Ndugu, Jamaa, na Marafiki, Watanzania wote;
Kwa masikitiko makubwa tunawataarifu ya kwamba, tumepokea habari za msiba wa Baba ya mwenzetu Doreen Mangia. Msiba umetokea leo huko nyumbani, Moshi Tanzania.
Marehemu Thomas Mangia amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mke wa marehemu(Mama Mangia), yuko hapa Marekani kwa wanae. Mama Mangia na wanae, wanahitaji kwenda nyumbani kwa ajili ya mazishi ya mzee wetu. Kwa mantiki hiyo basi, tunaombwa Watanzania wote, marafiki, ndugu, na jamaa, tumchangie Mama yetu na familia yake, ili waweze kuwahi mazishi huko nyumbani. Gharama za kuwasafirisha wafiwa zimefika roughly $ 8000.
Tunawaomba wote, kwa moyo wa upendo na utoaji, tusaidiane ili tukamilishe safari ya wafiwa ambao ni Watanzania wenzetu. Tunatanguliza shukurani za dhati kwa michango yenu. Wanaoweza kuwatembelea wafiwa mnakaribishwa nyumbani kwa Doreen Mangia kwenye address hapo chini. Kama hutaweza kufika North Carolina, unaweza kutuma mchango wako kwa;
Doreen Mangia;
Coastal Federal Credit Union
routing # 253175494
acc # 00702605300050
Marehemu Thomas Mangia amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mke wa marehemu(Mama Mangia), yuko hapa Marekani kwa wanae. Mama Mangia na wanae, wanahitaji kwenda nyumbani kwa ajili ya mazishi ya mzee wetu. Kwa mantiki hiyo basi, tunaombwa Watanzania wote, marafiki, ndugu, na jamaa, tumchangie Mama yetu na familia yake, ili waweze kuwahi mazishi huko nyumbani. Gharama za kuwasafirisha wafiwa zimefika roughly $ 8000.
Tunawaomba wote, kwa moyo wa upendo na utoaji, tusaidiane ili tukamilishe safari ya wafiwa ambao ni Watanzania wenzetu. Tunatanguliza shukurani za dhati kwa michango yenu. Wanaoweza kuwatembelea wafiwa mnakaribishwa nyumbani kwa Doreen Mangia kwenye address hapo chini. Kama hutaweza kufika North Carolina, unaweza kutuma mchango wako kwa;
Doreen Mangia;
Coastal Federal Credit Union
routing # 253175494
acc # 00702605300050
kwa maelezo ya ziada wasiliana na;
Doreen Mangia 919 264 5944
Pendo Mathias 919 815 4596
Moses Igbiinobia (Doreen's Husband) 919 414 36 51.
Msiba upo nyumbani kwa Doreen;
440 F Woods of North bend drive.
Raleigh NC, 27609.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe.
Asanteni.
Kuchangiana wakati wa shida ni jambo jema. Lakini hii michango naona kama vile imezidi. Kwani huko US wanakaa bila kazi jamani. Pengine achangiwe Mama tu, vijana wajitutumue
ReplyDeletePoleni wafiwa.
ReplyDeleteHata mimi nafikiria kwa kuwa gharama inaonekana ni kubwa kwa wenyewe kumudu, basi angechangiwa mama atangulie kuzika, na wanae wakafuata baadaye.
HUU NI MSIBA MZITO KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WOTE.
ReplyDeleteTUNAOMBA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI, ILI KUFANIKISHA MAMA YETU MPENDWA (MAMA MANGIA)
NA FAMILIA WAWEZE WOTE KUWASILI MOSHI KWA MAZIKO YA BABA YETU MPENDWA ALIYE TUTOKA (MZEE THOMAS MANGIA).
KWA WALE WALIOPO HAPA NCHINI TANZANIA, MSIBA UTAKUWEPO MOSHI (KARANGA AREA) AND KWA WALE WALIOPO DAR ES SALAAM TUNAOMBA MUWASILISHE MICHANGO YENU KWA MZEE LYIMO PALE KIMARA-KOROGWE.
WOTE TUNAWAOMBA KUSHIRIKI NASI KATIKA WAKATI HUU MGUMU WA KUMUAGA MZEE WETU THOMAS MAGIA AKAPUMZIKE KWA AMANI.
