Bro. Misupu pole na majukumu ya kutuhabarisha kupitia blog yako. Naomba unisaidie kupata utaalamu wa kisheria kuhusu issue ifuatayo;


Jana jioni nikiwa na ndugu yangu tukibadilishana mawazo kwenye ka-grocery nje ya nyumba yake alitokea mzungu (from one of the Scandinavian countries – naihifadhi kwa sasa!)ambaye alikuwa akifoka kwa kudharau nchi yetu pamoja na viongozi waliopo madarakani kama Presidaa, IGP, Kova, etc.


Baada ya muda si mrefu yule mzungu alimfuata ndugu yangu na kuanza kumsemesha vitu ambavyo havieleweki pamoja na kejeli mbalimbali...ndugu yangu kwa kuwa ni mtu mstaarabu alimwagiza muhudumu aende kwenye meza aliyokuwa amekaa mzungu huyo na kuwaomba wale aliokuwa amefuatana (waTZ) na mzungu huyo wamchukue kwani alikuwa anajiabisha yeye pamoja na taifa letu. 


 Lakini hawakufanya hivyo na baada ya dakika kama 2 hivi yule mzungu alikuja tena kwenye meza yetu na kuanza kumchapa makofi ndugu yangu pamoja na kumvunjia mali zake kama vile miwani, nk.


Haikuishia hapo yule mzungu alitoa kisu na kuanza kutishia umati uliokuwa hapo. baada vurugu nyingi na msaada wa majirani tulifanikiwa kumkamata na kumpeleka polisi.


yaliyojiri polisi; ndugu yangu alitoa maelezo na akapata RB ya "shambulio na kuharibu mali" lakini cha kushangaza pale polisi kulionekana kuwa na directives kupitia radio call ambayo ilikuwa loud and clear telling the junior polisi nini cha kufanya.


Kama mjuavyo polisi si pa kukimbilia walalahoi, ndugu yangu anahitaji msaada wa kisheria wa kuweza kufanikisha kupata mali zake pamoja na damage aliyoipata ya kupigwa na foreigner kwenye nchi yake.


Vithibitisho: tulikabidhi polisi vithibitisho kama kisu, vipande vya miwani ya ndugu yangu pia tulifanikiwa kupata jina na picha ya mtuhumiwa pamoja na silaha (kisu).
Naomba msaada!


=================================


Kaka Michuzi;
Tuwape pole hawa jamaa.
Nimeongea na wapiganaji wenzangu wa Legal and Human Rights Centre (LHRC) pale Kijitonyama, wameahidi kutoa legal aid ya msaada wa sheria katika suala hili.
Kwasababu taarifa walizotoa hazijitoshelezi, basi, nawaalika kufika kwenye ofisi - Justice Lugakingira House, Kijitonyama ili kupewa msaada huo. Amuulizie Rodrick kwa muda wa kazi.

Pole na kazi mpiganaji


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2011

    Kwa nini hamkumchangia na kumpiga makofi na ngumi huyo mzungu? Habari ya polisi na mahakama ni safari ndefu ambayo inaweza kuingiliwa na mambo mengi na haki isitendeke!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2011

    mdau hilo swala halina haja ya kulitafutia ufumbuzi... weka picha ya mzungu anapatikana wapi na sisi tutamuonesha kuwa hatutawaliwi bado.
    muda umefika wa kutowanyenyekea hawa nguruwe... pambaaaf sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2011

    Katika nchi hii nikawaida kitu kama hicho. Wazalendo hawathaminiwi siku zote. Huyo si mgeni wa kwanza kufanya hivyo na serikali isipoonyesha ujasiri wake wa kutetea raia wake wanapokuwa na haki basi watanzania wataendelea kujichukulia sheria mikononi mwao ambapo ni kitu kibaya sana. Ndugu zangu wanasheria/wanaharakati msaidieni huyo jamaa kupata haki yake. Ukiukwaji wa haki za binadamu imejionyesha wazi hasa pale mtu mweupe anapofanya atakavyo kwa kuvunja amani iliyopo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2011

    nimesoma hi habari imeniuma sana kama mbongo nilie ughaibun hao wazungu huku kwao wanatufanya kama sisi weusi tunadhiki sana SASA nashanga huko bongo polici wanawababaikia sana hao niwashenzi sana naomba sheria ichukue mkondo wake alipe mali zahuyo jamaa pia apate na kifungo mbona wao kwao wanatufungu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2011

    pole sana kwa yaliyowapata. ingekuwa vyema kama ungesema unahitaji msaada upi kwani kwa maelezo yako hujasema kama umenyimwa hiyo haki. endelea kufuatilia endapo utakosa hiyo haki basi utafute msaada.

