Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael Shirima akizungumza na hadhara ya abiria wa kwanza wa safari ya Precision Air kwenda Johannesburg katika kumbi ya VIP uwanja wa kimataifa Julius Nyerere. Bw. Shirima alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wateja na wadau wote wa Precision Air kwa ushirikiano mkubwa walionyesha kuweza kufanikisha safari hizo. “Hakika hii ni hatua kubwa sana lakini najua bila nyinyi tusingeweza kufika hapa, kwahiyo napenda kuwapongeza wateja wetu na wafanyakazi wote wa Precision Air kwa kazi nzuri. Nategemea mtafaidika kibiashara na kitalii kwa safari hizi,” alisema. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga nchini Tanzania (TCAA) Bw. John Njawa.
Wadau mbali mbali wenyeji wa Afrika Kusini na Tanzania wote walihudhuria hafla hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa O. Tambo.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mh. Radhia Msuya (katikati) alikuwepo kupokea ujumbe kutoka Precision Air jijini Johannesburg katika uwanja wa ndege wa kimataifa Oliver Tambo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko na Dr. William Nshama. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga nchini Tanzania (TCAA) Bw. John Njawa na Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw. Phil Mwakitawa. Balozi Msuya alifanya mahojiano na waandishi wwa habari na alisema kwamba Precision Air sasa ni kiungo muhimu katika kuendeleza uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili hasa hasa katika utalii na biashara.

Mdau Amani Nkurlu Afisa Mawasiliano wa Precision Air akiwa na mwanahabari mkongwe Jenerali Ulimwengu katika hafla fupi ya mapokezi yaliyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo, Johannesburg nchini Afrika Kusini. Msafara maalumu wa Precision Air ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko upo Jo’Burg nchini Afrika Kusini kwa uzinduzi na ziara maalumu itakayochukua takribani ya siku mbili.
Wadau wa Precision Air wakifurahia huduma za Business Class kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini ndani ya Boeing 737-300.
Hi ndivyo hali ilivyokuwa ndani ya ndege hiyo iliyofanya safari ya masaa 4 kwenda Johannesburg, ilibeba ya abiria 111, jumla ndege hiyo inauwezo wakubeba abiria 116.
Abiria wa safari namba PW 700 Kusini wakielekea kupanda ndege tayari kwa kupasua anga kwenda Johannesburg Afrika.
Ndege aina ya Boeing 737-300 ikijitayarisha kuondoka uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere jijini Dare es Salaam. Ndege hiyo iliondoka saa 2 na dakika 20 usiku.
Hongereni sana 'Precision-Tanzania'.Komaeni mpate zile boeing jamii ya 737-800.Mnaweza...niliona kampuni kama yenu ina makao yake Jijini Lome(Togo)inaitwa ASKY wana ubia na ET,hawa wana midege ya kisasa ingawa wanafanya biashara Africa magaharibi huko.Tunachotaka sasa ni kuturusha moja kwa moja kutoka Dar hadi tunakokwenda huko,tumechoka na connections za Nairobi.
ReplyDeleteNi mimi
David V
hongereni ila website yenu inaboa, nimejaribu kubook niondeke nextweek inakataa na kwenye home page yenu inaonyesha kuna promotion to J'bourg USD 57, ila jtatu na jnne kwenye search engine hamna ndege naomba kujua kama hii ndege si yakila siku na promotion ni ya siku gani, nijibu kwa debymbila@yahoo.com.
ReplyDeleteAsanteni