Picha wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wakiwa wanataka kumbeba mwenyekiti wao Mh. Freeman Mbowe wakati alipokuwa anatoka kwenye lango la chumba cha mahakama mara baada ya kesi yake kuhairishwa 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Mh.  Zitto Kabwe akiwasili  mahakamani Arusha leo kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe

Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema akiwasili mahakamani hapo

Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia kesi hiyo kwa nje


Picha zote na Habari na Woinde 
Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Mh.  Freeman Mbowe, ameachiwa huru kwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha  mara baada ya kuonekana kuwa hakuwa na kosa lolote la kujibu mahakamani hapo.
  
Pia mdhamini wa awali wa mwenyekiti huyo  Julius Margwe amekataliwa na mahakama hiyo kwa kushidwa   kutii Mahakama na kumtaka mthamini mwingine ambaye angeweza kufuata sheria za mahakama  bila kuzikiuka.

Mahakama hiyo ya hakimu mkazi Arusha ilimkubali mthamini mwngine ambaye alijitokeza  kulichukua gurudumu hilo  la mshitakiwa huyo,ambapo John Bayo ambaye ni Diwani wa kata ya Elerai wa CHADEMA ndie aliyekabidhiwa gurudumu hilo la kuwa mdhamini mpya wa Mh. Mbowe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa akizungumza  Mahakamani hapo, alisema kuwa kutokana na mdhamini huyo kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani hapo, kwa sababu za kuwa na yeye anakabiliwa na kesi Mahakama ya Mwanzo Maromboso, hivyo mahakama imeamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

 Alisema kuwa mahakama imeona kuwa mdhamini huyu ana makosa na hata hawezi kueleza
Alisema kuwa mbali na kueleza uongo Mahakamani hapo kuwa alikuwa akifika mahakamani hapo, bado mahakama haina sababu kuwa naye sababu tayari ana kesi ya jinai ambayo hatma yake haifahamiki.

Kwa upande wa mshitakiwa ambaye ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Freeman  Mbowe Hakimu alisema ni kweli mahakama iliruhusu washitakiwa wabunge wahudhurie kikao cha bunge la bajeti na hivyo hawana tatiz na Mh. Mbowe, ila kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri ya kukamatwa kwake.

Aidha Mh. Magesa alibainisha kuwa mahakama hiyo inaendelea kuwapa ruhusa washitakiwa wote ambao ni wabunge kutohudhuria mahakamani hapo hadi pale ambapo kikoa cha bunge kitamalizika ila aliwasisitiza wathamini wa washitakiwa hao kuhudhuria mahakamani hapa kila siku ambapo tarehe ya kesi imepangwa

Kabla ya Hakimu huyo kutoa maamuzi hayo, Hakimu huyo alimpa nafasi mdhamini wa Mbowe Julius Margwe na kumtaka aeleze sababu za kutofika mahakamani.

Akijibu maswali ya mahakamani hapo, Julius aliiambia Mahakama kuwa Mei 27 mwaka huu, hakufika sababu alikuwa na kesi Mahakama ya Mwanzo Maromboso na Mei 30 alifika mahakamani ila kwa sababu mahakama haikumpa nafasi kusema lolote hakujitokeza.

Naye Wakili upande wa Utetezi, Method Kimomogoro, aliiomba Mahakama hiyo, kuondoa amri ya kukamatwa kwa Mbowe  na kutaka apewe dhamana yake ya awali, ili aweze kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti ambalo yeye ni kiongozi wa kambi ya Upinzani.

Aidha Wakili  huyo alimtetea mdhamini wa Mbowe kwa kutofika mahakamani na kusema kuwa hiyo ipo kwa kila mtu na hata wao kama mawakili wanasahahu tarehe za mahakama na ndiyo sababu huwa wanaandika, hivyo kwa   mwananchi wa kawaida ni lazima wasahahu tarehee.

Pia alipinga kauli ya wakili wa serikali ya kutaka mahakama impe onyo Mbowe  kwa sababu kosa siyo lake na Mahakama ilimpa udhuru Aprili 29 mwaka huu, kesi hiyo ilipotajwa na kutoa sababu ya kuwa watakuwa katika vikao vya bunge la Bajeti na kuomba mahakama imrejeshee dhamana yake ya awali.