    pili: hadi huyo mgeni anawachapa vibao mlikuwa wapi. mnaogopa ngozi nyeupe? mlitakiwa kumtandika nyie. mnajidharaulisha ndio maana nao wanatudharau. mlitakiwa kutoa kichapo cha nguvu iwe fundisho kwao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2011

    Poleni kwa uungwana wenu huyo mzungu hakutakiwa apelekwe polisi, angeanza kwa hospitali tena ICU. Pambafu si unajua njaa za hao walinzi wetu k*&*$^. zao. wanajua kuzua maandamano tu!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2011

    Hahaha inabidi nicheke maana ingekuwa UK kitu cha mwanzo ni yule raia wa kigeni angaliletewa polisi sio chini ya kumi, suala lake la kwanza lingekuwa kujibu anaishi vipi hapo UK, baada tena ndio kuangalia mengineyo. Na usiombe ukashikwa usiku wa Ijumaa, maana utakaa mahabusu mpaka jumatatu itapokuwa wazi idara ya uhamiaji. Halafu kama jaji ataamua uende jela basi baada ya kifungu ni kuwa unashindikizwa mpaka uwanja wa ndege na mabausa wanne mpaka kwenye kiti cha ndege inayeelekea Dar es Salaam na wawili wataongozana na wewe mpaka Dar na kukukabidhi kwa uhamiaji wa TZ. Ama kweli hatuna nchi. Misaada hiyo!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2011

    mngemchoma moto huyo mkoloni mmekosea kumpeleka polisi mkiwa mnajua huko azima kaburu achiwe huru. kibaka akiba kuku anachomwa moto. maskini wadanganyika

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 21, 2011

    haiwezekani tu mtu kukurupuka na kuanza kukuchapa vibao lazima kuwe na kitu ambacho hujakieleza umekificha na kama hakuna kitu basi huyo mzungu ni mwenzawazimu anatakiwa apimwe akili yake au alikuwa under influence of drugs,nijuavyo mimi wazungu wanaogopa sana jela za nje na kwao maana wanajua shuruba yake,lazima kuna kitu kingine kama wewe hujui muulize huyo ndugu yako vizuri what's behind the curtain,nina uhakika kuna kitu tu....mwisho kama nyie ndio mlianza basi ni haki yenu kuchapwa vibao ndani ya nchi yenu ingawa sheria haimruhusu mtu kumpiga mwingine na haimruhusu mtu kumchokoza mwingine......simtetei mzungu ila ukiangalia sana maelezo yako hapo napata hisia nyie ndio wakorofi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 21, 2011

    Lakini alichokuwa anatukania hata ninyi mliona kilikuwa na ukweli. Alitukana IGP na afande Kovu, sasa mliweza kulinganisha maana ya matusi yake na mlichotendewa polisi? Mmeanda kushtaki badala yake issue imegeuzwa dili ninyi mnaonekana hamna haki.

    Saa zingine hawa jamaa wanatukana kutokana na ujinga waliokumbana nao kutoka kwa viongozi. Japo simshabikii katika kuwapiga wenye nchi yao. Nchi imeoza acheni wanaoambiwa ukweli waambiwe.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2011

    Penye wengi hapakosi jambo, jamaniii waswahili nyie msikurupuke tu bila fikra. Kama mtihami basi mmefeli, kama wengi wetu tulivyofeli na mpaka sasa tunafaka kazi za care na casual huko mamtoni. Stori nzima ni ya upande mmoja tu, hamjayasikia ya mzungu anayeelezewa mnakurupuka kutoa hukumu, nyie ndio mkimwona mtu kapita mbio mtaani kwenu alafu mkasikia sauti wa mwizi huyo mnatoka mbio na kumpiga mawe huyo jamaa aliyepita mbio, kumbe huyo ndie aliyeibiwa na vibaka wamemgeuzia kibano. Mtakoma
    mdau Alex Bura, dar

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 21, 2011

    Kwa mtazamo wangu kuna kitu mdau hajakielezea ambacho ndio mwanzowa huyo mdhungu kutoa maneno ya hovyo. LAKINI hakuna uhalali wa aina yoyote wa mtu yoyote kujichukulia sheria mikononi. KWAHIYO BASI alieanzisha kichapo na yeye alistaili kichapo halafu polisi wangefanya kazi yao ya upelelezi kwa nini mlikuwa mnachapana. QED

