Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili nyumbani kwa marehemu leo mchana kuhudhuria mazishi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Ghalib Bilal akipeana pole  na Kamishna wa Bunge na mbunge wa Mafia Mh. Abdulkadir Shah mazishini 
Rais wa Zanzibar,Dkt.  Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakiwa katika shughuli ya mazikonya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Silima. Maziko hayo yamefanyika leo Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi, kubeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja leo
 Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif na baadhi ya viongozi wakiwa katika dua ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, marehemu Mussa Hamis Silima, aliyefariki Agosti 23 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam, alikolazwa baada ya kupata ajali Agosti 22. Marehemu Silima amezikwa leo Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja leo. Picha na Mdau Muhidin Sufiani wa VPO na Prosper Minja wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...