Mhe. Freeman Mbowe na shangingi alilorejesha Bungeni |
Mnamo tarehe 21/06/2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012.
Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani CHADEMA kama vile ;
a) Kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petrol na dizeli.
b) Kupunguza kiwango cha faini za makosa ya barabarani kutoka shilingi 300,000/50,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 30,000.
c) Kufuta leseni za biashara kwenye Majiji,Halimashauri za Wilaya na Vijiji.
d) Kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi Nchini.
e) Kuongeza pesa kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya Mikopo.
Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura zaHAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali kutokana na sababu mbalimbali na haswa hizi zifuatazo;
1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.
2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya “Mashangingi” yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.
3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .
5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).
6. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa tunapunguza gharama za safari na haswa kuhakikisha kuwa ni viongozi wakuu na wenzi wao tuu ndio waruhusiwe kusafiri kwa kutumia daraja la kwanza (first class) ambao ni ;
- Rais
- Makamu wa Rais
- Waziri Mkuu
- Spika
- Jaji Mkuu
Pia misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya Nchi.
Hitimisho.
- Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
- Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya “Shangingi” alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.
Imetolewa na:
Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb), Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
21 Juni 2011
Kwa mwendo huu tutafika hata kama tutachelewa, Hayo ndio maneno sio kila siku wanajipangia mambo makubwa na kutuacha wananchi tunataabika na ugumu wa Maisha.Mungu awaongoze na kuwazidishia Maarifa kwa maamuzi mazuri yenye manufaa kwa Taifa
ReplyDeleteinatia matumaini CCM watabana mwishowe wataachia tu! Big up CHADEMA endeleeni kuvuta kamba kwa manufaa ya Watanzania wote! Kama Kenya waliweza kubadilisha magari ya Mercedes Benz kuelekea fuel efficient cars VW kwa nini sisi tusiweze? Ina maana tumebandikwa gundi katika hayo magari ya VX aka Mashangingi?
ReplyDeleteMtazamo safi na wenye Masrahi kwa Taifa Letu ila kama litapitishwa ninamashaka katika wakati wa huo MNADA.
ReplyDeleteHizi hoja ni safi kabisa kwa taifa linalo itaji maendeleo! Safi CHADEMA.
ReplyDeleteHawa sasa ndio viongozi. Kiongozi wa Unma huangalia maslahi ya taifa na si yake. Mbowe yuko serious. Na bahati nzuri pia kaenda shule. Tumechoka sana na serikali ya sasa. Really good initiatives. Well done and keep it up Freeman.
ReplyDeleteDennis B.
WATZ MNACHEKESHA...HIZI TABIA HAZIANZII BUNGENI! WATU HUTOKA NAZO KWENYE TAASISI. KWA SASA HATA VIONGOZI WA TASISI HUANGALIA MASLAHI YAO SI YA WAFANYAKAZI... MIMI NILIWAHI KUFANYA KAZI UNIVERSITY COMPUTING CENTRE MLIMANI. PALE NDIO KUNA PICHA HALISI.....MWANZONI NILIFIKIRI NI UNDUGUNIZATION LAKINI BAADAYE NIKAJA KUONA NI MASLAHI BINFSI ZAIDI....
ReplyDeleteHuwa nasikia hasira ninapoona kodi yangu (zetu wote) zikitumiwa ovyo ovyo kwa matumizi yasiyoleta maendeleo na raisi kafumba macho.
ReplyDeleteHapa ni pale Mla kodi yako anaamua atakavyoila yeye, wewe unayelipa huna maamuzi na pia ni lazima uilipe.
Juzi nasafiri kwenya kwa Mandela/SA kama mfanyabiashara mkubwa nimekaa business class na mfanyabiashara mwenzangu kutoka huko SA. Nauli Business class kwenda SA ni kama US$ 1,800 ukilinganisha na US$ 550 kwa economy. Basi bwana jamaa 5 kutoka wizara ya mambo ya nje, na wizara ya fedha nao hao wameingia business class, nikasema kula leki, kodi yetu hiyo. Sio suala la wivu wala ubaguzi kwani ni pesa zangu (kodi yetu) ndio imelipia ticket zao na sioni kweli umuhimu wa wao kusafiri business class, tena hawakuwa wakuu wa wizara.
