KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Nontsikelelo Sisulu, aliyekuwa mke wa mpigania uhuru wa Afrika Kusini, marehemu Walter Sisulu,katika Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa chama cha ANC, kufuatia kifo cha Mama Nontsikelelo Sisulu, mke wa aliyekuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini, Walter Sisulu.
Akuzungumza baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo ya kifo hicho, kwenye Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Dar es Salaam,Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, CCM imeguswa na kifo hicho kwa sababu mbali na kuwa mke wa mpigania uhuru, Mama Sisulu alikuwa mstari wa mbele kupigania haki na usawa wa binadamu.
Nape alisema, katika uhai wake, Mama Sisulu alitumia taaluma yake ya uuguzi kuwafundisha wauguzi wenzake ambao walihudumua wanaharakati waliokuwa katika mapambano ya kusaka uhuru wa Afrika Kusini.
Alisema, Mama sisulu atabaki kuwa mfano wa wapenda usawa wa binadamu duniani kwa sababu hata baada ya Afrika Kusini kupata uhuru, alikuwa miongoni mwa viongozi waliosimamia maridhiano ya kusahau madhila yaliyofanywa baina ya makaburu na raia wa Afrika kusini kabla ya uhuru.
Nape alisema, licha ya ukatili na ubaguzi wa rangi waliokuwa wakiufanya makaburu, lakini maelewano yaliyofanyika baada ya uhuru wa chini ya wanaharakati akiwemo Mama Sisulu wazungu hawakubaguliwa. Alisema matendo ya Mama Sisulu yatabakia kuwa mfano bora kwa wapinga ubaguzi na wapenda amani duniani ikiwemo Tanzania.


R I P OUR MUM.
ReplyDelete