![]() |
Mh. Kalonzo Musyoka, Makamu wa Rais wa Kenya akipokea maelezo juu ya bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa Tanzania |
Mataifa ya Afrika ambayo yana uwakilishi hapa Nairobi, kwa pamoja yaliandhimisha siku ya Afrika tarehe 25 Mei, 2011 sherehe ambazo zilifanyika katika ofisi za Uwakilishi wa Serikali ya Kenya katika Umoja wa Mataifa (Kenya Mission to UNON).
Haya ni maadhimisho ya 48 tangu kuazishwa kwa siku hii, ambapo kimsingi mataifa ya Afrika hutumia siku hii kama njia mojawapo ya kutathmini mafanikio ambayo yameweza kufikiwa katika Nyanja mbalimbali.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mh. Kalaozo Musyoka, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Afrika 2011 ni kuhamasisha na kuwawezesha vijana kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika yalienda sambamba na maonyesho ambapo kila nchi ilipata fursa ya kuonesha vitu mbalimbali.
![]() |
Mmoja wa wageni akipokea maelezo kutoka kwa Bibi Joy Njelango |
Katika maonesho hayo banda la Tanzania ambalo siku hiyo lilitia fora liliratibiwa ipasavyo na Ubalozi wa Tanzania Nairobi na lilisheheni bidhaa mbalimbali ambazo zinatengenezwa nchini Tanzania.
Bidhaa ambazo zilionyeshwa ni pamoja na hizi zifuatazo:
![]() |
Mgeni akiwa kavutiwa na Dodoma Wine |
(1) Kahawa
(2) Majani ya chai ya aina mbalimbali kama vile African Pride, Chai Bora, Green Lebel, Kilimanjaro, Simba chai.
(3) Wine za aina mbalimbali kama vile Rosier, Rose Wine ambayo inatengenezwa na CETAWICO LTD, Dodoma, G. MERLINI WINE ambayo inatengenezwa ma Missionaries of the Precious Blood, Miyuji Dodoma, Tanganyika vineyards – Dodoma, Dompo Red wine kutoka Alko Vintages Dodoma, Annunciata Sweet white Grape wine, inayotengenezwa na Missionaries of the Precious Blood, Miyuji, Dodoma, Buffalo wine na Rhino.
(4) Konyagi
![]() |
Wageni kibao walitembelea banda letu |
(5) Khanga, Batiki, na nguo zilizoshonwa kwa kutumia khanga na batiki ambazo zilipatikana kutoka Mitindo House Dar es salaam.
(6) Mbuzi ya kukunia nazi pamoja na nazi.
![]() |
Kikosi kazi cha Ubalozi wetu Nairobi |
Kimsingi Banda la Tanzania lilipata mvuto mkubwa na wengi walionyesha wazi kupenda wine ya Watanzania japo wageni wengi walionyesha wazi kutokuwa na taarifa kwamba Tanzania pia inatengeneza wine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...