Wadau wa Michuzi! Naomba mnisaidie kutafakari yaliyotokea leo bungeni,
pia dhamira ya watu wachache wanaotaka kueleza umma kuhusu "KUHUSU
KUFANYA SIASA KATIKA VYUO VIKUU HAPA NCHINI". Naomba wadau wangu
muhimu tuangalie hoja hizi ninazoziweka hapa, baadaye tuangalie nani
anafanya siasa ndani ya vyuo vikuu:

1. Mheshimiwa Shukuru Kawambwa na Vuai Nahodha walikuja mwaka jana
mwezi wa 12 katika chuo kikuu cha Dodoma na kuahidi mbele ya jumuiya
ya Wana-UDOM kuwa madai yao ya mafunzo kwa vitendo yatatekelezwa na
serikali imesikitishwa kwa nafasi hizo kutotolewa mapema-Matokeo yake
Hakuna mwanafunzi hata mmoja( 1) aliyeenda kufanya field ( Je kawambwa
alipata ujasiri ule wapi kuwadanganya wasomi wa UDOM?-   WALIPOONYESHA
DHAMIRA YA MGOMO, VIONGOZI WENGI TENA WA CHAMA CHA KIJANI WALIJITOKEZA
HARAKA NA KUSEMA KUWA KUNA WANASIASA WANAHAMASISHA MIGOMO
VYUONI!!!!!!!!!!!!!!!

2. Mheshimiwa Ester Bulaya(CCM) amewahi kukariwa akisema kuwa UVCCM
hapa nchini imejipanga vizuri hadi kuwa na viongozi wao katika
serikali za katika vyuo vikuu hapa nchini. Alimtaja Mwenyekiti wa
Serikali ya wanafunzi Udom kama kiongozi wa UVCCM katika serikali za
wanafunzi.

3. Mwezi wa tano mwaka huu. Mheshimiwa Nape Nnauye amewahi kutembelea
chuo kikuu cha Dodoma tena akiwa na vazi la Sera na Uenezi wa itakadi
ya Chama cha Mapinduzi-Je alikuwa anafanya kazi gani?

4. Uongozi wa chuo cha Dodoma umepiga marufuku shughuli zote za
kisiasa ndani ye eneo la chuo-Lakini mbona tumeshuhudia mabasi makubwa
yakija na kuchukua baadhi ya wanafunzi tena wakiwa wamevalia sare ya
chama cha kijani?.

Wadau wangu wa michuzi! Nani anafanya siasa vyuoni, naona kuna njama
zinataka kuhalalishwa kupitia vazi la siasa vyuoni. Tuweni makini sana
tena sana. Karibuni kwa mjadala huu.

                  Mungu bariki Tanzania
                  Mungu bariki Wananchi werevu uchungu na nchi yao,
                  Mungu bariki Japo mafisadi waone aibu juu ya mipango yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2011

    Kaka hujui wewe kuwa chama cha kijani/ccm bado kinataka kuendelea na kujiona kuwa ndio chama pekee chenye haki ya kufanya kitakacho? Wakifanya wao CCM ni halali ila chama kingine kikifanya ni kosa!siasa ya maji taka ccm inaiweza sana na watanzania tumekuwa viziwi, wasahaulifu na tusiopenda kuchambua kutofautisha kati ya mchele na mchanga! Mie bado nashangaa wanaoendelea kuisaidia hiyo ccm maana ndio chanzo cha matatizo yote, matatizo hayakuletwa na upinzani, ila upinzani unajaribu kuyatatua hayo matatizo yaliyoletwa na ccm.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2011

    Huo ni Mjadala ni swali ambalo unalijibu mwenyewe? Halafu unaandika yaliyotokea leo Bungeni, kisha unatoa historia ya viongozi wa CCM kuja chuoni kwenu, whatsup meen!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2011

