Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Mh. Mansoor Yussuf Himid amesema mfumo wa muundo wa Serikali mbili kwa sasa ni butu. Amependekeza kuwepo kwa muundo wa Serikali tatu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Makaazi Maji na Nishati leo katika Baraza la Wawakilishi, Waziri Mansoor alisema umefika wakati kufikiria Serikali tatu kwa maslahi ya Wananchi wote.
“Mheshimiwa Spika, mfumo wa Serikali mbili ni butu na haufai…sasa basi twende katika Serikali tatu” Alisema Waziri Mansoor.
Alisema katika dunia ya leo ni ile yenye kusikiliza maoni ya umma, hivyo tabia ya vitisho dhidi ya watu wanaotoa maoni haina nafasi kabisa, matamshi hayo yanaonekana kama kujibu maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta Bungeni aliyesema kwamba hoja ya Serikali tatu ni kutaka kuua Muungano.
Akichangia mjadala huo Sitta alisema siku ambayo Watanzania wataamua kuwa na serikali tatu za muungano, itakuwa ndiyo tiketi ya kuuvunja muungano huo.
"Kuunda tena Tanganyika ni kutengeneza mbia mwingine atakayekuwa anashindana na Zanzibar," alisema Sitta.
Alifafanua kuwa hali hiyo itajenga mazingira ya mvutano kwa serikali ya Tanganyika na Zanzibar wa kila mmoja kupigania maslahi yake na Serikali ya Muungano haitakuwa na nguvu kwa sababu uwepo wake utategemea pande hizo mbili.
“Mimi simtaji mtu,lakini inaonekana fikra zao ni za zamani kutisha tisha watu, yale maneno ni ya kupotosha zipo sheria za kimataifa kuhusu Territory Water na matumizi ya rasilimali, mambo ya mipaka yameelezwa sana” Alisema Waziri Mansoor.
Alisema marekebisho ya Katiba ya Muungano kwa Wazanzibari maana yake ni kujadili Articles of Union na ni vyema tuwaelimishe wananchi wetu wakati ukifika waweze kuitumia vyema fursa hiyo.
Waziri huyo alisisitza msimamo wake kwamba mafuta na gesi asilia sio suala la Muungano na ni lazima yakabakia kwa maslahi ya Wazanzibari.
“Makubaliano yetu ni kuyatoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano” Alisisitiza Waziri huyo na kuongeza kwamba kuzungumzia mafuta na gesi kuwa ya Muungano ni dhambi kubwa.
Kauli ya Waziri huyo inakubaliana na hoja iliyowahi kutolewa na kundi la Wabunge 55 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maarufu kwa jina la “G 55” lilipotaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika mwaka 1993.
Hoja hiyo ilizimwa na marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambaye mbali ya kuwatuhumu Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi kwa wakati ule, Holice Kolimba na John Samwel Malecela kwa kumshauri vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi.
Kutokana na suala hilo, Rais Mwinyi alivunja Baraza la Mawaziri na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Kolimba alihojiwa na Chama chake.
Hadi sasa msimamo wa CCM katika muundo wa Muungano ni kuwa na Serikali mbili ambazo mara kadhaa zimekuwa ikitetea msimamo huo katika mijadala mbalimbali.
Kwa nini tuwe na serikali tatu? Wapi tutatowa pesa za kuendesha serikali tatu? Kwa sasa tuna serikali mbili lakini the burden ya kuziendesha wanapewa vizazi vijavyo sababu tunakopa leo na kulipa ni kesho.
ReplyDeleteNadhani imefika muda wa kuwa na serikali MOJA yes MOJA and ZNZ and Tanzania iwe moja. Tubadilishe mfumo wa wakuu wa mikowa na tuweke magavana. Serikali hizi zijendeshe kwa pato lake lenyewe na serikali kuu isubsidize zile ambazo zinajiendesha kwa maendeleo zaidi.
TANGANYIKA NA ZANZIBAR ni serikali tatu
ReplyDeleteHAKUNA MAJOTROOOOO
MTABANAAAAAAAAAAAA NA MWISHOEEE MTAACHIA mnaogopa nini PUNGUZENI BAJETI.
Mbunge wa Zanzibar mmoja anachaguliwa na watu wachache ni uharibifu wa pesa za wananchi
Hivi Bara kwa nini tunang'ang'ania muungano hivyo?
