Na Mwandishi Wetu
WALINZI wa Kampuni ya KK Security wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu shitaka la kuvunja godauni la Kampuni ya Tanzania Distilleries
Litimed.
Ilidaiwa mahakamani hapo juzi kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walivunja godauni la kampuni hiyo na kuiba vinywaji vya aina mbalimbali vinavyotengenezwa katika kampuni hiyo.
Watuhumiwa hao ni Ezekiel John (22), Hamisi Mustapha (27) na James Shetta (21).
Mbele ya Hakimu Issa Kasailo, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Mtani Magoma kuwa Novemba 2010, usiku eneo la Ubungo Millenium Business Park, washitakiwa walivunja godauni lililokuwa na vinywaji vya aina mbalimbali vyenye thamani ya sh. 36,186,042 mali ya kampuni ya konyagi.
Awali, washitakiwa hao walifutiwa kesi yao chini ya kifungu cha sheria cha 225,lakini hata hivyo Wakili wa Serikali, Hellen Moshi aliwakamata tena ili kuhojiwa upya, kesi ianze tena.
Hakimu alifuta kesi kwa sababu shahidi ambaye ndiye mpelelezi wa kesi hiyo alikuwa hakufika mahakamani hapo.
Hata hivyo, washitakiwa hao walikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Juni 4 mwaka huu.


wafanyakazi wa hii kampuni wanashirikiana sana na wakubwa kuiba mizigo kwenye makontena bandarini,kuna kesi zipo mahakamani lakini haziishi,sababu wanaoneana aibu
ReplyDelete