Mkuu wa wilaya ya Muleba Mh. Angelina Mabula akipanda mti, hii ilikuwa ni sehemu ya kuwahamasisha wananchi wajenge utamaduni wa kupanda miti hasa ambayo ni rafiki wa mazingira, Mkuu huyo wa wilaya alipanda mti huo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani. Mti huo aliupanda mbele ya ghala la mazao la wananchi wa kijiji cha Bisheke.
Wasanii wa vikundi vilivyotumbuiza au kutoa burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kimkoa wilayani Muleba.
Baada ya mkuu wa wilaya ya Muleba Angelina Mabula kupiga marufuku usafirishaji wa mkaa tomka katika wilaya hiyo na kuelekea katika maeneo mengine umewafanya wafanyabiashara wa mkaa kutumia mbinu mbalimbali za kusafirisha mkaa huo toka wilayani humo, kama inavyoonekana gari lenye namba za usajili T486 ADZ lilikamatwa na mkuu wa wilaya likiwa limebeba mkaa, gari hilo lilikuwa limebeba mkaa huo katika staili ya pekee ambapo mkaa wote ulikuwa umefunikwa maturubai.
Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii,Muleba
Huku jamani ni kuoneana,sasa watu watatumia energy gani kupikia?gas,umeme hakuna hata kama upo bei hatuiwezi.usikute hata huyo DC anatumia mkaa.tuache visheria vya hovyo.
ReplyDelete