Nimesikitika sana nilipokuja kugundua kuwa mawaziri na wabunge wetu wanalipiwa ndege "first class", kwa hela ipi tuliyonayo kama sio kukomoana na kutiana umaskini!!! Hivi hii nchi inamtazamo wowote wa maendeleo?
ReplyDeleteMbona vitu vingine vinatupa raia wakati mgumu na kupoteza uelewa wetu mdogo tulionao? Hivi kweli wamegoma proposal ya mabadiliko ya hayo madaraja (classes) ya kwenye ndege jamani?
ReplyDeletembowe sio mchovu ndio maana kafanya hivyo!!!!!!wenzangu na miyeee msiona na magari mengine mtawezaaa!!!tuliangalie hili!!
ReplyDeleteHuu ndio uzalendo wa kweli kujali maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla, big up sana upinzani hususani Chadema, hakuna kulala mpaka kieleweke
ReplyDeleteHONGERA MBOWE, HONGERA CHADEMA. HAYA NDIYO MAAMUZI MAGUMU YANAYOTAKIWA KUFANYWA KWA MASLAHI YA WANYONGE NA MASKINI WA TANZANIA. INSHALLAH, KWA MSIMAMO HUU WA KUTETEA WANYONGE, NITAWAPATIA CHADEMA KURA YANGU 2015 PAMOJA NA KWAMBA MIE NI CCM. NINA MPANGO PIA WA KURUDISHA KADI YANGU YA CCM KWANI KWA UWAZI KABISA NIMEONA WANAANGALIA MATUMBO YAO TU HUKU SISI WANYONGE TUKIENDELEA KUTAABIKA. MWE!
ReplyDeleteChadema mna akili sanaaaaaaaaa ndio maana mmeenda shule wote,maana hizi kodi zetu hatujui zinaenda wapi wanazila weeeee,this time liwalo na liwe kama noma na iwe noma sisi sio wale wa TZ wa miaka iliyopita kazi kutunyonya tuuu hapana,ukiangalia umeme ndio huo tunalala giza alafu asubuhi ndio wanarudisha Arusha tunapata shida na Moshi sasa hatujui wenzetu mikoani, Chadema tunaipenda,yani hii nchi ovyoooo kabisa kujilimbikizia mali tuu mafisadi wamejaa tele,wanakumbatiwa sasa imefika kikomo sasa liwalo na liwe tunaelekea pabaya.
ReplyDeleteMTAZAMO MWINGINE KUWEKA MAMBO SAWA:
ReplyDeleteNiijuavyo serikali yetu katibu wa Bunge anaweza badilisha fomu za kusaini mahudhurio na posho kama kambi ya upinzani ilivyoomba. Kisha wakatumia mafungu hayo yaliyosalia katika posho(ambozo kambi ya upinzani hawajachukua kwa uzalendo) wakajilipa tuu si unajua mambo ya re allocation???
MTAZAMO MBADALA
Wabunge wa upinzani wafungue akaunti ya pamoja waweka pesa zao za posho kila siku hapo na baaada kama ya mwaka mmoja wajenge kitu kama shule au chuo na wakibatize jina la "POSHO" na siku ya ufunguzi aitwe raisi au waziri mkuu na ihakikishwe vyombo vyote vya habari vinaalikwa ili kutoa taarifa sahihi kwa wana wa nchi. Hii inafaida zifutazo:
Kwanza inaonyesha uzalendo wa wapinzani
Pili inaziba mwanya wa matumizi mabaya ya hizi pesa za posho
Tatu itawaonyesha wana wa nchi kwa vitendo ni kwa kiasi gani tutaendelea kwa kubana matumizi.
Nne itaongeza imani ya wana wa nchi kwa wapinzani
Tano na muhimu majimbo yote mtapata mhula ujao
Ni mtazamo tu, Natumaini nimeeleweka.
