Salaam Sana Mjomba Ankal,

Kwanza tunakushukuru sana na pole kwa kazi nzito na nzuri ya kutupatia khabari motomoto na zinazotufikia kwa wakati muafaka sisi tulieko nje ya Tanzania.

Je zama za viongozi au watu mbalimbali kuonekana wameshikilia simu za mkononi haswa kwenye shughuli za maana zitaisha lini? Mi naona nchi zilizoendelea huwezi kumuona kiongozi anahudhuria mahali akiwa ameshikilia simu ya mkononi.

Tanzania imeshakuwa na simu za mikononi siku nyingi kiasi hata mababu na mabibi zetu wanazo vijijini. Tafadhali fanya kampeni hii ili tuwe tumevuka hizi zama za kale tuende mbele.

 Kuitwa simu za viganjani siyo kwamba mtu aigandishe mkononi saa zote bali ni rahisi kuitoa mfukoni na kuiweka kiganjani kupokea. Kuna vijimfuko vingi kwa ajili ya kuwekeka simu au tupa mfukoni ikilia toa ongea rudisha mfukoni.
--
Patrick

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2011

    Asalaam aleykum ndugu Patrick
    Naomba radhi
    Nataka kukuarifu kuwa kuna kitu kinaitwa personal choice.You or anyone else cant tell other people what to do, especially if they are not breaking the law of the land.Wataka bunge ipitishe sheria kuwalazimisha watu watie simu zao mifukoni? Tanzania tuna tabia ya kujishughulisha na mambo yasiyo na maana na yashio na faida ye yote.Ni hiyari ya mtu akitaka kunyoa au kusuka
    Samahani

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2011

    SIMU BONGO MTAMA,MWANANGU NA USHAMBA ULIOTUJAA KUANZIA VIONGOZI MPAKA WAZALENDO HUKO VJJN

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2011

    Ndugu yangu uliye nje ya nchi, sio kila kitu wanachofanya wazungu ni cha kuiga. Kushika simu mkononi sio tatizo labda ulete hoja ya kisayansi ndio tutakuelewa. Mimi nafikiri ni jambo la kheri kila mtu akafanya maisha yake kadiri anavyofurahia kuliko kufanya jambo usilolifurahia eti kwa vile wazungu wanafanya hivyo. Tuwe na utamaduni wa kupenda vyakwetu ili mradi havina madhara mabaya.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2011

    Nakubaliana na wewe kabisa huu ni ujinga na ushamba AJABU sana utawakuta hata mawaziri na kijisimu mkononi kwenye maongezi ya maana sana wakati huo simu haitumiki ila kaishika mkononi inachukiza sana hii kitu ila bado watu washamba sana bongo

    simu kwao ni show na kujionesha ni simu gani yuko nayo, wanasahau kuwa simu nikukusaidia wewe kuzungumza na ukiwa huitumii iweke sehemu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 19, 2011

    Bwana Patrick asante kama umeliona hilo nami pia uwa linanikela sana yaani utakuta mtu yupo kwenye shughuli za maana lakini simu ipo mikononi au yupo bissy nasimu au kubonyeza bonyeza kujifanya anatuma ujumbe au kujifanya anasoma ujumbe lakini ni ustaarabu wakaida hata ungekuwa na simu ya galama kiasi gani siku hizi kila mtu anayo hata na wanao kaa vijijini wanazo ,jirekebisheni wenye tabia hiyo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 19, 2011

    Yaani Patrick umeongoa kitu ambayo ipo moyoni kwangu. Hivi kwanini watu wanapenda kushika simu mkononi huku wanaongea kwenye hadhira? Waziri na akili zake unamkuta anahojiwa na TV station eti kashika simu mkononi. Huo si ustaarabu. Sijui waafrica tukoje hatuzoei tu hizo simu?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 19, 2011

    Patrick, hujaeleza tatizo wakishikilia mkononi ni nini mpaka ipigwe kampeni ya kuwafanya waache? Bongo kuna vibaka kila pahali, ukiweka mfukoni wanajichukulia kiulaiiini!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 19, 2011

    Someni Namba 6 hapo chini....

    Source: http://careerplanning.about.com/od/workplacesurvival/tp/cell_phone.htm

    Having your cell phone at work can be useful but it can also be very disruptive. Your friends and family can reach you anytime, anywhere, which can be annoying.
    When you're on your own time, the choice to turn off your cell phone is entirely yours. When it comes to using your cell phone at work, however, you have to be mindful of your co-workers and your boss, not to mention your own ability to get your job done. Here are some rules you should follow if you have your cell phone at work.


