Evans Bukuku ameendeleza kuchana watu mbavu katika shoo yake ya stand up comedy la kila mwezi mara moja. Usiku wa kuamkia leo anaonekana katika moja ya vichekesho vyake, akiigiza utembeaji wa masharobaro wa kimarekani. Kwa picha zaidi na Michuzi Jr BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kaka

    Hivi hii shoo inakuwa kwa KISWAHILI au kiingereza?

    Kama kiingereza wengine hatukielewi hicho ili nisije nikaenda nikapoteza shing. elfu 10 yangu ya ngama bure.

    Tafadhali nijuzeni mnaofahamu

    ReplyDelete
  2. Toka watu wajue kutumia mtandao ishakuwa shida. angalia mdau hapo juu anadai hajui kiingereza wakati kuingia humu katumia lugha hio hio. Unajua ujuaji na kutaka sifa kunatupeleka wabongo pabaya.nani kasema kiingereza ni ukoma? acheni upuuzi nyie waswahili. kiingereza ni lugha rasmi ya biashara Tanzania na hakuna ubishi. Sasa nyie wajuaji wanafiki eti (unabana na pua) wengine kiingereza hatuelewi. Kama ulikimbia umande wewe na wazazi wako ni juu yako. sie wacha tujinome. ukuda na ujuaji wako huko huko kwa babaako. na wewe ankal wanafiki kama hawa uwe unapiga chini bwana alllaaaaaaah!

    ReplyDelete
  3. anony Wed Aug 03, 08:22:00 AM 2011 mwalimu wako kala hasara manake umesoma lakini hujaelimika. kwani ungesema kama kinatumika kiingereza au kiswahili ingekuwaje? ndio nyienyie kina NSHOMILE (nimesoma).

    ReplyDelete
  4. Mimi ndie nilieandika kumsema huyo jamaa wa kujidai hajui kiingereza. Na wewe hapo acha kudandia treni kwa mbele. Nshomile ndio maana na nyie mmezidi uswahili. koma na ukomae, ushindwe ulegeee kwa kujitia kukosa kila kitu. Wewe nawe ni limbukeni afadhali huyo jamaa wa mwanzo. Kama umesoma na huwezi kusoma na kuandika kiingereza unakuwa juha tu. Leo wakenya na waganda wakija kuchukua kazi zenu kwa kutema yai nyie ooooh (unabana pua) wanapendelewa. Leo hii kwenye mambo ya kiingereza hapa kwenu (unabana pua tena) ooh kingereza cha nini. Nyooooo....acheni unafiki na ujuaji nyie waswahili. huna cha kuandika shaddup!

    ReplyDelete
  5. Nadhani huyo Anony wa pili ni M beba boksi kakulupuka usingizini, halafu jana mahesabu yake hayakukaa vizuri na Rent ndo ishakwisha, LendLod yuko shingoni mwake.

    Eee baba tunakuomba umrehemu huyo kwa maana hajui asemalo.

    Amen

    ReplyDelete
  6. wewe unaesema heti wakenya na waganda wanakuja kuchukua kazi huku bongo,kwa sababu ya yai,wewe mbona limbukeni sana hivi umetembea kweli,au ?mimi nimetembea duniani, kuna nchi kama za ulaya nyingi tu ,awatemi yai mbona atuwaoni hao wakenya na waganda uneosema wanachukua kazi,acha ujinga wewe,bongo ndio unadanganyika huko, nenda kozi fupi ya kiingereza ukimaliza utapata kazi,mwanangu mimi nimemsomesha bongo mimi nikiwa nje,sasa hivi nimemchukua naishi nae ,shuleni huku walimu na watoto wenzake wanamshangaa hesabu ambazo watoto hata awajaanza chekechea ukiwapa wanafanya lakini yeye anababaika ,hila hilo yai unalosema wewe anatema balaa,ndio maana bongo mambo yenu mengi longolongo nyingiiii,weee dunia ya sasa imekuwa ndogo kama chungwa habari za ulimwengu mzima unapata kwa lugha zote, sio kiiengereza tuuu,lakini bado mnakatiwa umeme,maji shida,kwa hiyo naona wewe uoni ajabu heti mtu akitema yai ndio kasoma huyo..Mjinga wewe soma elimu ya dunia ndio ufahidike.asante.na nimemaliza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...