Taswira hii naidaka nikiwa katika ndege ndogo ya American Airways uwanja wa ndege wa Taifa wa Ronald Reagan jijini Washington nikielekea Uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK wa New York kukwaa pipa kubwa la kunirejesha nyumbani Bongo kupitia Dubai. Tumepaa leo saa 12 asubuhi na safari hii ya saa moja hadi New York ni kianzio cha safari nzima ya masaa 19 angani hadi natua Ukonga.
Napenda kutoa shukurani nyingi kwa Afisa ubalozi wetu wa Washington DC Bw. Suleiman Saleh aliyekuja kunipokea, Balozi Mama Maajar na wafanyakazi wote wa ubalozini kwa kunikarimu. DJ Luke Joe wa Globu dada ya Jamii ya Vijimambo kwa kampani baab'kubwa pamoja na wadau wa Baltimore, Maryland, wakiongozwa na kaka Benja kwa bonge la babekyuu Jumapili.
Timu ya veterani ya Bongo Real ya Maryland nashukuru kwa kunikaribisha kwa furaha bila kuwasahau wenzangu wa idhaa ya Kiswahili ya Voice of America (VOA) kina Da'Khadija Riyami, Sunday Shomary na Da'Aida Issa kwa kunipokea vyema, pamoja na wadau wengine wote, ikiwa ni pamoja na Kaka Muganda aliyeacha shughuli zake na kuja kutusalimia hotelini Omni Shoreham. Da'Bupe Mwangota asante kwa kunikumbuka japo kwa simu. Najua boxi lilikuwa taiti kiasi ulikwama kuja kutusabahi.
NASEMA AHSANTENI SANA SANA KWA
UKARIMU WENU NA MOLA AWAZIDISHIE
-MICHUZI



Tunashukru kwa kututembelea Kaka......Safari Njema!!
ReplyDeleteTuambie kama umepanda dege kubwa la Emirates la kupakia abiria 800.Na utuonyeshe picha zake za hilo dege kubwa.Mungu atakufikisha salama
ReplyDeleteSAFARI NJEMA KAJENGE NCHI HUO NDIO UZALENDO TUWACHE SISI HADI TUJUE MWISHO
ReplyDeleteKaka,
ReplyDeleteKweli we MZALENDO. Me nilidhani utazamia hukohuko, utafute MAKARATASI ili UBEBE BOKSI huko kama wengine kumbe we unarudi?!?
Homgera sana kaka
Karibu tena Na tena, Ndaga fijo
ReplyDeleteIlikuwa furaha sana kuweza hata kuzungumza nawe. Dada Bupe
Ustaadhi una bahati sana ,maana hii safari mlitakiwa kuja wawili tu kuiwakilisha,lakini mungu anauwezo wake basi wote mkapata kuja tembea.
ReplyDeleteWahimize wengine nao wawe na bidii na maadili kama yenu katika kujenga nchi na sio kuidhulumu nchi.
Lakini je mmejifunza lolote na mpo tayari kuleta mabadiliko huko nyumbani au ndio kama safari za viongozi wetu hazina manufaa yoyote.