Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu shughuli za kikao cha nane cha mkutano wa nne wa Bunge leo mjini Dodoma ambapo wabunge mbalimbali wamepata fursa ya kuchangia bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 iliyowasilishwa hivi karibuni na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo.
Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Augustino Mrema akiingia ndani ya ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha nane cha Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde akichangia bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 iliyowasilishwa hivi karibuni na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo na kuhoji uchelewaji wa baadhi ya ofisi za serikali na Viongozi mbalimbali kuhamia mjini Dodoma ambako ndio makao makuu ya nchi leo mjini Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2011

    Bunge jeupeeeee. Watu hawana shida wameshakomba posho zao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2011

    Kumbe hata wabunge huwa ni watoro? Wakakamatwe kwa kuvunja sheria ya kutohuria, mmmhhhhhhhh hawa tu ndo wabunge wa Tz?

    ReplyDelete
  3. Mangi wa KiboshoJune 21, 2011

    Mbona viti viko wazi? au wapo katika vikao vya kupeana POSHO? Mzee wa 'Kiraracha' nakuona unaingia ndo ulitoka katika kikao cha 'Mkwanja"? Poa tu msee wangu. Nimependa sana mawazo ya Lusinde kuhusu serikali kuhamia Dodoma kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano DSM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...