Hasta ala vista siempere
Mheshimiwa Freeman unachekesha sana. hiyo gari ni ya taasisi ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na siyo yako kama mheshimiwa Mbowe. Umeikataa kwa sababu wewe una uwezo wa kuwa na magari zaidi ya hayo. kama uliweza kukodi helikopta kwa miezi mitatu hushindwi kuwa na gari aina hiyo ila sasa unataka kutudaganya watanzania tukuone kuwa unatujali. Kama mna dhati ya kutaka kushika dola basi enendeni kwa wafadhili wenu tafuteni msaada utakaojaza fuko la serikali ili sisi watumishi tulipwe kima cha chini mlichokitaja na wastaafu waweze kupata pensheni mliyoikusudia, hapo ndipo mnaweza kutueleza kitu tukawaelewa. Mmepewa milioni mia mbili na Sabodo mmegawana wenyewe, hatujawasikia hata mkipeleka kwenye makazi ya yatima japo elfu hamsini. Hatudanganyiki
ReplyDeleteAlichofanya Freeman ni sahihi kabisa kurudisha huo Mshangingi na baada ya hapo natarajia Rais ataagiza magari yote ya serikali yarudishwe na yauzwe kwa mnada kama alivyofanya President Kagame.
ReplyDeleteKimsingi magari yabaki kwa Rais,Makamu wa Raisi ,Waziri mkuu na Mawaziri wengine wote hawastahili kuwa na magari ya serikali.
Hebu fikiria driver anakaa Mbagala na Boss anakaa Mbezi beach ni kama Km 40 kwenda na kurudi Km 80 kwa siku bado Boss hajapiga misele yake unategemea nini?gari CC 4000 What do you expect? na hapo yupo peke yake yeye na Driver tu.
Kweli watz tuamke.
Pamoja na mambo mengi ya msingi waliyopropose wapinzani, suala la posho Mi nadhani cha msingi sasa hivi siyo marumbano kuhusu posho. Hizo posho ambazo wanazikataa wangezitumia kwa maslahi ya wananchi kwqenye majimbo yao badala ya kuweka marumbano yasiyo na msingi. Sisi wananchi tumewapa kura zetu ili tupate maendeleo. Pamoja na wao kutaka maslahi yao binafsi vile vile nasi tunahitaji tupate maendeleo kupitia wao. Hakuna haja ya kukataa poshoo hata kidogo walichotakiwa ni kuzipokea hizo posho na kuzitumia "effectively" kwenye majombo yao kwa maendeleo ya wananchi wao. sasa wakiziacha wanadhani zitawasaidia nn wananchi? Au walifikiri kuwa hizo posho ni za kutunisha mifuko yao binafsi? nadhani na wenyewe bado uelewa wao ni mdogo sana."Intention" yao ni kupokea hizo posho na kuzitumia zote kwa maslahi yao binafsi? basi wapokee then wazifungulie akaunti moja na wazifanyie kitu fulani cha maendeleo ili kuwaongezea imani wananchi tunataka "implementation" sasa marumbano is too much!!!
ReplyDeleteGod Bless Tanzania,God Bless Chadema.
ReplyDeleteHawa wanatuzingua sana hawa viongozi wote upinzani na tawala coz wanachogombania ni hilo jikeki tu hakuna lolote la maana. tena heri zimwi likujualo halikuli likakwisha kuliko zimwi lisilokujua.......
ReplyDeleteWatu acheni ushabiki usiyo na maana, hao wanagombania madaraka tu sasa tumewashtukiaaaa kila siku kufanya kazi na waandishi wa habari tu..Ninyi kila siku mnalima mnalima lini tutavunaaa?????? fanyeni jambo kupitia hicho mnachokipata ili tuone dalili za uzalendoo wenu...
Mnatafuta umaarufu usio na faida kwa wananchi.tumechoka jamanii..tuliwategemea kuwa mkifika huko mijadala itakuwa kugombania "activities za kufanya" kumbe mnagombania mafwedha..mmhh hatarii..hivi ninyi wapinzani lini mtatuonyesha uzalendo wenu kwa vitendo badala ya maneno?????
