Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, 
Mh. Ummy Ally 
NA MAGRETH KINABO - DODOMA.

WANAUME wanaofanyiwa vitendo vya kikatili wameshauriwa wasiogope kwenda kuripoti katika vituo vya polisi ambapo vina madawati ya watu waliofanyiwa ukatili .

Wito huo, ulitolewa leo Bugeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Ally Mwalimu wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Faida Mohamed Bakar (CCM) Chakechake lilioulizwa kuwa wanawake wanaofanyiwa vitengo vya ukatili wanaficha.

Akijibu swali hiyo Naibu Waziri huyo alisema alisema wanawake wanaofanyiwa vitendo hivyo wako wengi na hawafichi ila wanaume ndio wanaoficha.

Hata hivyo alimtaka mbunge huyo kuwasiliana naye baadae iliampe twakimu hizo kkwa kuwa suala hilo linajumuisha wadau mbalimbali.

Naibu Waziri huyo akijibu swali la Msingi Viti Maalum( CCM, Agnes Hokororo lililouliza kuwa je ni kwa kiwango gani serikali imetekeleza Mpango wa Kitaifa wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto(2001- 2015, pia ni wangapi waliotambuliwa na wangapi sheria imechukua mkondo wake.

Naibu Waziri huyo alisema utekelezaji wa mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali zikiwemo asasi zisizoza kiserikali ,Mashirika ya dini na taasisi za serikali.

Alisema kwa mujibu wa wa Tanzania Demographic and Suvery(TDHS) za 2010, twakimu zinaonyeshankuwa asdilimia 39 ya wanawake wenye umri wa miaka 15. Hivyo theluthi moja aua asilimia 33 ya wanawake hao wamefanyiwa ukatili wa kijinsia kwa kipindi cha mwaka 2009.

Aliongeza kuwa ukatili dhidi ya wanawake unajumuisha makosa mbalimbali ya jinai makosa haya yanaripotiwa polisi na mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo alisema tatizo hilo halijaiisha katika jamii, hali halisi inaonyesha matukio yanazidi kuongezeka na juhudi za pamoja za serikali na wadau mbalimbali zinahitajika ili kutokomeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    Bado kuna wanawake wengi sana wanafanyiwa ukatili na hawatoi ripoti, hizo ni asilimia za kesi zilizo ripotiwa tu, fanyeni uchunguzi zaidi. Tamaduni na mila zilizopitwa na wakati pamoja na mfumo dume unamkandamiza mwanamkea na kupelekea kunyamaza unyanyaswaji au uteswaji kutoripotiwa. Inatakiwa kuhamasishwa kampeni ya wanawake kutonyamaza kwa unyanyaswaji unapofanywa kwao na watoto. Hongera Agness Hokororo kwa kuuliza swali la kututetea.

    Mwathirika

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2011

    Swali ,hivi mweshimiwa huyu anatokea mji gani jamani ,plse naombeni jibu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2011

    Mi sichafuwi hali ya hewa,kwani kusifu nakusema ukweli ni wajibu.
    Bi waziri Lips amejaaliwa,masha-Alla

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2011

    Kuna mbunge mmoja machachari ananyanyaswa sana na mkewe lakini anakufa na tai shingoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...