ReplyDeletenini maana ya TANZANIA?...according to mimi ninavyoona neno tanzania limetokana na maneno tanganyika na zanzibar yaani TAN kutoka tanganyika na ZAN kutoka zanzibar sijui ile IA imetoka wapi lakini tanzania maana yake ni muungano wa nchi mbili na serikali zake na kupata nchi moja ya tanzania ambayo ina rais wa jamhuri ya muungano Dr Jakaya ambaye anachaguliwa na pande zote za muungano...lakini tatizo lililopo ni kuna serikali ya zanzibar na rais wake ambayo hai-make sense yeyote kuwepo, lakini kwa kuwa ipo basi tanganyika nayo iwe na serikali yake nayo ichague rais wake, tanganyika ina mali nyingi sana na siyo zanibar tuu pekee ndio ina mali. kuna mambo ya kushangaza ambayo huwa yakitaka kuamuliwa lazima pande zote mbili za muungano zihusishwe lakini always huwa inakusishwa pande moja ambayo ni zanzibar na serikali ya muungano maana hakuna serikali ya bara, wananchi lifikirieni sana swala hili.
ReplyDeleteMnajazana viongozi weeeeeeeeeeeeengi mnachofanya hakionekani. Zanzibar yenyewe kakisiwa kadogo tu kana: Bunge, mawaziri kibao, makatibu,sasa makamu raisi watatu, Afisi nyingi to lakini miaka nenda rudi kuko vile vile tu hakuna jipya zaidi ya hoteli za kitaliii
ReplyDeleteHakuna Zanzibar na Tanzanzia weka sawa maneno yako mtowa maoni namba moja ni Zanzibar na Tanganyika kwasababu ukisema Tanzania manaake ni Zanzibar na Tanganyika hapa lazima Tanganyika ifufuliwe upya
ReplyDeleteKwa sasa serekali inatumia pesa nyingi kwa kuendesha mfumo wa serekali mbili na kuwa wabunge wengi na sasa unataka serekali ya mfumo wa serekali tatu na wabunge waongezeke na pamoja na mawaziri wa serekali tatu, huko ni kutumia hovyo kodi za wanannchi, kwa nini tusiwe na serekali mmoja kwa masilie ya wote. je kwa nini Mh mansoor yusufu anaogelea hii na hapo hapo anajipiga goli kwa kusema hivyi mafuta na gesi inayopatikana zanzibar ni mali ya zenji people. kwa hivyo kama kuna maliasili yoyote inayotakana tanganyika ni maliasili ya watanganyika. haya ndio mwalimu alisema kuwa leo hii tukisema kuwe na serakali tatu kwa nini kesho wa zenji wasisema wanataka zanzibar ingawanyike kuwe na muungano wa wapemba na zenji. haya yote ni uchu wa madaraka. kwa sasa sijaona kiongozi yoyote tanzania hata kwa vyama vya upinzani yupo tayari kuongoza watanzania maana wote wana tamaa ya kuwa waziri au rais na badala ya kuwatumikia watanzania na kulete maendeleo kwa jumala .. asante uncle kwa kunipa nafasi hii ..
ReplyDeletehivi kwa nini hatuvunji huu muungano na hawa ma yakhe kwani tunafaidika na nini kutoka huko zanzibar ni bora tuwaachie kama Sudan ilivyoiwacha South sudan na ethiopia ilivyoiwacha Erietria...tuishi kwa raha bila ya kusikiliza kelele za wazanzibar
ReplyDeletewe need out tanganyika back, we miss our country...it was a bad idea to have this unity
ReplyDeletewazanzibari hata hawajui muungano ulikuwa na maana gani, muungano ulikuwa na nia ya kuwasaidia wao baada ya kumuondoa sultan walikuwa wanahaha hawajui nini cha kufanya nyerere akawabeba la sivyo walikuwa wachukuliwe na wakenya
ReplyDeleteNashangazwa sana kuona watu hapa wanasema kwa nini tunnang'ang'ania muungano eti wazanzbari mayakhe,na tunabebwa ? Pia munasema kuwa muungano hauna faida yoyote ? Ni kweli hauna faida yoyote na ndio maana wazanzbari hawautaki,na nyinyi watanganyika/watanzania ndio mumueuganda na ndio munao faidika.
ReplyDeleteFaida ya serikali tatu ni hizi.
Kwanza rasilimali za tanganyika zitasimamiwa na serikali yenu watanganyika,na mutakuwa na uraiya wenu na historia yetu ambayo ipo babu na mababu.
Pili kila upande kutakuwa na serikali yake ikijiamulia maamuzi yake na uwendeshaji wake.
Serikali yamuungano itapunguziwa mzigo mkubwa katika uwendeshaji kuliko tukiwa na mfumo huu tulio nao.
Haya tuangalie mifumo ya muungano wa nchi za wenzetu,wenzetu mbunge zao kama ERUPIAN union,wanahuzuria pale wote ni mawaziri tu,hakuna wabunge,kwa maana hiyo sisi serikali ya muungano ambayo ya shirikisho itakuwa na mawaziri wa pande mbili tanganyika na zanzibar,watakua wakijadili mabo yale ya muungano tu.