Upande wa Wakili wa serikali Juma Ramadhani, aliiomba mahakama hiyo itoe onyo kali kwa mshitakiwa kwa kutofika mahakamani hapo na pia kumtaka mshitakiwa huyo na wenzake wawe na mawasiliano ya karibu na wadhamini wao, ili wasikosekane wanapotakiwa  mahakamani hapo.
  
Alisema kuwa kuhusu dhamana ya Mbowe hana mashaka nayo, isipokuwa mdhamini wake hana uhakika na hajuwi nini anafanya, hivyo hafai kuwa amdhamini na kuomba mahakama kutoa uamuzi wa mdhamini huyo.

Baada ya pande hizo zote kuongea Hakimu alimwachia huru kw adhamana Mh. Freeman Mbowe na kutoa idhini ya kuendelea na bunge la bajeti hadi hapo Juni 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Baada ya  Freeman Mbowe, kuachiwa huru na mahakama  alipata nafasi ya kuzungumza   na wafuasi waliofurika mahakamani hapo na waandishi wa habari, kwenye viwanja vya mahakama hiyo ambapo alisema anapendakuwashukuru sana wananchi na viongozi wa chadema jinsi walivyojitokeza kumpa ushirikiano na kusema kuwa hiyo ni moja wapo ya kuwaonyesha serikalil  nini maana ya nguvu ya umma.

 Alisema kuwa anasikitishwa sana na kitendo ambacho serikali wamekufanya cha kutumia nguvu kubwa kumlinda yeye na kumsafirisha usiku wa  huku akiwa chini ya ulinzi mkubwa kama kwamba yeye alikuwa ni gaidi ambaye alikuwa na silaha .

 “Mimi nilijipeleka mwenyewe polisi sasa kama kweli ningekuwa wa kukimbia ningejipeleka? Sasa wao hawajaona hayo yote haitoshi wameamua kutumia nguvu kubwa sana maana wakati wakinipeleka uwanja wa ndege walikuwa na polisi wengi sana zaidi ya 50 yaani utadhani ni gaidi anapelekwa alafu ndege ya kubeba watu mia ndo wameniweka mimi,  wakati hayo mafuta wangeyaweka ata kwenye kutengeneza vitanda vya hospitali. Wanatumia vibaya kodi za wananchi “alisema Mbowe.

Alisema kuwa serikali ilitumia ndege ya jeshi, ambayo ina uwezo wa kubeba watu 100, ambayo ilichukua watu watatu yaani yeye, Kamishina wa Polisi kanda kanda ya Ilala na Kamishna wa Polisi wa kikosi cha kuzuia ghasia wa Tanzania hadi KIA usiku wa majira ya  saa 9.00.

Pia alisema mbali na kusafirishwa kwa ndege hiyo kubwa, pia kulikuwa na magari nane ya FFU ambao walikuwa na mabomu na silaha kama wanasindikiza mhalifu. Mbowe alisema kuwa kimsingi yeye hakuwa ana kosa la kukamatwa na ndiyo sababu mahakama haikumuhoji hata swali moja kwa sababu waliona mwenye shida ni mdhamini wake.

Alisema hakukuwa na sababu za msingi za kutumia rasilimali za serikali ambayo ni mali za umma na kumsindikiza kama muhalifu mtu ambaye hakuwa na hata na silaha. Alisema kwamba anachoshukuru ni Polisi kutomfanyia unyama wowote na walikaa naye vizuri, isipokuwa alinyimwa haki yake ya msingi ya kuwa na uhuru wa kuwasiliana na watu. Mara baada ya kesi hiyo kumalizika wananchi walimbeba kiongozi waho kwa juu huku wakiimba nyimbo za furaha.

Katika kesi hiyo ilihudhuriwa na wabunge 13 wa CHADEMA ambao ni Zito Kabwe, Halima Mdee, GodBleess Lema, Suzan Kiwanga,Ezekia Wenje, Christina Lisu,Paulina Gekulu,Israel Natse, Suzana Lyimo, Joseph Mbilinyi, Rahya Ibrahimu, ambaye ni Mbunge toka Pemba, Joyce Mukya na  Joseph Selasini.

