Ankal,  Issa Michuzi,
Salaam! Habari za Kazi?
Tunakupongeza kwa kazi nzuri ya kuwahabarisha wananchi wa Tanzania kwa habari mbalimbali.
Sisi WANANCHI wa Mivumoni Block 5&6 Kata ya WAZO Wilaya ya Kinondoni tunaomba utuhabarishie kwa kuitoa taarifa hii kwenye Blog yako ya Jamii ili Wahusika na  UMMA kwa ujumla waweze kujua jambo hili kama walikuwa hawajalijua na kulichukulia hatua za utekelezaji.
Tunaambatanisha taarifa yetu hii pamoja na picha za eneo husika.
Asante sana,
Sisi Wananchi wa Mivumoni Block 5&6
(B56 Mivumoni Community Development Association- B56 MICODA)

Kusoma barua ya wazi ya  wananchi hawa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2011

    Pole mtanzania, nasi tuna tatizo kama hilo maeneo ya Gezaulole, Kigamboni, Michuzi namimi nitakutumia picha za eneo zinazoonyesha uharibifu unaofanyika na hatua tulizochukua.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2011

    This is sinful
    Man is so destructive of his own environment, and mismanages natural resources.But there must be laws and regulations that make sure that such acts do not take place, there must be agencies that protect the environment, as somebody said, even in Tanzania.
    I have faith Michuzi will alert the concerned
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2011

    MICODA big up kwa sana kwa jitihada za kukomesha uharibifu wa mazingira. Nakumbuka kuna issue kama hiyo iliwahi kujitokeza eneo la Bunju A miaka ya nyuma kwenye shamba la mzee mmoja. Alifanikiwa kukomesha tabia hiyo kwa fundisho kuu! Alichokifanya ni kuchimba shimo kubwa kwenye njia ambayo malori yalikuwa yakipita katikati ya shamba lake...kisha akalirunika kwa miti milaini na kuweka majani makavu juu yake pamoja na maeneo yanayolizunguka shimo hilo. Siku ya siku Fuso tani 7(a.k.a bajaji) ikawa inaingia usiku kuchota mchanga ..tahamaki gari zima likadumbukia kwenye lile shimo la mtego basi hapo ndiyo ikawa mwisho wa kuchimba mchanga eneo hilo. Kwangu niliiona hiyo ni effective method ya kuhakikisha uharibifu unakoma maana hadi leo hajathubutu mtu kusokelea shamba lile!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...