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 21, 2011

    Hapo ni Daresalama?
    Njoo nikupe ya Babati
    Gari la abiria liligonga na kung'oa sidemirror ya gari la wachina. Wachina wakaita polisi, na polisi wakaona raia hawana hatia wakaamuru gari lipeleke abiria Arusha. Wachina wakagoma eti lisiondoke mpaka kesi iishe. Baada ya dereva kutoa gari wachina wakalipiga mawe kioo cha nyuma kikapasuka
    Muziki munee: wananchi walianza waliwatwanga wachina na wawili kati ya 20 walikuwa na hali mbaya, walipelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu ya kina.
    Sasa ninyi wa Dar na ujanja eti unafuata sheria......tandika watu hata kama ni kesho waache dharau.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 21, 2011

    nakubaliana na badhi ya wachangiaji hata kama huyu mtz alianze yey kumchokoza huyu mzungu azingetakiwa ampige na kumwaaribia mali yake hizo ni dharau wanafikiri ni enzi ya ukoloni mungempiga kisawasawa halafu mkifikisha polisi hata sheria isipochukuliwa basi mzungu angebaki na maumifu sasa mlikuwa mnapinga nini namefanya nini mnanitia hasira kama hamjampiga mmefanya ujinga san au mliogopa kwa sababu ngozi nyeupe

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 21, 2011

    amekucha nawewesiumchape yani wewe anakupiga unamwangaliatu,hebu tutoleeni hii mada hapa ,kama mwanaume mzima umekaa kimya hadi umechapwa eti kisa mzungu,angekua mwafrika kakuchapa ungekaa kimya kweli sikingenuka sasa kipi kimekushinda kukinukisha kwa mzungu?
    Alafu nyie wanaume wote mmekaa kimya mwenzenu anapigwa ghraaaaaaaaaa mmeniudhiii
    nyie mnadhani polisi wa bongo na njaa yote hiyo wakihongwa watawaona nyie? chapatu huko huko then mnaheshimiana

    ReplyDelete
  16. Bajeti ya Tanzania(Mishahara ya wa-serikali, jeshi, walimu, Polisi NGO's...) kwa ujumla 65% inatoka kwenye kodi anayolipa huyo Mzungu huko kwao.Ulaya..
    Sasa kwanini asikuchape Makofi, tena kwa confidence nyingi kabisa akijua popote utakapoenda yeye ndiyo Boss wao??

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 21, 2011

    Babu hapa kuna kitu umetuficha, huwezi ukafatwa na kuanza kutukanwa pamoja na kupigwa bila sababu, Mimi nipo US na wazungu sio watu wakupigana ngumi labda dharau na fitna. Mimi nahisi huo uongo wako ndio umekufanya Polisi wasikutendee haki

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 21, 2011

    Anajuwa Nchi yake itamlinda.
    Tena angekuwa kwao angetumia silaa kubwa..
    Watu weusi zaidi ya 14 walipigwa risasi kule Scandic nchi kwenye mabano, na hakuna aliyewashikia bango kwa unyama walio ufanya.
    Umaskini mbaya...Nhi zetu zinzsibitisha dhahiri kwamba hazifuatiliii haki za raia wake.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 21, 2011

    Watanzania tuache kukimbilia ubaguzi pasipo kutumia akili. Hii ni kesi ya Jinai. Kuna kitu wamemfanyia huyo mzungu ndio maana akafanya alichofanya. Hata sisi wenyeji (Watanzania) ukipeleka kesi polisi ya kumshitaki mtu lazima polisi wachekeche kwanza kujua ukweli uko wapi. Na mimi ni shahidi kesi nyingi polisi huwa wanasuluhisha na kuzimaliza wenyewe.

    NI MAKOSA KUONEA WAGENI ETI KWA SABABU WAKO NCHINI KWENU. MKUMBUKE WATANZANIA NA NYIE MTAANZA KWENDA NCHI ZA WATU. HAPO NDIO MTAELEWA MAANA YA USTAARABU.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 21, 2011

    Mtanzania akikupigia story asilimia 90 anayosema ni uongo na asilimia 10 ndio ukweli!

    ReplyDelete
  21. MATANGALUJune 21, 2011

    Wewe uliyeleta habari na hao wenzako wote nikiwakamapa nawachapeni makofi. Pumbaavu kabisa nyie. Mmesoma shule gani nyinyi? hivi hamkusoma au kuelewa kisa cha Kibanga ampiga mkoloni? au ndiyo wale wale mnaosoma bila kuelewa? mnasoma ili muwatishe wasiokuwa na bahati ya kupelekwa shule?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 22, 2011

    Heri wewe umechapwa vijikofi ukavunjiwa mawani. Wenzako kule Mara walipigwa risasi kabisa. lakini kama ulikula vyake lazima ulipe. Huyo mzungu demu au jike? I bet ni jike.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 22, 2011

    Alivyofanya mzungu ni safi sana, asilimia kubwa ya wabongo ni washenzi na hawasarifiki....ingekuwa vizuri zaidi angemtemea na mate ya uso

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...