Pia rais wa muungano atakuwa anateuliwa na mawaziri ndani ya bunge la muungano,na raisi huyo lazima atokee kati ya mawaziri,sio sisi wananchi tupige kura kuteuwa rais wa muungano.
Rais wa muungano hatukuwa na powe r yoyote ile kama alivyo sasa hivi kama vile dictetor,hapana atakuwa hana nguvu hivyo isipokuwa kutatumika kisheria tu tena kwa kupitia makubaliano ya mawaziri hao ndio watakuwa kama wabunge wa muungano.
Uwiyano wa wabunge/mawaziri katika bunge la muungano utakuwa sawa sawa,pia itakuwa hakuna mdogo wala mkubwa,katika muungano huu,hapa ndio tutadumisha muungano.
Haya ndi mawazo yangu nahisi ndio tutaweza kumaliza kero za muungano na pia ile dana kuwa muungano unabeba sehemu moja na mwengine kufaidika,kila mtu atakuwa na national yake.Utambulisho wake.
Nassyin,
ReplyDeleteNaomba niseme kwamba uwezo wako wa kuangalia mambo ni mdogo au umekuwa brain washed popote pale ulipo. Unajua in every dollar that Tanzania is using leo 50 cents ni mkopo. Do you know that? Na hapa tuna s erikali mbili, sasa tukiweka serikali ya tatu operating cost yake unajua ni kiasi gani? Unaongeza expenditure wakati revenue yako ni constant? Unajua where the next fund will come? Unakopa..... Then you borrowed at 15% interest, na watakaolipa ni next generation.
Kwa nini tusiwe na serikali moja? One government then mikoa ipewe power ya kukusanya kodi, kuchanell. Naomba tusioongelee kuongeza serikali yoyote ile.
Mdau wa USA
Haya ni mawazo ya kibinafsi yaliyotengenezwa tokea enzi za utwana na ubwana. Mtu anapotoa mawazo yake kwa kuwa ni Chogo basi anatisha wengine lakini wengine walioundwa na vimelea vya kulalama na jazba wanahaki ya kuchimba mkwara.
ReplyDeleteHakuna umuhimu wa kuwa na serikali tatu kwa kweli. Mi nadhani uwepo wa serikali moja unatosha kabisa lakini swali ni kwamba wale waliopata wake wa kupora miaka ya sitini na kujenga mahekalu mbinguni na kuacha kundi la wengine maskini wa selwa na boflo na mlo mmoja kwa siku watapata nafasi wapi kuonyesha tambo zao za kutumia magari ya serikali kwa ajili ya birthday za watoto wao?
Hilo ndilo kubwa ambalo linawashinda wengi kuliongelea kwa undani zaidi badala yake visingizio vya kutaka kuwa proffessional ombaomba ndivyo vinavyojenga hoja zaidi ya kuwa na serikali tatu. Mimi naamini kabisa kama kutakuwa na kura ya maoni inayosema uwepo wa A)serikali tatu B)serikali moja C)serikali mbili halafu Watanganyika wakachagua kuwe na serikali moja na kuwashinda Wapemba basi watasema wameonewa. Tusijenge misingi mibovu ya kuwaachia watoto wetu katika karne hii kwani dunia imekuwa ndogo sana.
Huu muungano umefikia tamati tu kama watoa hoja wana uwezo wa kuzipigania hoja zao kwa dhati. Tuache kuwasemea watu kisa tu wewe ni mwanasiasa.
lakini tanzania hawana kosa kwa kuwa wamerithi tabia za watawala wao wakati wa ukoloni, waingereza. muungano wa kiingereza ni wa nchi nne lakini una srekali tatu tuu, na kila nchi ina first minister isipokuwa england
ReplyDeleteHatuwezi kusema tuwe serikali moja kwa sababu sisi ni mataifa tofauti,zanzbar ni nchi hatuwezi kufuta serikali yetu,ikiwa haiwezi kani kuwa na serikali tatu basi bora tuvunje,kama munaona ni gharama,sisi wazanzibari tuko tayari kutoa 50% kuchangia katika serikali ya muungano,lakini tuwe na na serikali ambayo itakayoleta usawa baina ya pande zote mbili. sio muungano huu mmoja kumanyanyasa mwengine hatukubali wazanzbari.
ReplyDeleteMawazo yetu watanganyika kuitawala zanzibar,na ndio maana nyini mumeshikiliza one govt lakini kwa upande wenu hilo,sisi hatuko tayari.
Sikiliza radio mzalendo.net utasikia mjadala wakatiba,nafiriki wengi hamujui hisotria ya tanganyika wala zanzibar ndo mana munakumbatia muungano.