukumu la kila mkaazi wa huo mji. Wakorofi hawakosekani, lakini kuna watu wakikuta takataka zimetupwa hovyo basi waziokota na kuziweka zinapotakiwa kwenye pipa la taka. Kuna miji ukitupa taka sio sehemu yake ni kosa unalipa faini. Kwa hivyo ni kuwa wenzetu wana utamaduni wa kufanya usafi kwa hiyari na kuweka sheria kali kwa wakorofi.
ReplyDelete