Kweli kabisa, chukueni hizo posho kimyakimya fanyeni mambo ya maendeleo katika majimbo yenu ili wananchi watambue kweli wana wawakilishi. Kuziacha huko ndiyo zitatafutiwa matumizi mengine yasikuwa na manufaa. Hii itasaidia kutoa nafasi mijadala mingine iendelee.Tutafika tu
ReplyDeletenami naungana mkono na mdau hapo juu. hiyo posho yenu muichukue iwekwe katika mfuko mmoja ambao mtauita "OPPOSITION ALLOWANCE FUND" baada ya hapo muamue nini mfanye na hiyo posho kama ni kujenga chuo au kujenga barabara ya umbali wa Km. kadhaa ni juu yetnu. hapo kweli tutaona mko serious alkini kuniambia eti Katibu wa Bunge aweke fomu za kusaini mahudhurio tofauti hapao mmechemesha hebu chakachueni fikra yenu kwanza. Mie nawajua wabunge wau upinzani hapo asilimia 90 wanapenda posho. so alternatively mnaweza kuchkua hiyo posho kila mtu katika akaunti yake kama kawaida then majiwekea utaratibu wa kuchangia huo mfuko wenu na ni kila kichwa sh. 100,000 kwa siku itakuwa bomba.
ReplyDeletemwisho wa mwaka mnakusanya mihela yenu mnafanyia jambo la maendeleo ambalo ni tangible. msilazimishane wakati wengine roho zinawauma na posho zao. watashindwa kusaidia wananchi wao majimboni na nawahakikishia MTAPOTEZA 2015.
But all in all mawazo yenu bomba chakachueni ya yangu na ya yule ninayemuunga mkoo kule juu mtapata CREAM ambayo hata mkiila na kuwapa wengine wanameza bila wasiwasi.
Kazeni mwendo tupo pamoja msiwe vichwa vigumu.
jamani nimewapigia hesabu CHADEMA tu. mimi ni huyo mwenye mchango hapo juu. wao kama wabunge 49 x 100,000 x 28= 137,200,000 hii ni posho yao ya sitting kwa siku 28 sasa ukiipiga mara miezi mitatu wanayokaa bunge la bajeti = 411,600,000.sasa je wakichangishana vijisenti hivyo katika mkutano mmoja wa bunge la bajeti si watakuwa mbali. nasisitiza wasirudishe posho ng'o bali wafungue mfuko "OPPOSITION ALLOWANCE FUND" kwa kuchakia kiasi hicho. kweli kwa milioni 411 watafanya jambo madarasa, mabwani mangapi watajenga. nadhani watafika mbali.Na wakiungwa mkono na wabunge wengine wa CUF, NCCR na TLP watakuwa mbali mno. itapendeza sana
ReplyDeleteMdau
ROK
mnaosema mbowe ana uwezo wa kuwa na magari zaidi ya hayo ni kweli lakini hapa tunaongelea mali za serikali sio za mbowe!!
ReplyDeleteWAtu hata kufikiria ni shida!unasema mambo ambayo hata hayana maana!!
Hapo suala kubwa ni mali za umma.kuhusu yeye kuna na helikopter huo ni mfuko wake binafsi!
Kimsingi, Kambi rasmi ya upinzani bungeni chini ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)imeonyesha moyo wa dhati na dira kuelekea kuleta mageuzi ya kweli katika maisha ya Mtanzania.
ReplyDeleteCCM ifikie hatua mseme ukweli kuwa Chadema wamewazidi kete, nathibitisha katika hoja kuu zifuatazo:
1. Angalia uppuuzi alioandika Ndugu Nape Nnauye kuhusu bajeti ya Upinzani Bungeni.
2. Angalia uppuzi aliofanya ndugu yangu Shukuru Kawambwa kuhusu mgomo wa UDOM(Ndugu watanzania ni Jamaa huyu alikuja Desemba mwaka jana pale UDOM-Uwanja wa block 3 na akaahidi kwa umma kuwa wanafunzi wote wataenda field then mwezi wa tano anakuja anawaambia hamtaenda field=unategemea nini kitatotokea.
