Ankal salamaleko,

Pole na swaumu ingawa sina uhakika kama huko ughaibuni uliko inapanda. Mie nna shida ndogo tu, naomba wadau mnisaidie. Ni kwamba huku Mbezi Beach jijini Dar Tanesko hawajakata umeme siku ya tano mfululizo. Yaani toka wiki iliyopita, wikiendi hii na hadi hii leo haujakatwa  - Je, kuna tatizo?

Mdau Mbezi Beach

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. DAH ASANTE SANA KWA MSAADA WAKO KWA KWELI SISI TUNAJUA TUNAWAKATIA SASA SIUI TATIZO LIKO WAPI NAFIKIRI KUNA MTU ANAIHUJUMU OFFICE HAPA, SASA MASHKHOFU TUTAKATA LEO MPAKA MWEZI UJAO, OFF COZ HII NDIO PLAN TULIOKUA NAYO KWA MBEZI, ILA ANYWAY HUJUMA TU

    TUNASHUKURU KWA KUTUKUMBUSHA


    MDAO TANESIKO

    ReplyDelete
  2. Inasemekana kuwa vifaa vya kukatia umeme havijafanyiwa service tangu mgao uanze, kwa hiyo na vyenyewe vipo kwenye hali mbaya sana. haviwezi kutumika mara kwa mara kukata umeme. kwa hiyo tuwe na subra, hali ikiwa nzuri, mgao utaendelea kama kawaida

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Mbezi beach ungepiga simu kitengo cha Emergency hapo Tanesco Mikocheni uripoti hiyo hali, nina amini kutakua na tatizo kubwa sana maana siku 5 mfululizo umeme haujakatika!!!

    ReplyDelete
  4. Haa haa, mdau you made my day!

    ReplyDelete
  5. Acheni hizo huna kazi ya kufanya??

    ReplyDelete
  6. Thanks mtoa maada umenisawazishia siku yangu kwa kicheko!

    ReplyDelete
  7. Ahahahahah, hilo tatizo siyo dogo mdau wa Mbezi Beach, hili lina hadhi ya kufikishwa Bungeni, maana kama mtu wa kukata umeme eneo la Mbezi anaumwa, hawawezi kupata msaidizi mara moja?

    Mdau Degelavita, Bergen, Norway.

    ReplyDelete
  8. Namshukuru sana mdau na watoa comment maana mmeifanya siku yangu kuwa ya furaha natumaini kicheko cha leo kimeniongezea siku za kuishi.

    ReplyDelete
  9. Dah watu wanaongea kiswahili kibovu humu ndani. Ajabu mtu akikosea kuongea lugha ya kigeni wanamjia juu.
    Sasa "maada" inahusiana na nini na hii habari?
    **Jamani tukipe kiswahili kipaumbele ndiyo LUGHA yetu... Thanks.

    ReplyDelete
  10. Mdau Tabata SEGEREAAugust 03, 2011

    Mdau asante kwa uchunguzi wako huo, na pole maana kwa siku tano umekuwa ukifuatilia tu kutokatika kwa umeme. Natumai umeme utaendelea kuwaka mbezi mpaka mvua zitakaponyesha tena.
    La msingi naomba tuende tukafanye kazi tu. KWANI KILA KITU KINAWEZEKANA.

    Mdau Tabata SEGEREA

    ReplyDelete
  11. duh !mdau kweli u made my day!xso xso xso!

    ReplyDelete
  12. Nimesikia! Nitawafikia! Mimi ndo mzima switch ya umeme wa Mbezi, ntakata umeme sehemu hiyo kwa wiki mbili mfululizo kufidia siku zote 5 mlizokuwa na umeme.

    ReplyDelete
  13. Shukuran kwa kunifahamisha kupitia blog ya jamii, taarifa sasa ipo kwenye desk langu na nitaishughulikia as soon as posible. Mbezi beach kwanza tuna ugomvi nao kwa miaka miwili sasa, tunatakiwa tukate umeme kwa miezi kama 12 mbaka waanze kutumia vibatari, kwa tatizo kama hili lilitokea kwa upato wa umeme siku tano mfululizo linatokana na mashine mpya ya kukatia umeme inayoitwa "bunsen burner" na kishikizo chake kinachoitwa aparatus, ni kwamba engineer wetu alifanya makosa ndo maana mmepata umeme siku zote hizo. Nitalishughulikia hili swala immediately hivyo mtaanza kukosa umeme kuanzia jioni hii na mambo yatarudi kama kawa.

    Asante sana kwa kutujulisha,

    Wenu Meneja Mkuu TANESIKO.

    ReplyDelete
  14. si unyamaze tu, mtakatiwa siku 10 mfululizo kilipizia ohooo

    ReplyDelete
  15. Jamani upendeleo huu mpaka lini? Sasabu wanakaa wazito ndio wapewe umeme kwa siku zote hizo, chondechonde angalieni tusije geuka kuwa Mbwa mwitu.

    ReplyDelete
  16. Aliyepangwiwa kukata umeme wa mbezi yupo msibani kwa wiki mbili, mpaka atakaporudi.
    Utawala-Tanesco

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...