Mzee mwinyi katika picha ya pamoja na watoto wawili pekee wanaoshiriki kupanda milima Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro 2011 kuchangia waathirika wa ukimwi iliyoandaliwa na Geita Gold Mining Company wikiendi ilopita
Mzee Mwinyi akiwa na mkuu mkuu wa wilaya ya Hai Dk Norman Sigela (kulia) nja nmmoja wa viongozi wa Geita Gold Mining company wakati wa uzinduzi huo
Mzee Mwinyi akiwa ameambatana na mkewe mama Mwinyi pamoja na kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Meja Jenerali Said Kalembo na viongozi wengine wa Geita Gold wakipanda sehemu ya mlima Kilimanjaro kama uzinduzi wa Geita Gold Kilimanjaro Climb Challenge wikiendi hii. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,
Not bad for a mzee who is 86 years old. Mzee wetu A. H. Mwinyi, tunakutakia wewe na watu wote wa familia yako kila la heri.
ReplyDeleteRais mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Asante kwa kutupa vyama vingi, TV huria, magazeti huria, uhuru wa kuongea na pia asante sana kwa kufuta sheria ya watu kutiwa kizuizini bila kufikishwa mahakamani (Preventive Detention Act) kuwafungua watu kutoka jela kwa kuwa walikamatwa na sabuni miche mitatu au colgate 4, kutuletea nguo Kasulu wakati tulikuwa tunavaa magunia na watoto wanatembea uchi kati ya 1983-1985. Ubarikiwe mzee wetu. Amen. J Ruhitana.
ReplyDeleteMmhh, kanipa moyo. Ijapokuwa kwetu ni Marangu mtoni bado sijapanda Kilimankyaro. Nia yangu ni kuukwea mlima huu kabla sijafikia miaka 40. Yes we can.
ReplyDeleteNdugu Ankal, fundisho la leo? Mtu unaweza kutoa mchango kwa jamii hata kama una miaka tisini.
ReplyDeleteMaisha yenye MCHANGO.
ReplyDeleteNa ndio mambo ya maana.
Sio ufisadi.
Kwanza mafisadi wengi wanakufa mapema!
Viongozi wote wanamapungufu yao ikiwa pamoja na Mzee wetu Mwinyi lakini ukweli utabaaki palepale mzee Mwinyi kama kula kala na wananchi na pia nikweli mpenda watu wake sincerely....!you always been rembered n been missed too.
ReplyDeleteMZEE RUHSA HATA IWEJE WEWE WETU DAM DAM
ReplyDelete