Hayati Dennis Joseph Masanja |
Familia inashukuru kwa kupewa faraja kubwa wakati wa kipindi kigumu cha msiba wa mtoto wao mpenzi Dennis na inawaombea wote kwa Mwenyezi Mungu awajalie baraka tele.
Shukrani za pekee ziwafikie Paroko, Jumuiya na Wanakwaya wa Kanisa Katoliki la Mt. Gaspari wa Mbezi Beach, Dar es Salaam; Father Veri Mturushwe Urio wa Kanisa RC Mtakatifu Anna, Kinondoni Dar es Salaam, wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (waliopo ndani na nje ya nchi), Kampuni ya Simu Vodacom, Standard Chartered Bank na Benki kuu ya Tanzania; majirani wote ikiwa ni pamoja na Familia ya Msaki, Meja Mstaafu Fatuma Myalla, Ezra Mzirai, Peter Kajiru, Hussein Katanga, Salim Madati Kikundi Maalum cha marafiki wa Shabani-Kessi & Devota, na Walpha Tours. Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja, familia inatoa shukrani za pamoja kwa wote walioshiriki kwa namna moja au ingine katika kipindi chote cha maombolezi.
Familia inamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha aliyompatia mtoto Denis hadi siku iliyompendeza kumuita kwake. Denis atakumbukwa milele katika mioyo na mawazo na kwa imani kwamba siku moja Mungu atatukutanisha naye.
Denis, tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi.
Raha ya milele umpe eeh Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani - Amina.
Familia inawakaribisha wote katika Misa ya Shukrani itakayofanyika nyumbani Mbezi Beach, Jumamosi tarehe 23 Julai 2011 kuanzia saa 1.30 asubuhi.
2 Corinthians1:3-4 What a wonderful God we have-He is the Father of our Lord Jesus Christ, the source of every mercy, and the one who so wonderfully comforts and strengthens us in our hardships and trials. And why does He doe this? So that when others are troubled, needing our sympathy and encouragement, we can pass on to them this same help and comfort God has given us.
ReplyDeleteR.I.P. our loved one.
RIP Dennis
ReplyDeleteI have heard that this was a brutal murder case that was very unfair to this cute young boy...RIP Denis.
ReplyDeleteRIP Dennis, always u will be remembered.
ReplyDeleteI miss you dear boy...Its so unbelievable that you are gone,june has been a sad month for me since my father joined you in heaven on June 29th
ReplyDelete