    Ha sasa wewe mtoa mada unajichanganya mwenyewe. Waziri amepeleka hoja kupiga marufuku siasa vyuoni. Hajasema siasa za chama fulani. Kama siasa zilishafanyika huko nyuma basi. Hivyo usiwe biased katika maelezo yako. Tukianza kutaja viongozi wa vyama ambao walishaenda vyuoni si tutakesha. Ndiyo maana serikali inapendekeza kama mwanafunzi anataka siasa atoke nje ya chuo akafanye siasa halafu baadaye arudi. Hujakatazwa kufanya siasa kinachokatazwa ni siasa chuoni.
    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2011

    Nilazima tukumbuke kuwa CCM, ni chama tawala, na katika uongozi wa Rais J.K UDOM ikatokea, nilazima watu wapongeze hili, si kulaumu laumu bila kufikiri kwa kina. Mawazo mengi ya wasio ona ccm imefanya nini yanatoka na ubongo kumezwa na mitazamo ya vyombo vya habari, hawajishughulishi kufikiri, tena inashangaza sana kuona wasomi wazima mitazamo yao inayumbishwa na baadhi ya siasa chafu zinazo tolewa kwenye baadhi ya vyombo vya habari. Mimi nimetembea nchi nyingi dunia bado wanamatatizo kibao, watu wanao ishi nje wanajua hao ila wanao bisha wanataka tu kujionesha nawao mambo safi kumbe hakuna kitu. Kila chama kinataka kushika madara, hivyo sishangazi na njii kama hii unae tumia mdau,kutafuta kuungwa mkono kwa jambo kama ili maana yaelekea tayari wamesha kupa fungu lako ueneze uzushi. Haya ungeyamalizia huko huko chuoni kwenu na si kwa wananchi. hii inamaana umesha shika mawe unataka kurusha baada ya kuuliza na kuto onekana ulikuwa unasababu ya kurusha. Lazima watanzania tujifunze toka kwenye nchi zilizo kumbwa na matatizo. Jua ukisha maliza vita kuigenga tena nchi nivigumu sana sikitu cha miaka mia, nazaidi. Kwahiyo mdau kuwa makini sana na mambo unayo shirikisha watu, sisi tusio wanafunzi kuna mambo tunapambana nayo katika uwanja wetu na nyinyi muyamalize huko huko chuoni. UDOM ni mtoto wa CCM naweza nikasema hivyo, kwanini mzazi asimtembelee mwanae? au Mdau unataka mambo yaharibike alafu watu waanze kukulaumu chama cha watu kuwa ndicho kimeharibu mambo!. NAKUSHAURI TENA MALIZA MAMBO YAKO HUKO HUKO, USISAMBAZE MABANGO YASIYO CHUJWA KIAKILI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2011

    Acha siasa ndugu soma kwanza, pata kazi nzuri uone kama siasa itakushughulisha. Kila nchi ina matatizo yake, rushwa kila mahali usifikiri UK au USA hakuna rushwa, vijana wao wanajishughulisha na mambo yanayowahusu. Uonevu kila mahali. Hivi sasa UK kosa dogo tu kama si raia kwenu hata kama la trafiki, mshike mshike sehemu za maviwanda hususan vile vyenye wageni wengi. Hata maprofesa sasa wameingia mzigoni wanachukua mahudhurio ukiwa hupo siku chache tu uhamiaji wamepewa taarifa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2011

    inawezekana labda mimi sielewi mjadala na wachangiaji wanachochangia. Mbona watu mnataka kuita kijiko beleshi wakati kinaonekana ni kijiko. Swala la kusema kuwa UDOM imetokea kwenye awamu ya JK na CCM haihalalishi viongozi wa CCM kukifanya hicho chuo ni jukwaa lao la kisiasa hata kama ilikuwa historia tutakaponyamaza si wataendelea? Na ikiwa UK na USA kuna uonevu basi sehemu nyingine zote wakubali kuonewa? kama upo yuukei na unaona ni sawa kuonewa thats your stupidity! KWA KIFUPI KINACHOFANYIKA SIYO na wanasababisha vitu then wanakimbilia kusema upinzani umechochea. Mfano mzuri vijana wa Nyamongo chunguza chanzo chake na uzembe ulikuwa wa nani then lawama zilielekezwa kwa nani?UPINZANI, acheni upuuzi wa kulea vitu na kutokemea vitu coz madhara yake ni makubwa mno baadaye.HATA KAMA USHUHUDA ANAOTOA MTOA MADA ULISHAPITA USIPOKEMEWA SI WATAENDELEA? NA WEWE UNAYESEMA MTOA MADA AACHE SIASA ASOME KWANZA NYIE NDO MNAOTAKA WANASIASA MAMBUMBUMBU,UNAFIKIRI HAO KINA MNYIKA AU ZITO SIASA WAMEZIANZA WAPI KAMA SIO VYUONI.jifunzeni kusema noo kwa vitu ambavyo siyo unafikiri kuwa UK au US hauhusiki familia yako iko wapi hivi sasa unapotetea ujinga ni madhara gani itapata upuuzi huu ukiendelea.TAFAKARI CHUKUA HATUA!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2011

