Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA umeisaidia Tanzania kujinyakulia tuzo ya utumishi wa umma Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Umoja wa Mataifa hasa kwa kuangalia ubunifu wa kuweza kuharakisha huduma nzuri kwa umma. 


Mkurugenzi mtendaji wa MKURABITA
Bw. Stephen Rusibamayila 
Baada ya kushika nafasi ya pili mwaka jana mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika. Tuzo hiyo imetolewa sambamba na kongamano la kimataifa la utumishi wa umma linalofanyika jijini Dar es salaam Tanzania kuanzia Juni 20 na litakamilika june 23.


Wawakilishi takriban 300 kutoka nchi 80 wanashiriki kongamano hilo. Mwandishi wa Umoja wa Mataifa Stella Vuzo anafuatilia kongamano hilo na amezungumza na mkurugenzi mtendaji wa MKURABITA Stephen Rusibamayila kuhusu ushindi wao wa tuzo


Kusikiliza mahojiano haya bofya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2011

    Ankal... "Title" ya hii habari na "caption" vinatofautiana, huyu ni mkurugenzi mtendaji au mkurugenzi wa uendeshaji????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...