Eng. Patrick Mfugale
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amemteua, Bw. Patrick Mfugale kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).

Taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Herbert Mrango na kusambazwa kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa uteuzi huo unaanza Mei mwaka huu na utadumu kwa miaka mitatu, "Kwa mujibu wa sheria ya Wakala wa Serikali (Excutive Agencies Act No 30 ) ya mwaka 1997 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009, Waziri Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli amemteua Injinia Patrick A. L Mfugale kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS)," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mfugalea alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS na amewahi kushika nafasi mbalimbali katika serikali na kusimamia ujenzi wa barabara na madaraja muhimu kwa taifa.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa Bw. Mfugale pia aliwahi kushika majukumu maalumu katika wizara hiyo kama Mkurugenzi wa Idara ya Barabara za Mikoa.

Bw. Mfugale ambaye ana Shahada ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Roorkee India, na Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu Loughborough cha Uingereza, ni mhandisi aliyesajiliwa na amehudhuria mafunzo ya Ujenzi na uchumi, Mafunzo ya miradi na utunzaji wa barabara pamoja na ujenzi na utunzaji wa madaraja. 

source: http://www.wavuti.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2011

    hii mambo yabkuteuana mpaka lini? weka mchuano halisi apatikane anayefaa, siyo kujuana

    ReplyDelete
  2. Congratulations Eng. Mfugale. I wish you all the best in this new position and I am sure you will do us proud!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...