**BWANA AMETOA, NA BWANA AMETWAA, JINA LA MUNGU LIBARIKIWE**
FROM: EDWIN BRUNO SHAYO (KILEO)
MJUKUU WA MAREHEMU.
Huyo mtoa maoni wa kwanza hajui maana ya msiba. Jamani msiba hautoi taarifa kuwa nitakuja siku na saa ipi. Usafiri wa mtu mmoja unaweza kukaribia dola za marekani 2000. Sasa hata kama mtu anafanya kazi, unaweza kukuta kiasi hicho ni mshahara wa miezi miwili ya mtu. Sasa tatizo kama hilo likimfika mtu kwa ghafla unafikiri kweli atakuwa na akiba ya kutosha kusafiri mpaka Moshi na Kurudi USA??? Tusipende kukatisha watu tamaa. Kama hauyajui maisha ya ughaibuni nyamaza! Wanaoyajua watachangia.
ReplyDeleteWaheshimiwa wapiga-box, me nadhani ni jambo jema kama mtaanzisha vyama vya kusaidiana katika shida na raha. Au hamuoni umuhimu wake? Live everyday as though it were your last, atleast one day you will be right. Poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteMdau mla vumbi.
Wewe ananymous wa kwanza sidhani kama ni vizuri kuanza kusema watu wanakaa bila kazi. Yeye katumia blogu kufikisha taarifa kwa ndugu, jamaa na marafiki. Watu kama ninyi mnaanza kutoa kauli negative na mchango hamtoi. Si ajabu akapata mchango zaidi ya hizo alizoomba toka kwa ndugu na marafiki wanaomfahamu, ambao hawana mawazo kama yako au ambao wao walishawasaidia. Hii tabia ya kuanza kutoa kauli zisizo nzuri wakati watu wana matatizo si nzuri. Mimi nawapa pole wafiwa na Mungu atawajalia mambo yote yataisha salama, ndi dunia. Mambo ya "huko US mnakaa bila kazi" hayahusiani na hii.
ReplyDeleteHaitakuwa busara kumchangia mtu kwenda mazikoni. Bali michango iendelee kwa kurejesha maiti kwao TZ.
ReplyDeleteThis is NOT ok. Hivi kweli tumefikia kuombana hata mchango mtu aende kwao msibani? Whatever happened to keeping an emergency fund sawa na gharama za miezi sita kuishi i.e. including rent/mortgage/food/clothes etc? Hata huyo mama wanashindwa kumlipia? Samahani ila hiyo familia naona inajidhalilisha kuomba mchango kwa jamii nzima ya Marekani. Hata pakukopa hakuna? Kama wangejipanga ndugu na marafiki wa karibu ningeelewa. Hata sisi huku NY tunachangiana lakini sio kwenda kwa Michuzi na kutanga account # ili kila mtu ajitolee. Take responsibility for your own life people!
ReplyDeletesomeni ujumbe kama unaweza changia sawa kama huwezi acha, as simple as that
ReplyDeleteMisiba mingi imenitokea lakini sijawahi kuomba mtu anisaidie nauli! Kama msiba nzito natumia credit card. Mtu akifa hapa USA naona ni sawa kuomba hela ya kurejesha maiti lakini kuomba nauli, NO WAY tunaelekea wapi?
ReplyDeleteKwani huyo mama alipokuja marekani hakuwa na return ticket? Poleni san a wafiwa lakini mkisubiri michango mnaweza msiwahi Maziko.
ReplyDeletejamani jamani watanzania tuwe na huruma, mimi sioni ubaya kwa wao kuomba mchango!!!!!!!! kama huwezi kusaidia basi wache tu, sio kilazima.
ReplyDeletelakini huyu baba alikuwa ni mtu wa watu, na kifo chake ni cha ghafla mno, inasikitisha...
jamani watanzania msaidieni hata huyu mama mangia tu,akamzike mume wake. pls pls
mdau
Nakubaliana na wote wanaopinga kuchangia nauli ya kwenda msibani. Mchango wa kusafirisha maiti unakubalika; lakini wa tiketi ni kuvuka mipaka. Wataokwenda kuwapa pole hapo kwao wakatoa michango sawa; lakini ya kuanika kwenye blog hii ni kujidhalilisha! Kama alivosema mdau mmoja hapo juu, mama alipokwenda Marekani hakuwa na return ticket?
ReplyDelete