Waziri wa Habari,Utamaduni na michezo Dr.Emmanuel Nchimbi na Mwenyeji wake Waziri wa Utamaduni wa Afrika ya Kusini Paul Mashatile wakisaini mkataba wa kuanzishwa rasmi ushirikiano katika Nyanja ya utamaduni kati ya Afrika ya kusini na Tanzania jana jijini Pretoria huku Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Afrika ya kusini Jacob Zuma wakishuhudia.
 Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya mshujaa waliopigania uhuru wa Afrika ya Kusini nje kidogo ya jiji la Pretoria jana. Wapili kushoto ni Mama Salma Kikwete na watatu kulia ni mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini.Rais Kikwete yupo nchini Afrika ya Kusini kwa Ziara rasmi ya Kitaifa ya Siku mbili.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Zuma kwa heshima yake wakati wa kilele cha Ziara Rasmi ya siku mbili nchini humo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2011

    tutaendela kutoa maoni yetu hata kama hayawafikii wahusika au hayafanyiwi kazi

    wahusika wa ngazi za juu wa taifa letu tungependelea bodigadi au huyo mlinzi wa mheshimiwa rais asiwe amevaa hayo magwanda kwani yamepitwa na wakati kila sehemu muhimu ikiwa mikutano au sherehe mbali mbali ambazo mheshimiwa rais wetu anahitajika kufika utamuona huyo bodigadi na magwanda yake kwa kweli haipendezi hapo ukiangalia huyo rais wa afrika ya kusini anao mabodigadi vilevile lakini hawakuvaa magwanda

    bodigadi anaweza kuvaa suti kama kawaida na akaendelea kuwa bodigadi na muonekano nadhifu na ni bora zaidi kiusalama

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2011

    Sasa wabongo ninini kinawasumbua tukiwa tofauti mnalalamika tukifuata mkumbo mnalalamika daa Mwacheni JK aonyeshe anaye mjeshi kwenye msafara wake….

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...