Wakati hayo yakiendelea mara baada ya kuachiw ahuru mshitakiwa huyo, kulilipuka kelele za shangwe, huku wakiimba nyimbo za kumkataa Meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    Kaka Ankali Mithupu tunakuvulia kofia sie wadau wako hapa Wichita kwani mitandao yote ya Bongo tunakuta ni blog yaku tu yenye latest news kama hii ya Mbowe. Wengine wataishia kukopi na kujifanya ya kwao. Keep it up Chum. We are really, really proud of you and ur blog> sijui vyombo vingine vina mpang gani wa kwenda sambamba na habari kama wewe>>> Wao akili mgando wanafikiria keshooooo habari za leo. Wape pole zao...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Pole sana shujaa wetu Mbowe. Hii ndiyo Tz iliyojaa unyanyasaji. Kumbe walijua huna hata kosa lakini kwa vile wanapenda kudhoofisha upinzani wakaamua wakudhalilishe! Ipo siku hilo joka litaachia ngazi na haki itarudi.

    Nashukuru kwamba CUF nao wameona uonevu huo. Keep it up. Mkishirikiana mtaweza kuliondoa hilo joka. Tunawatakia ushindani mzuri wa kisisasa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2011

    ninachoweza kusema ni kwamba wananchi wanatakiwa kutafakari sana ni viongozi wa aina gani walio wachagua kilasiku ni mahakamani maandamano nk.
    je wanatatua vipi matatizo majimboni kwao.
    je nigharama kiasi gani wanazo tumia kwa kufuatana kuja kusikiliza kesi ya mbowe na kuacha kutekeleza wajibu wao majimboni kwao. wasifikiri watu wanavyo kusanyika wanafurahia hiyo hali wanakwenda kusikiliza na kuwacheka kwani wamegeuka katuni miongoni mwa wananchi. ASANTENI.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2011

    Hivi niwaulize tu hii serikali ya ccm kama wana akili hivi ni kweli mnachukua ndege ya watu mia moja mnamleta nayo muheshimiwa mahakamani angali mmeshamuona ni mualifu tena dizaini ya ugaidi. aisee Mbowe wewe ni maarufu mtu wangu. asante kaka H/some boy kijana mwenye elimu, kijana machachari, vijana wenye mvuto wa kusimama na kuongea mbele ya watu wanaume wapo CHADEMA akiongea unassimka kwani ni mwanaume kaingia na kuongea. hana tabia za kike. weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  5. MuadilifuJune 06, 2011

    Michu, hizi picha umesafisha kwa majenta nini?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2011

    mbowe yuko juu wala hatukuachi tuko tayari kuingia barabarani inapobidi. SHUJAA WETU POLE SANA MUNGU YUKO UPANDE WAKO.

    ReplyDelete
  7. Mimi hii hainiingii kichwani Watanzania Tax payer tunataka tujue Total cost ya Tukio zima kuanzia malipo ya ulinzi wa mbowe na transport ya ndenge mpaka Arusha. I dont know the law of freedom of information zinavyofanya kazi hapo Tanzania kwa sasa. Lakini kama wote hapo juu walivyosema this is waste of Tax payer Money and need to stop immediately.Mambo mengi yamekuwa yakifanyika kienyeji sana hapo bongo KIKWETE ameshidwa kuonyesha LEADERSHIP how to run the Government. natsikia uchungu sana wa nchi yangu ninayoipenda kushindwa kuwatumikia wananchi wake.2015 isn't too far CCM going to End. As we know mihimili ya uongozi Mahakama bunge na Executive power inatakiwa kufanya kazi independent lakini nashangaa Tanzania ni tofauti as we can prove in this issue. Huyo Judge Magessa acting in favor of Govrnment not governed by law. Ndio maana we need A NEW KATIBA to stop this MADNESS. CCM Tumechoka.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2011

    kusema laukweli hata kama chadema isipochukua nchi lakini wanawatia jambajamba ccm vijana wachadema ni ngangari kinoma hawa ndio wanaitwa wanaume wa shoka hawataki ujinga hatakidogo ccm hata wafanyeje cha moto wanakiona tu pamoja na kushika dola na kuwapiga wanachama wa chadema lakini wanakipata fresh ya shamba big up mbowe dume la mbegu wafuasi tuko nyuma yako hakuna kurudi nyuma mbele kwa mbele mpaka hawa manyangau waachie ngazi hata roma haikujegwa kwa siku moja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...