3.Angalia upuuzi wa Bulaya eti Rais wa federal wa UDOM NI UVCCM (Peleka kcmc kwa operashion ya ubongo).
4.Nyara za serikali zinapitishwa uwanja wa ndege( serikali inakwambia tunafuatilia).
5.Magufuli anataka aboreshe miji, pinda na kikwete wanakwambia haina ulazima kwa sasa bomoabomoa
6. Sijasahau ile scandal ya EPAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA, Tamuuuuu kwa ccccmmm na kama ni chungu je KAGODA NI NANI?
7.Angalia yule waziri aliyeapa kuwa mabomu hayatalipuka tena na tena (ndani ya mwaka mmoja nini kilitokea gongo la mboto)
8.Kuna yule kiongozi wa serikali alisema nchi ina element ya udini kisa tu kaona mambo hayamuendei vizuri-NIMTAJEEEEEEE-CCCCMMMMMMM SI MNAJUAAAAA AU MPAKA MJIVUE GAMBA?
9.Llle songi la mauji Arsha, nyamongo? au tamuuuuuu kwa ccmmmmmmmmmmmmm
10.CCCCCMMMMMMMMMMMMM Mnalo tena mnalo, mtaisoma mwakaa huuuuuuuuuuuuuu
"GOD BLESS DK.WILBROAD SLAAAAA, CCCCMMMM SEMA SLAAAAAAAAAAAA, RUDIA TENA SLAAAAAAAA. HAPA RAHA TUUUUUUU TENA SLAAAAAAAAAAAAAAA"
MWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Tatizo lenu CHADEMA mnataka kuingia Ikulu kwa gharama yoyote ile. Na mbaya zaidi, mmejawa no Choyo, Chuki, na Tamaa. Huu UCHU wa madaraka mlonao Unanipa wasiwasi!
ReplyDeleteWANGIEZUMZIA NA POSHO ZA VIKAO SERIKALINI. MAMBO YA SAFARI ZA BUSINESS CLASS MBONA MADOGO HAYO!
ReplyDeleteHAWAELEWI MAANA YA 'INTERNATIONAL DEMONSTRATION EFFECT' -- UKIWASAFIRISHA MAWAZIRI WA NCHI MBILI KWENDA KWENYE NEGOTIANTIONS LAZIMA UINGIE GHARAMA YA KUMFANYA WA KWAKO AKAE SAWA KI-SAKOLOJIA. AKIWA ECONOMY NA MWENZAKE AWE BUSINESS, WAKISHUKA TU KWENEYE NDEGE ASHAANZA KUMWITA MWENZIE 'MZEE' - TUTAFIKA HAPO!
SUALA LA MASHANGINGI NAKUBALI - LAND CRUZER MKONGA ZATOSHA - VILE VILE KUONDOA GARI NA MADEREVA WA KUHUDUMIA NYUMBANI KWA WAHESHIMIWA WAZIRI.
POSHO ZA VIKAO VYA BUNGE TUWE MAKINI NAZO - MAANA UNAWEZA KUSHANGAA MAHUDHURIO YAKAWA MADOGO MNO BUNGENI. HILI TWENDE NALO TARATIBU.
MAGARI YA WABUNGE YAENDELEE KUKOPESHWA - PUNDE UTAKUTA DOCUMENTS ZA BUNGE ZIMEACHWA KWENYE BASI LA ABOUD/SIMBA MTOTO, AU KENYE SOKO LA KUKU WA KIENYEJI. TUWE WAANGALIFU NA HOJA HIZI - TUSIKURUPUKE TU KWA KUTAFUTA UMAARUFU.
MWISHO HONGERA MBOWE KWA KUARUDISHIA SHANGINGI LAO - IWEJE SPIKA AENDESHWE KWENYE MERCEDEZ S CLASS LATEST KABISA NA WEWE UPEWE SHANGINGI LA MWAKA 47?
BRAVO! SASA INGIA NA ILE S CLASS YENYE HADHI YAKO! AU SIKU MOJAMOJA NA HELIKOPTA YAKO YA KUKODI. WATAKUKOMA SASA!
we laiza koko acha fix hapo juu.
