Rais Dkt Jakaya Kikwete akimvisha W.P Namsemba Amani Mwakatobe cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi kwenye sherehe hizo leo katika Chuo Cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam
Askari wa Jeshi la Polisi wakipita mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo mjini Dar es salam wakati wa kuadhimisha miaka 95 ya Jeshi hilo iliyokuwa inakwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru. Sherehe hizo zilikwenda sanjari na mahafali ya kufunga mafunzo ya wahitimu wa kozi ya Maofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi.
Askari wa Jeshi la Polisi wa Kike wakionyesha mavazi (uniform) rasmi wa askari za askari wa kike zilivyokuwa katika miaka ya mwanzo ya uhuru mara baada ya kupata uhuru ikiwa ni maadhimisho ya 95 ya Jeshi la Polisi inakwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru. Sherehe hizo zilikwenda sanjari na mahafali ya kufunga mafunzo ya wahitimu wa kozi ya Maofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi.
Askari wa Jeshi la Polisi (wakati ukoloni) wakionyesha uniform wakati Ukoloni mbele ya Rais Jakaya Mrisho kikwete leo mjini Dar es salam wakati wa kuadhimisha miaka 95 ya Jeshi hilo iliyokuwa inakwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru. Sherehe hizo zilikwenda sanjari na mahafali ya kufunga mafunzo ya wahitimu wa kozi ya Maofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya miaka 95 ya Jeshi la Polisi nchini inayokwenda sanjari na miaka 50 ya Uhuru. Sherehe hizo zilikwenda sanjari na mahafali ya kufunga mafunzo ya wahitimu wa kozi ya Maofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Askari wa mwanzo walikuwa hawavai viatu!

    ReplyDelete
  2. Wengine walikuwa wavaa viatu lakini hawakuvaa socks.Nakumbuka afande Chacha akimtukana askari sababu PATISI kavaa kama gaguro.Hizo patisi...English puttees or Hindi Patti...zilikuwa wazivaa kama bendeji miguuni,zilikuwa rangi ya kaki.
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  3. Twende mbele turudi nyuma nina swali. Hivi hizi uniform za askari wetu wanashonewa "special" kwa kila mtu au wanapokezana kama "enzi za mwalimu" tulivyokuwa tunapokeza viatu mimi na wadogo zangu? Uniform zimewavaa hawa askari badala ya kuzivaa.

    ReplyDelete
  4. Askari akina mama walikuwa wakivaa kiheshima kweli kweli, mbona hivi sasa visketi wamevipandisha sana?

    Na hao mabukta ndiyo wale African Rifles au siyo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...