Habari na picha na Woinde Shizza
Globu ya Jamii, Arusha
Mheshimiwa Freeman Mbowe ameachiwa kwa dhamana asubuhi hii baada ya kufikishwa mahakamani Arusha akitokea Dar es salaam ambako alikamatwa na polisi na kuwekwa rumande kwa siku mbili kabla ya kusafirishwa saa tisa usiku kwa ndege ya jeshi chini ya ulinzi mkali.

![]() |
Mh. Freeman Mbowe akiwa kabwebwa na wafuasi wa CHADEMA mara baada ya kesi yake kuahirishwa leo |
Mh. Mbowe anakabiliwa na mashtaka ya kufanya mkutano bila ya ruhusa, na fujo, baada ya maandamano yaliyofanywa mapema mwaka huu huko Arusha.
Mahakama hiyo awali iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Bw. Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini) na wengine Bi. Josephine Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba wakamatwe.
Pamoja na washtakiwa na wadhamini wao kutofika mahakamani ikiwemo Mawakili wao, Method Kimomogolo na Bw. Albert Msando pia hawakuwepo mahakamani wakati hati hiyo inatolewa, lakini washitakiwa Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwakamatwe kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.
Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Nai Steven, Mathias Valerian, John Materu, Daniel Titus, Juma Samuel, Walter Mushi, Peter Marua na Erick Makona.
Hakimu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo wala mdhamini wake, hivyo Ofisa Inchaji wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama ni si vinginevyo.

“Wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo wanapatikana na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu. Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa Inchaji amkamate na kufikishwa mahakamani,” Hakimu Magesa aliamuru
Habari zinasema pamoja na kuwepo umati mkubwa wa watu mahakamani, ambako pia ulinzi ulikuwa umeimarishwa maradufu, hakujatokea vurugu ya aina yoyote hadi tunakwenda hewani hivi sasa na kwamba kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 25 mwaka huu. Pia amembadilisha mdhamini wake.

Akiongea na waandishi baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mh. Mbowe amewashukuru viongozi wenzake, wanachama wa CHADEMA na watu wote waliosaidia kwa njia moja ama nyingine hadi kufikia hapo.
Polisi wana maigizo kweli.
ReplyDeleteSasa nani aliyelipa hela za helicopter/ndege ya kumpeleka mbowe arusha.Polisi mlijua ataachiwa huru tena na mkaendelea kupoteza pesa kumshikilia na kumpeleka arusha, je ni wananchi wangapi wanapata hiyo lifti ya ndege za polisi
Anony wa kwanza. Hapo ndio ujue jinsi nchi yetu wasivyojali matumizi ya pesa kana kwamba zipo tu mahali zikiisha unaenda kuchota. Maendeleo wameshindwa kuwapelekea wananchi lakini kwenye vitu rahisi kama hivyo wanatumia mapesa mengi for nothing!
ReplyDelete