Ankal akiwa na mkongwe wa picha za habari Mzee Jonas Marios ambaye amestaafu na anaishi Dodoma sasa
 Mbunge wa Ludewa Mh. Filikunjombe (shoto) akiwa na mpiga picha mkongwe Madanga Shaaban Madanga bungeni
 Waziri wa Fedha Mh Mustafa Mkullo akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa bungeni
 Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, akichangia hoja ya Wizara ya Fedha leo
 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe na Naibu wake Mh Zitto Kabwe wakisimama kwa heshima baada ya Spika Anne Makinda kuahirisha bunge kwa mapumziko ya mchana leo
 Maafisa wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali za kifedha wakitoka bungeni leo baada ya bajeti ya Wizara ya Fedha kupitishwa na wabunge
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw Erio akimpongeza waziri wa fedha Mh Mustafa Mkullo baada ya bajeti ya Wizara hiyo kupita mchana huu 
 Ankal na Mh Freeman Mbowe leo
 Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akoneshwa picha na mpigapicha mkuu wa Mwananchi Edwin Mjwahuzi leo
Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akiongea na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. ninawasiwasi na picha ya kwanza,huyo ni simbachawene kweli????hebu jaribu kuangalia vizuri nadhani siye!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Mbowe acha usanii.

    Hivi alivyovaa Mbowe ambaye si muislamu ni sahihi? Waislamu nisaidieni hilo vazi lina maana gani kwenye dini yenu?

    ReplyDelete
  3. Ma'ansha'Allah Ma'ansha'Allah!!!!Freeman na Zitto Makanzu yao na vibaragashia na makoti wametoka Chiiichaa!!!OOOhh Mbowe you fit into Muslim!Fabulously Look!Ahlam UK!!!

    ReplyDelete
  4. hawa jma jamaaa utafkiri wako pikniki wabunge baaana kuleni kwa raha zenu

    ReplyDelete
  5. Ankal umetudanganya hiyo picha ya kwanza huyo sio SIMBACAWENE bwana hebu tafuta jina sahihi la huyo mtu laasivyo nakushitaki kwa kudanganya jamvini maana naamini kuna kamati ya maadili ya Jamvi hili Hahahahaha
    Willy

    ReplyDelete
  6. kumbe freeman mbowe ni muislam mimi nilikuwa sijui yote ni sawa tu kila mtu anauhuru wa kuchagua dini anayotaka big up mbowe

    ReplyDelete
  7. Anon wa pili, hilo ni vazi la heshima kwani linamsitiri mtu vema huku likimpa nafasi ya kuwa free, bila kubanwa. Sio waislamu tu, hata watawa wa Kikristo..mapadri, maaskofu nk huvaa kanzu wakati wa Ibada. Mvaaji anapaswa kujiheshimu katika vazi hilo, haifai kutukana, kupigana wala kumfanyia mtu mwingine karaha ya aina yeyote. Usivae pia maeneo yasiyo ya heshima kama bar nk. Otherwise, ruksa kuvaa, sio lazima uwe muislamu.

    ReplyDelete
  8. Tena kukubaliana na wewe uku kwetu kanda ya Ziwa Wanyambo/Wahaya na Wagandaa/Wanyakole, Watoro, Wachigga, na Wanyoro vazi la kazu uvaliwa wakati wa harusi au mnapokwenda ukweni kuchumbia, mzee lazima uvae kazu vinginevyo hujulikani kama mzee. Mzee katika shughuli hizi hakuna kuvaa suti. Ni kazu na koti juu yake, ila upendenza zidi ukiweka kofia ya Garushnda.

    ReplyDelete
  9. Kanzu ni maalum kwa makuhani (wachungaji na Mashekhe) sasa inakuwaje kila mtu anapaswa kuvaa? hasa kwa waislam? Je si vazi linalovaliwa wakati wa kuendesha ibada tu? Hebu munisaidie mwenzenu!!

    ReplyDelete
  10. Kanzu ni vazi lenye asili ya kiarabu. Halina dini kwani wote huwa wanavaa.

    Ila nakubaliana na wadau hapo juu ni vazi la heshima kwa pande zote, uwe muislamu au mkristo.

    ReplyDelete
  11. But real is funny kuvaa vazi ambalo hujui maana yake, eti na vibarakashee haipendezi msomi, kiongozi kuiga unapaswa kuonekana serious kwa vitu unavyofanya ila kwa hili sijawafagilia, bungeni siku hizi ovyoooo hadi kinamam/dada wanafunga midundiko. Hivi hamjui kuwa hata nchi zingine zinawaangalia?

    ReplyDelete
  12. Asalaam aleikum Muftiis, nimesikia mna mke mmoja kuna nafasi tatu za wake zimebaki naomba nitume maombi hasa kwa Free niko tayari kuwa mke wako wa pili, manshaalah hapo ukiwashwa ubani tu ndoa kamili

    ReplyDelete
  13. Sheikh Zito bin kabwe na sheikh Freeman bin Mbowe mbarikiwe sana kwa kuondoa udini

    ReplyDelete
  14. Mmh Mrema amekivaa sana kibaraghashia watu hamsemi. Kweli hizi ni chuki binafsi.

    ReplyDelete
  15. NI vazi tu mbona maswali kibao lol ngoja namie nivae nione kama nita..................... kama........................lol

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...