    1. Turn Your Cell Phone Ringer Off
    If you have your cell phone at work, it shouldn't ring. If you don't want to turn off your cell phone completely, at least set it to vibrate. The sounds of different ring tones going off all the time can be very annoying to others. In addition, you don't want your boss to know how often you get calls.


    2. Use Your Cell Phone Only for Important Calls
    If you have your cell phone at work, you should only use it for important calls. What should you classify as an important call? The school nurse calling to say your child is ill, your child calling to say he's arrived home from school safely, and family emergencies that you must deal with immediately are important. Your friend calling to chat, your child calling to say the dog had an accident, or your mom calling to tell you your cousin Tilly is engaged should not be considered important.

    3. Let Your Cell Phone Calls Go to Voice Mail
    While you are at work if you are in doubt about whether an incoming call is important, let voice mail pick it up. It will take much less time to check your messages than it will to answer the call and then tell the caller you can't talk.

    4. Find a Private Place to Make Cell Phone Calls
    While it's okay to use your cell phone at work for private calls during breaks, don't stay at your desk. Find somewhere else to talk, where your conversation can't be overheard, even if what you're discussing isn't personal. You may be on a break but your co-workers have a job to do.

    5. Don't Bring Your Cell Phone Into the Restroom ... Ever
    This rule should apply to using your cell phone at work or anywhere. Why? Well, if you must ask — you never know who's in there; the person on the other end of the line will hear bathroom sounds, e.g., toilets flushing; it is an invasion of your co-workers' privacy.

    6. Don't Bring Your Cell Phone to Meetings
    Even if you have your cell phone set to vibrate, if you receive a call you will be tempted to see who it's from. This is not only rude, it is a clear signal to your boss that your mind isn't 100 percent on your job. All calls can wait until your meeting is over or until there is a break. Remember, there was a time before we had cell phones.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 19, 2011

    Bongo simu za mikononi ndio kila mtu anaweza kuwa nayo na mawasiliano ni rahisi. Ukitaka simu za kwenye magari, majumbani na maofisini ni kuwa hakuna. Ofisini kwangu hata simu za mezani hakuna au hazifanyi kazi, watu wote wanategemea mawasiliano kwa simu za mikononi kwa hiyo kila mtu ameizoea simu ya mikononi kuliko kitu chochote. Huku TZ hatuna uwezo wa kumiliki wagari au kwenda holiday kwa hivyo pesa zetu tunaziwekesha kwenye simu na ukweli sasa huna wa kumwambia akawacha simu yake nyumbani au akaweza mfukoni. Tuwapongeze makampuni ya simu kuwa huduma pekee nchi inayopatikana ni simu. Hongera mitandaooooooooooooooooooo!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 19, 2011

    uko kwenye press conference simu mezani ya nini?

    ReplyDelete
  11. nshimimana aka dumisaneJuly 19, 2011

    ningependa kumshauri mdau alitoa tuta kwamba, hayo ni maamuzi binafsi, acha vurugu. unakuja kasi.

    - - -
    buffalo,
    new york

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 19, 2011

    Mh mi sijui hii ni mjadala wa nini.... HATUNA UMEME TUJADILI HILO NA SI KINGINEWE MPAKA KIELEWEKE TAFADHALI. TUAMKE TUACHE U

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 19, 2011

    UMEME KWANZA KILA KITU STOP. NO NONSENSE PLS

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 19, 2011

    THIS IS COMPLETELY NONSENSE topic. KILA MTU ANAJUA NAMNA YA KUJIHESHIMU MWENYEWE. NA NINA HAKIKA HATA HAO WAHESHIMIWA WANAFAHAMU UTARATIBU KUWA WANATAKIWA KUZIMA SIMU WANAPOKUWA SEHEMU KAMA MIKUTANONI.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 19, 2011

    Halafu utamkuta anasimu Tatu, ana vodacom ambayo wanaiita vodafone sometimes, Zain ana malizia na tigo. Zote mezani wakati wa press conference. Ukikuta ni Kamanda basi atakuwa na radio call as well.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 20, 2011

    aaaah wabongo ndio mana tunakufa masikini..yani matatizo yote tuliyonayo mnawaza habari za kushika simu...mmekosa cha kufanya ndio mana mnapata muda wa kuwa na mawazo ya fulani kafanya nini na kwanini...mimi hapa ni mwenyekiti wa bodi nipo kwenye kikao ngoja niwashe simu yangu nicheze game pambafuuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...