Taswira hii naidaka nikiwa katika ndege ndogo ya American Airways uwanja wa ndege wa Taifa wa Ronald Reagan jijini Washington nikielekea Uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK wa New York kukwaa pipa kubwa la kunirejesha nyumbani Bongo kupitia Dubai. Tumepaa leo saa 12 asubuhi na safari hii ya saa moja hadi New York ni kianzio cha safari nzima ya masaa 19 angani hadi natua Ukonga. 

Napenda kutoa shukurani nyingi kwa Afisa ubalozi wetu wa Washington DC Bw. Suleiman Saleh aliyekuja kunipokea, Balozi Mama Maajar na wafanyakazi wote wa ubalozini kwa kunikarimu. DJ Luke Joe wa Globu dada ya Jamii ya Vijimambo kwa kampani baab'kubwa pamoja na wadau wa Baltimore, Maryland, wakiongozwa na kaka Benja kwa bonge la babekyuu Jumapili. 

Timu ya veterani ya Bongo Real ya Maryland nashukuru kwa kunikaribisha kwa furaha bila kuwasahau wenzangu wa idhaa ya Kiswahili ya Voice of America (VOA) kina Da'Khadija Riyami, Sunday Shomary na Da'Aida Issa kwa kunipokea vyema, pamoja  na wadau wengine wote, ikiwa ni pamoja na Kaka Muganda aliyeacha shughuli zake na kuja kutusalimia hotelini Omni Shoreham. Da'Bupe Mwangota asante kwa kunikumbuka japo kwa simu. Najua boxi lilikuwa taiti kiasi ulikwama kuja kutusabahi.

NASEMA AHSANTENI SANA SANA KWA 
UKARIMU WENU NA MOLA AWAZIDISHIE
-MICHUZI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tunashukru kwa kututembelea Kaka......Safari Njema!!

    ReplyDelete
  2. Tuambie kama umepanda dege kubwa la Emirates la kupakia abiria 800.Na utuonyeshe picha zake za hilo dege kubwa.Mungu atakufikisha salama

    ReplyDelete
  3. SAFARI NJEMA KAJENGE NCHI HUO NDIO UZALENDO TUWACHE SISI HADI TUJUE MWISHO

    ReplyDelete
  4. Kaka,

    Kweli we MZALENDO. Me nilidhani utazamia hukohuko, utafute MAKARATASI ili UBEBE BOKSI huko kama wengine kumbe we unarudi?!?

    Homgera sana kaka

    ReplyDelete
  5. Karibu tena Na tena, Ndaga fijo
    Ilikuwa furaha sana kuweza hata kuzungumza nawe. Dada Bupe

    ReplyDelete
  6. Ustaadhi una bahati sana ,maana hii safari mlitakiwa kuja wawili tu kuiwakilisha,lakini mungu anauwezo wake basi wote mkapata kuja tembea.
    Wahimize wengine nao wawe na bidii na maadili kama yenu katika kujenga nchi na sio kuidhulumu nchi.
    Lakini je mmejifunza lolote na mpo tayari kuleta mabadiliko huko nyumbani au ndio kama safari za viongozi wetu hazina manufaa yoyote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...