Simba ilikuwa  nyuma kwa goli 1-0 goli ambalo Kipa Juma Kaseja aliokoa shuti ya Motema Pembe  kwenye chaki na refa akaonesha kati akisema ni goli katika  kipindi cha kwanza. Baada ya mapumziko Motema Pemba wanapata bao la pili dakika ya 57

Huko Nigeria mabao ni kama huko DRC ambapo Vijana wa U-23 wako nyuma kwa bao moja na pia ni mapumziko sasa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. simba tumefungwa goli la pili kizembe dak 15. 2nd half

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2011

    .......vijana stars imepigwa 3-0, na simba mpaka sasa imepigwa 2-0

    Timu ya vijana ni nzuri sema kocha wake hana viwango, Julio, wakutoka ...anaongea sana!

    simba nao, ni bora walivyokuwa na Phiri, Huyu mganda anawapotezea!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2011

    Simba imetolewa 0-2

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2011

    kiwango bado hamna tunacheza kwenye vyombo vya habari sisi washindi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2011

    What's up with final scores????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2011

    Sababu zimeshaanza, oo! liliokolewa! Na la pili Je? OO! Saababu ya lile la kwanza, Mara ooo! walitufanyia fitna...Mpira kana kwamba mpira unachezwa kwa mdomo!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2011

    Tanzania wamelala 3-0. Michuzi naona unaogopa ku-update news. Nigeria wamesonga mbele kwa 3-1 aggr.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2011

    Mkuu wa Libeneke mbona ume-mute matekeo ya hizo timu zetu? Inamaana mpira haujaisha mpaka saa hii? Tuambie tu hata kama tutapata machungu. Tumeshazoea mbona.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2011

    Bora Simba wametoka maana fitina zao dhidi ya TP Mazembe zilikuwa za kitoto sana.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 20, 2011

    Ndio kusema Simba wametolewa kwa mara ya 3 mfululizo katika michuano ile ile ndani ya mwaka mmoja au? Kwanza na TP Mazembe, pili na Wydad Casablanca, na tatu na DC Motema Pembe, si ndio? Hii si rekodi mpya katika michuano duniani kwa upande wa soka????

    Duh, aibu kwa Tanzania, yaani hata jitihada za utalii zinazofanywa kwa kutumia pesa inayotokana na kodi za wananchi hazizai matunda kwa taswira mbaya mbaya kama hizi kwa taifa. Kwenye michezo ovyo, burudani (hasa BBA) mikosi, na siasa ndio uozo kabisa!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 20, 2011

    INANIUMA SANA HATA KUONGELEA SUALA HILI....bora kulia tu na kunyamaza!!...kila mwaka timu hazisongi mbele....bullshit kabisa!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 20, 2011

    simba kwishni

    ReplyDelete
  13. Dewji - MANISPAAJune 20, 2011

    Haha ha ha ! duh! jamaa wa takwimu nakukubali. Ni kweli Simba wametoka tena kwa aibu kubwa sana. jumla ya goli walizopigwa ni nyingi sana. pole zao na hao wanaomwona Kaseja kipa na kummwagia sifa kila siku. wenzake wakishaona hivyo wanahama timu. yeye anang'ang'ana kwenye timu hiyo ambayo ni mbovu. Kwa kweli Simba mmetutia aibu watanzania. sasa njooni kwenye Kagame Cup mfanye fitna zenu.
    Ila mkiweza Kateni Rufaa kama kawaida yenu. kama hamna hoja nawadokeza kama mlivyozoea kudokezwa, REFA alikuwa kanywa bia 2 za baridi. haya kateni Rufaa kama kawaida yenu! watu weeeeeeeeweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
    Timu ya vijana poleni. watanzania wote tupo pamoja nanyi. mjipange kwa tukio lingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...