    Wadau wengi wachangia maada wanajaribu kupotosha ukweli hama kwa makusudi au kwa kutojua. Mtu anasema UK usipokuwa darasani Prof anapeleka taarifa uhamiaji ni kweli kwa vile wengi mmeenda si kusoma bali kufanya kazi nawao wanaangalia raia zao kwanza kabla ya kuangalia wageni. Kuhusu rushwa ni kweli kila sehemu rushwa ipo lakini zinazidiana kwa TZ zimezidi sana huko ulipo wewe unaweza ukampa rushwa trafic?

    Nyie mlio nje ndio watu mliokuwa mnategemewa katika kutoa michango mizuri ambayo inaweza kuleta changamoto kwenye nchi yetu badala yake hamna tofauti yoyote na sisi ambao hatujawahi kuona maisha ya nchi nyingine zaidi ya TZ.

    Na bora UK walivyoweka sheria kali ili mrudi huku muone adha tunazozipata za umeme, maji n.k

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2011

    Tuacheni majungu CCM is a killer of this country. Wenye mitazamo finyu wanaona ccm imeleta mendeleo lakini wenye akili wanajua maendeleo yaliyoletwa na ccm ni "insiginifacant" ukilinganisha maendeleo hayo na rasilimali zilizopo au pesa walizopeleka kwenye mifuko yao. Ndio maana tunataka mabadiliko. Tuone kama wengine nao wakipewa madaraka watatumia vipi vipaji vyao kutuletea maendeleo. Hatuwezi kusema eti kwa vile vyama vyote vinataka madaraka basi tusiamini kile vyama vingene wanachotaka kuifanyia nchi hii na tutumie kigezo hicho kuendelea kuwasapoti ccm hata kama wanaimaliza nchi. Nini maana sasa ya kuwa na mfumo wa vyma vingi nchini? Tutawezaje kufaidika na mfumo wa vyama vingi kama hatutaki wengine waingie madarakani? Kwa nini basi mfumo wa vyama vingi usifutwe kama hauna manufaa kwa taifa? Kuwanyima vyama vingine kuongoza nchi kwa kutumia hila na mabavu ya dola ni kuwanyima watanzania fursa ya kupata experience ya utwala wa aina nyingine ambao unaweza kuwa chanzo cha mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Maendeleo yanakuja kwa kubadilisha mbinu mabalimbali za kiutawala, kitu ambacho ccm imeshindwa kukifanya. Ndio maana wabunge wake wamekuwa wakipiga makofi na kuitikia ndioooooooo hata kama hoja iliyoletwa na serikali haina maslahi kwa taifa. Pia Mtoa maoni hapo juu aemesema UDOM ni mtoto wa CCM. Hili nalikataa katakata kwa sababu UDOM imejengwa kwa kodi za wananchi wote wakiwemo wasomi na watu toka vyama vingine. Naomba uone aibu kwa kutoa kauli ya kijinga kama hii. Pia vyombo vya habari vitaendelea kuaminiwa kwani vimekuwa mstari wa mbele katika kufichua maovu ya ccm. Ndio maana ccm mnavichukia.

    Lakini sishangai ndio maana tunaitwa wadanganyika. Kwanini ccm wao wafanye siasa vyuoni lakini wakataze vyama vingine kufanya hivyo? Hizi si zama za kudanganyana tena.

