Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,David Minja (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza udhamini wa mashindano ya mchezo wa Pool Taifa.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo na kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),David Minja akicheza mchezo wa Pool ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa mashindano hayo yatakayoanza hivi karibuni.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kwa mara nyingine udhamini wake katika mashindano ya Taifa ya mchezo wa Pool mwaka 2011. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 30 mwezi June 2011 katika ngazi za Mikoa na inatarajiwa kumalizika july 17,2011.

Bia ya Safari Lager ndio mdhamini mkuu wa mashindano haya.

Akitangaza udhamini wa mashindano ya mwaka huu, Mkurugenzi mkuu wa Masoko wa TBL Bw David Minja alisema TBL kupitia Safari lager imekuwa mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imeweza kuleta mapinduzi ya kweli katika mchezo huu, hivyo ni dhamira ya bia ya Safari na TBL kiujumla kuendelea kudhamini mashindano haya ya Taifa na mengi mengineyo ya mchezo wa pool hapa nchini. 

Udhamini huu unaanzia ngazi ya mikoa hadi fainali ambazo kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi July 2011.

Akizungumzia zawadi za mwaka huu meneja wa bia ya Safari Bw Oscar Shelukindo alisema kuwa udhamini wa mwaka huu umeongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma, ikiwa ni pamoja na zawadi za washindi.

Akiweka wazi aina za zawadi ambazo washindi wa mwaka huu watapata katika ngazi za mikoa na Taifa alisema kumekuwa na ongezeko la wastani wa asilimia arobaini (40%) kulinganisha na mwaka jana “tumeongeza sehemu ya zawadi kwa kiwango kikubwa ili kuweza kutoa nafasi kwa washindi kupata nafasi ya kushinda kiwango kikubwa cha fedha ili kiweze kuwasaidia katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo. 

Sote tunatambua kuwa mchezo wa Pool kwa sasa umegeuka kuwa sehemu ya ajira nasi tunaendelea kuboresha na kuwawezesha washindi kunufaika na kiwango cha juu cha zawadi”alisema bwana Shelukindo.

ZAWADI NGAZI YA MKOA


Akiongelea uendeshaji wa mashindano ya mwaka huu, Katibu wa chama cha Pool Taifa Bw. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu yataendelea kushirikisha mikoa 14 kama ilivyokuwa mwaka jana na tutaendelea na ushiriki wa mchezaji mmoja mmoja pia (singles) kwa wanaume na wanawake kama ilvyokuwa mwanzo”.

Bw. Amos aliitaja mikoa itakayoshiriki kwa mwaka huu kuwa ni Kagera,Shinyanga, Mbeya,Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Mwanza, Iringa, Manyara, Morogoro,Kinondoni, Ilala na Temeke.

Katika ngazi ya mikoa mashindano yataendeshwa kwa club na hatimae Mikoa yote itaunda timu zao za mikoa ambazo zitawakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa zitakazofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa mwezi wa July mwaka huu. 

Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Isaac Togocho alisema “Taswira ya mchezo wa pool hapa nchini imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inavutia vijana wa kaliba mbalimbali kwani si mchezo wa kupotezea muda tena kama Wengi walivyoudhania, bali ni miongoni mwa michezo inayokua kwa kasi kubwa na kuwapatia kipato wachezaji na vijana kwa ujumla. 

Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa kuweza kuleta mapinduzi haya makubwa katika mchezo wa Pool hapa nchini. Ni dhahiri kuwa mchango wa mdhamini ndio umeleta matunda yote haya ambayo tunayaona hii leo TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2011

    Hizi zawadi zimepangwa kwa ubaguzi mkubwa sana wa kijinsia kwanini wanawake walipwe pesa pungufu na wanaume na wote wanacheza mchezo mmoja? Gender discrimination is the main problem in African countries. Women you need to fight about your rights.
    This is not fair at all!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2011

    Ninakubaliana na mtuma maoni wa kwanza. Ni nani aliyepanga hizo zawadi? Mimi ni mwanaume na ubaguzi huu ninaona hauna nafasi katika jamii yetu inabidi tuungane pamoja kuupinga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...