hivi ndivyo hali ilivyotokea baada ya basi la Hood lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Arusha,lilipogongana uso kwa uso na lori la mizigo lilolokuwa na mafuta ya kula tani 24 kutoka Morogoro kwenda Songea jana kwenye barabara iliyopo ndani ya hifandi ya Taifa ya Mikuki,mkoani Morogoro.watu watano walifariki na 41 kujeruhiwa.
Moto mkali ukiwaka mara baada ya magari hayo kugongana.
Basi la Hood lionekanavyo mara baada ya kuteketea kwa moto.
Dereva wa basi la Hood, Salehe Tembo ( 42) mkazi wa Mbezi , Jijini Dar es Salaam, akiwapelekwa chumba cha X –Ray kwa ajili ya kupigwa picha kabla ya kupatiwa matibabu baada ya kuungua sehemu mbalimbali mwilini.
Mama Asha Maneno akiwa na mwanae Milka Maneno , wakazi wa Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wodini baada ya kuumia sehemu mbalimbali za miili yao , katika ajali ya basi la Hood lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Arusha lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mafuta, eneo la mbunga ya wanyama ya Mikumi. Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2011

    serikali ibadili mifumo ya ukaguzi na training za lesseni.hakuna mchawi hizo ajali zina kinga.inauma

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2011

    Mimi nashangaa sana tz, yani hawa polisi wanafanya kazi gani hasa trafiki? kwann kila siku ajari? magari hayakaguliwi halafu kwann kusiwe na sheria ambayo inambana dereva kwamba mwendo unaotakiwa nihuu. Ajari tz inamaliza watu, mungu tusaidie. Hapa hakuna chakusema mungu kapenda watu wafe kwa ajari huu ni uzembe tena wahali yajuu. Yani tz kila sekta imeoza kazi yakuchaguana maswahiba kwenye kazi ndoinayotuharibu. Nina hasira sana lkn poa tu siku inakuja wote wazembe kila sekta tutawaondoa.
    Hakuna siasa hapa kwan tusipo simamia ukweli tz tutakwisha.

    Mungu walaze pema waliotutoka na wape nguvu majeruhi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2011

    Mimi natka kuuliza anayechomaga nyasi Mikumi ni Nani?Ni maafisa wanyama Pori au maana hata Juzi Dina Marios alilalamikia hilo swala hii Nchi sijui inaenda wapi?Ukipita tuu utakuta kila mara moto kwenye Mbuga huku watekelezaj wa Nchi wanajua kutalii nchi za wenzao...Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2011

    Hapa wala tusiwalaumu polisi. Kuna moto ulikuwa umewashwa katika hifadhi ya mikumi na barabara yote ilikuwa imetanda moshi. Hivyo madreva walikuwa hata hawaoni wanakoenda na bado wanalazimisha kwenda tu then matokeo yake wakagongana uso kwa uso. Magari hayakuwa na shida ile wenye shida ni madereva!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2011

    Hivi huyu Mkuu wa hifadhi hachukuliwi hatua yo yote?

    Kwa maoni yangu yeye ndiye aliyesababisha ajali hii kwani hakuweka alama yo yote inayoonyesha hatari mbele. Alitakiwa hata kuwazuia madereva kama aliweka watu kufanya monitoring ya moto ule.

    Haitoshi kusema tu miaka yote huwa tunafanya hivi na ajali haitokei, sheria za usalama lazima zifuatwe.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2011

    Inasikitisha sana.kama kuna wazembe waliousika wachukuliwe hatua kali na mabasi ya Abood yakaguliwe milango yake ya Tahadhari,inaelekea abiria wengi walikwama kutoka kwenye basi.je hilo basi linauwezo gani wa kuokoa watu 65 kwa ajali za namna hiyo?inaelekea milango ya ajali ni kuokoa watu 18 tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2011

    mola awape moyo wa subira ndg wa marehemu .....!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2011

    yaani hiyo ajali nimeikuta,nimepita pale saa kumi na mbili jioni,yaani magari yameteketea kabisa,yalikuwa nje ya barabara,inamaana basi la hood lilikuwa kwenye mwendo au la,ila mhh inasikitisha sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...