    NB: Tafadhali sana Michuzi naomba usibane hii comment kwani bila kuelezana ukweli hatutafika.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2011

    Watu wengine wajinga kweli,then wanakaa kutetea kuwa UDOM ni mtoto wa CCM.Hii tabia inabidi ikomeshwe

    ReplyDelete
  10. Ndugu acha kutoa hoja zisizo na mashiko. Nape kuja UDOM au Nahodha na Kawambwa kuja ni wajibu wao kwa sababu mbili. kwanza ni viongozi wa serikali na pili ni viongozi wa chama kilichoshika dola. Watu wanachopinga ni tabia yenu (Chadema) ya kwenda vyuoni na kuwashawishi wanafunzi kuwa kama hamjapata mlo wa saa sita basi gomeni ..kama hamjafunguliwa milango ya uani basi gomeni....CCM kamwe haiendi kuhamasisha migomo ila ninyi ndio mnaokwenda kuhamasihsa migomo na tunawashauri muache kwani na sisi tukuhamasisha watu wetu hapatakalika

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2011

    mbona tunakuza mjadala bila sababu za msingi. alieandika makala katuchanganya sana! kwanza kasema yaliyotokea bungeni kisha anaandika kuhusu mambo ya miezi kadhaa nyuma!

    mbona umetaja viongozi wa cc tu! ina maana viongozi wa chadema akina lema, mdee, mnyika wanapokuja udom huwaoni!? wiki 2 zilizopita slaa alikua duce! uko dunia gani? au unaandika kiupendeleo? toa utoto wako hapa. kasome kwanza siasa baadaye.

    wanafunzi someni kwanza. siasa baada ya masomo!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2011

    hii ni Takrima jamani. Tutafika kweli?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 21, 2011

    Wachangiaji mnao support mada, lazima muwe wazalendo na wenyeufahamu zaidi, lasivyo tutakuwa na wasisi na elimu zenu mlizo nazo,Mambo yachuo yatamalizwa na chuo, kila chuo kina SERA ZAKE, isitoshe kunavyombo vinavyo simmia utendaji wa Vio vikuu nchini, malalamiko haya pelekeni huko. Mtoa mada amesema kunamabasi huwa yanakuja na kuchukuwa wanachuo na kuwapeleka..., na kuna mchangiaji amesema mwanafunzi akatazwi kuwa mwanasiasa ila asifanye siasa chuoni,atuoni kuwa ccm hapo inafanya jambo jema la kuwaondoa wanachama wake maeneo ya chuo na kwenda kufanyia siasa zake huko nje? Juzijuzi tumeshuhudia SLA akikusanya wanavyuo na kuongea nao na hii si mara moja, SUA alifanyia siasa chuoni kwa kufungua tawi la CHADEMA chuoni hapo, hii si siasa machuoni? Vikao vidogo vidogo vya CHADEMA vinavyo fanyika mavyumbani huko vyuoni mbona amviongelei!!! Unavyo zungumzia Nyangombo ( Huko kwenye Madini) chunguza vizuri kija mgogoro umetoka na nini acha kufatilia sana na kukubaliana habari za magazetini, CHADEMA ndio walio chochchea ule mgogoro. HAYA KILA MOJA ANITOLEE MFANO, NINCHI GANI DUNIANI, HASA AFRICA ILIYO ONESHA MAFANIKIO HADI SASA BAADA YA MZOZO? tusijidanganye, tutafute njia zakibusara kutatua matatizo yetu. HILI LENU LA CHUO NIDOGO SANA PLZ FATA USHAURI WANGU.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 21, 2011

    Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Je huyo mdau anayesema kuwa CCM is a killer of this Country anaweza kututajia chama kimoja tu ambacho kimeleta uhai nchi hii kinachotarajiwa kuleta uhai nchi hii...ili tu tuanzie hapo katika kujibu hoja hii.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 21, 2011

    Mnafiki mkubwa we wa chadema. You are not talking on our behalf m*******r. Sababu ya uongozi wa chuo kupiga marufuku shughuli za siasa zinatokana na godbless lema (aka fungamlangotupigane)kuja chuoni kuwachochea wanafunzi wa kichaga wakafanye fujo bungeni (Pius Msekwa Hall). Period. Koma kujifanya eti unaongea kwa niaba yetu..