ReplyDeleteMbowe/Upinzani unasema hakuna sababu ya Mashangingi na si gari kwa mmbunge wa kambi ya Upinzani. kwa nini utumie gari la kifahari na bei mbaya kama alilorudisha Mbowe wakati kuna magari ya kawaida kama VW, prado ndogo au hata Rav 4. It make sense kidogo na si migari kama hiyo. Wewe ni mbumbumbu maana huoni jinsi madereva wanavyochezea magari ya serikali mitaani, bar nk hata wale wa taasisi nyeti.
Lazima kuwe na mabadiliko. Sasa nataka mbowe atupie picha nje ya nchi tuone mabalozi na maofisa wetu wanaishije.
Mbowe mnafiki, magari yake mabovu kawakodisha CHADEMA wakati wa kampeni siku moja 100,000/- kila gari. Kila gari ilitumika siku 100, kila gari imeingiza 10,000,000/-. Matengenezo yote gharama kwa CHADEMA. Baada ya uchaguzi kawauzia CHADEMA hayo magari. Kila gari kapata faida 30,000,000/-. Hizo pesa zote zinatoka kwenye ruzuku ambazo ni fedha ya mlipa kodi! Hamumdanganyi mtu. CCM Oyeeeee!!
ReplyDeleteKwa nini viongozi wetu hawasomi alama za nyakati? Ni vigumu sana kuingia akilini kwamba nchi yenye matatizo makubwa kama yetu, mfano, jana tuu nimeongea na ndugu Bongo nikaambiwa hakuna umeme sababu ya mgao!! Ambao mpo na mimi huku ughaibuni mtajua nini maana ya kukosa umeme japo sekunde tuu! Viongozi wetu hamjui kuwa umeme ndio basis ya uchumi na maendeleo? Ngonjera zote za uwekezaji na nyimbo lukuki kuhusu maisha bora itabakia kuwa ndoto iwapo changes hazitakuwepo! CDM kazeni buti mlete maendeleo ya kweli katika nchi yetu!
ReplyDeleteJG, Stadskanaal, Netherlands
Ni kweli inapendeza. lakini kumbukeni kuna wabunge wengine hawana gari wala mkokoteni kweli watarudisha? na huwakika wakupata tena baada ya miaka mitano hana. najuwa kabisa kuna wapizani wengine roho zinawahuma wanajuta wanajiona wana mkosi miaka yote miposho ilikuwa mingi lakini mwaka huu zito kiwingu. weeeh zito wengine miposho kama hiyo wanajengea chumba ndogo nyumba badala ya kutoa misaada kwa wananchi ambao wamewapa kura zao. watu wazima kazi zao ni totozi wakifika bungeni. nawafagilia sana chadema lakini siyo mwanachama wenu lakini kwenye kweli tuko pamoja. mwisho naomba pesa chukuweni mpelekeni majimboni mwenu mkasomeshee watoto wasio na uwezo au yatima. By Pilingu - Nangumbu-Lindi
ReplyDeleteNA ILE MILION MIA MBILI NI RUZUKU KWA AJILI YA KAMPENI YA UCHAGUZI ULIOPITA AMBAPO CCM WAMEJICHOTEA MILION MIA NANE UNALIJUA HILO? HEBO!!!
ReplyDeleteNA WE ANOYMOUS WA 09:16:00AM HIVI KWANINI WATZ. MNAKUWA RAINI RAINI HIVI WEWE CCM IMEFANYA NINI TANGU NCHI IPATE UHURU,KIZA NCHI NZIMA,MGAO WA MAJI ,UFINYU WA AJIRA,MAFISADI NDO HAO HAO THATS WHY WANALINDANA.TUTAFIKA WAPI?NAILE POSHO NI KWA WATUMISHI WA SERIKALI WOTE WAACHE, UNAJUA KWA MWAKA ZITAKUSANYWA MABILIONI MANGAPI POSHO NDO MANAKE.NDO MAENDELEO SIO KURUDI NYAMA.NYAU WE.MDAU mlalahoi mwenye hasira kali.
ReplyDelete