Mzee mwinyi katika picha ya pamoja na watoto wawili pekee wanaoshiriki kupanda milima Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro 2011 kuchangia waathirika wa ukimwi iliyoandaliwa na Geita Gold Mining Company wikiendi ilopita
 Mzee Mwinyi akiwa na mkuu mkuu wa wilaya ya Hai Dk Norman Sigela (kulia) nja nmmoja wa viongozi wa Geita Gold Mining company wakati wa uzinduzi huo
Mzee Mwinyi akiwa ameambatana na mkewe mama Mwinyi pamoja na kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Meja Jenerali Said Kalembo na viongozi wengine wa Geita Gold wakipanda sehemu ya mlima Kilimanjaro kama uzinduzi wa Geita Gold Kilimanjaro Climb Challenge wikiendi hii. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2011

    Not bad for a mzee who is 86 years old. Mzee wetu A. H. Mwinyi, tunakutakia wewe na watu wote wa familia yako kila la heri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2011

    Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Asante kwa kutupa vyama vingi, TV huria, magazeti huria, uhuru wa kuongea na pia asante sana kwa kufuta sheria ya watu kutiwa kizuizini bila kufikishwa mahakamani (Preventive Detention Act) kuwafungua watu kutoka jela kwa kuwa walikamatwa na sabuni miche mitatu au colgate 4, kutuletea nguo Kasulu wakati tulikuwa tunavaa magunia na watoto wanatembea uchi kati ya 1983-1985. Ubarikiwe mzee wetu. Amen. J Ruhitana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2011

    Mmhh, kanipa moyo. Ijapokuwa kwetu ni Marangu mtoni bado sijapanda Kilimankyaro. Nia yangu ni kuukwea mlima huu kabla sijafikia miaka 40. Yes we can.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2011

    Ndugu Ankal, fundisho la leo? Mtu unaweza kutoa mchango kwa jamii hata kama una miaka tisini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2011

    Maisha yenye MCHANGO.

    Na ndio mambo ya maana.

    Sio ufisadi.

    Kwanza mafisadi wengi wanakufa mapema!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 20, 2011

    Viongozi wote wanamapungufu yao ikiwa pamoja na Mzee wetu Mwinyi lakini ukweli utabaaki palepale mzee Mwinyi kama kula kala na wananchi na pia nikweli mpenda watu wake sincerely....!you always been rembered n been missed too.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 20, 2011

    MZEE RUHSA HATA IWEJE WEWE WETU DAM DAM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...