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 21, 2011

    Nadhani mdau ametumwa na asio wajua vizuri, watampotezea DIRA, vijana wametekwa ili wafanye siasa chafu, Mtoa mada elewa kuna mikono ya watu wenye pesa, wanje wanao taka kuiteka nchi yetu kwa kupandikiza chuki za kijinga kama hizi. Soma historia ya nchii vizuri ata kuwa mtumwa wafikra. Tanzania tunaendelea vyema, wapo wanao tamanani maendeleo yetu ndio maana wanataka kutupandikizia chuki. Mimi si mwanachama wa chama chochote ita sikubaliani na ujinga wako huo. Mkutaka mbambo hayo tokeni nje ya nchi mkafanye hayo kisha mrudi kama mkifanikiwa kuwa hai.
    Hao unano fikiria ndio wema kumbe siyo, tunawaona kila kukicha wanafanya bihashara ya kuutangaza utamaduni wa Magharibi, kuaribu vijana kwa kukesha kwenye majumba yao ya Starehe, kwanjia hiyo unajenga wasomi wa namna gani. ZINDUKA KIJA. ACHANA NA WAFANYA BIASHARA SOMA WEWE.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 21, 2011

    Wewe Anony unayepinga kuwa CCM sio killer wa nchi hii ina maana wewe ni blind kiasi gani huoni kuwa mambo kama haya ndio yanaiua nchi? EPA, Kagoda, Rada, Mishahara hewa kwa wafanyakazi, Rushwa zilizokithiri, Mikataba mibovu ya kibiashara inayosainiwa mafichoni ili wadanganyika wasijue kinachoendelea na sasa hivi rushwa kwa ajili ya kushwishi bajeti ipite. Haya yote yametokea chini ya utawala wa ccm na hakuna hatua za ziada zinazochukuliwa kukomesha tabia hiyo. Kinachofanyika ni viini macho tu ili wadanganyika waendelee kuwaamini na kuwapa madaraka. Je hayo maovu niliyotaja hapo juu ukiondoa hili la juzi milioni 50 za kushawishi bajeti ipite, hayakufichuliwa na wapinzani? Je wakati wapinzani wanfichua haya wabunge wa ccm hawakuwazomea? Je ni uongo kuwa wabunge wa ccm wanapitisha hoja kwa kusema ndiyoooooo hata kama haina maslahi kwa taifa? Penye ukweli acheni tuongee.

    Jaribu kuwa mtu mwenye upeo mkubwa wa kuelewa. Hatuwapingi kwa sababu ya rangi zenu za njano na kijani ila tunawapinga kwa sababu hamna nia ya dhati ya kuliletea taifa hili maendeleo badala yake mnajitajirisha wenyewe. Kwa mtaji huo nyie ndio mnaotaka kutokee vita katika nchi hii kwani wananchi watakapoamka na kukuta hali ni ngumu kupita kiasi itabidi wafanye lile wanaloliona linawafaa. Jaribuni kuangalia mbali zaidi kuliko kukaa kulumbana na chadema. After all sina chama chochote ila yule anayeongea facts niataendelea kumuunga mkono na kumpinga yule anayetumia siasa za hila. Ogopa watu waliokata tamaa na maisha.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 21, 2011

    SASA HIVI MNADIRIKI HATA KUSEMA ETI UDOM NI MTOTO WA CCM. HAMUONI AIBU. NDIO HVI HIVI MKAFANYA VIWANJA VYA MIKOA NA KUENDELE KUWADANGANYA WATANZANIA ETI NI VYA CCM WAKATI VILIJENGWA KWA PESA ZA WATANZANIA WOTE. ENDELEENI TU KUWADANGANYA WATANZANIA ILA SIKU WAKISHTUKA MTAJUA KACHUMBARI NI MBOGA AMA DAWA. HILA ZENU ZA KUWANYONYA WENGINE NDIZO ZINAZOHATARISHA USALAMA WA NCHI KWANI ALIYEIBIWA SIKU AKIGUNDUA ANAIBIWA ATATAFUTA NI NANI ALIYEMUIBIA. MNGEKUWA MNAJALI MASLAHI YA TAIFA TUSINGEWASEMA VIBAYA. PENYE UKWELI UONGO HUJITENGA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 21, 2011

    mtoa maada alilenga jambo jema sana sema watu mmemcchukulia pesono sana jamaa yuko safi kwani alilenga kwenye ukweli na siku zote msema kweli hupingwa angalia siasa za fitina na za kuchafua ana humo humo ndani ya wava kijani halafu nyie woooote mlio changia mada ya mdau hamja jaribu kufikili kwanini wao wenye we wenzenu ambao ni viongozi wasema sema kweli kuwa sasa wana amua kujivua gamba what doe's this mean to u pipo hebu fungukeni acheni unafiki wa kuwa na mlengo usiona ma maana kwa taifa halafu mienashindwa kushangaa kwanini kama raisi hachukui hatua kwa viongozi wa serekali yake wanao mfanya aonekane hana maana na haelewi nini cha kufanya watu wana maksha kibao lkn tunaambiwa bado wako madarakani hebutujifunze kwa wenzetu mtu kama kiongozi akiwa tu na kshfa hata kabla haijathibitika kwanza lazima aweke uongozi pembeni lkn sie tumekalia kubebana tu hata mahali inapo bidi mtu kuwajibishwa wanaweka ushkaji hivi tuta fika kweli mie kueni wakweli jamani hata kama nyie mpo mahali pazuri sie wengine tuna umia mdau kutoka uswazi

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 21, 2011

    CHADEMA mkatatue kwanza tatizo la rushwa walizochukua madiwani wenu Arusha then mje tuongee kuhusu rushwa za kitaifa. Madogo tu yanawashinda, je mkipata dola!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 21, 2011

    Mi naona tujadialiane kama watu wazima, wajameni hivi tunavyosema UDOM ni mtoto wa ccm walitoa hela zao mfukoni au ni hizi hizi hela zetu za kodi? Ebo kama J.K alijenga kwa hela zake basi chuo ni chake but if is our TAX sahauni kikiita ni mtoto wa CCM. na je huyo mdau wa UK kweli yuko serious huku nchi ya Malkia ukilinganisha hela wana zopata na maendeleo yao is 95% but Tz oooh Heaven is 40% means wanaokula rushwa ni wengi sana Tz eti madini, tour, hata kahawa ni rasilimali za Tz but leo zimeandikwa zinatoka south Africa na Kenya eti bado mtu mzima unasema rushwa kila mahali we huoni hata barabara za wenzako utazinganisha na za Tz? Tangu nifike UK huu ni mwaka wa 6 sijaona tukipata shida ya umeme, gas au maji na jiulize ziwa lao linatoa umeme liko wapi? We shut up kama D.Cameron kakuambia hakikisha unaenda xkull wahi maana soon atakunyanganya visa na unapewa second flight. Wa Tz mi niko na nyie kuwapinga mafisadi iwe itatawala CHADEMA au hata tukikaa bila chama is ok ila amani ni jambo la msingi. Pia ushirikiano na pia tusiwe wanafiki tukikubaliana jambo Yes iwe yes, no iwe no. Mdau hawa wa kijani wasiwafanye huko vyuoni mkalemaa na kuona wansema ukweli, kama waliwadanganya kwa madogo wakati wao wanaendesha magari ya mabilion na bila uoga wanataka na posho wakati watoto yatima, wajane, wagonjwa wa ukimwi hawajui baada ya lunch watapata dinner? Wenzetu UK wanasaidiana sana hawaendi kanisani wengi kama sisi Africa but wakivaa nguo mara moja au mbili wanazitoa ziuzwe ziwasaidie wenye matatizo na hata serikali yao inawasaidia. Sisi viongozi wooooooote ni wacha Mungu hakuna hata mmoja asiye na dini ila hawamuogopi Mungu. Ole wenu mafisadi mnaenjoy hapa ila cha moto mtakiona siku mkifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...