Meneja wa kinywaji cha Redd's,Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo jijini la Dar wakati wa hafla fupi ya ftari iliyoandaliwa kwa ajili ya warembo wa kanda tatu za jijini Dar (Ilala,Temeke na Kinondoni) pamoja na waandishi wa habari iliyofanyika kwenye hoteli ya City Garden iliyopo katikati ya jiji la Dar.
Baadhi ya Warembo wa Kanda tatu za jijini Dar es Salaam,wakiwa katika maandalizi ya kupata ftari jioni ya leo kwenye hoteli ya City Garden jijini Dar.
Baadhi ya Warembo wa Kanda tatu za jijini Dar es Salaam wakipata ftari ya pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari leo jijini Dar.
Meneja wa kinywaji cha Redd's,Victoria Kimaro (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya warembo wa Kanda tatu za jijini Dar,mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya ftari iliyofanyika jioni ya leo kwenye hoteli ya City Garden,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hakika kumbe shaytan huwafanya wabaya pale mnapokuwa hamjajisitiri(nusu uchi)angalieni sasa mlivyo pendeza mashaAllah,mnaonekana watu wa maana zaidi na binaadamu mliotimia na bila shaka sasa mnaweza kuitwa warembo! naombea kwa Mola mwezi huu ndio uwe mwezi wa kujikomboa kwenu kurudi katika hali ya ubinaadamu tena ishaAllah!

    ReplyDelete
  2. hivi city garden ni hoteli au mgahawa (restaurant? sidhani kama ni hoteli kama ilivyoandikwa hapo juu.

    ReplyDelete
  3. Mumependeza mumekuwa kama watu sasa, naamini hamtarudi tena kwenye kukaa utupu. Mungu awajaalie mendelee kujistiri. Amini

    ReplyDelete
  4. Bora hivyo mulivyo sasa hivi muko wazuri kulikoni mukiwa UCHI.....ati ndio munaitwa warembo

    sasa hivi munaweza mukapata mume akawaowa mukastirika nyinyi, acheni kuhashuliwa na vyombo vya habari na urembo, UMALIZIKAPO HUU MWEZI MTUKUFU BAKIENI HIVYO HIVYO MULIVYO SASA MUSIRUDI TENA KWENYE KUITWA WAREMBO, MAMBO YENU YATAKUWA MAZURI KIMAISHA YA HAPA DUNIANI NA AKHERA

    ReplyDelete
  5. ni kweli wamependeza but mnapenda kuwaonea sana wanawake,ni kitu gani kinaangaliwakwani kupata mume? ina maana bila hilo vazi hawapati wa kuwaoa? wewe wa kwako ulimpata akiwa na vazi hilo au? kumbukeni kwanza mitabia yenu wanaume ilivyo mibaya ndio muanze kuwaza mavazi ya wanawake: jirekebisheni: kama wamependeza wamependeza tu but msiingilie maisha yao kuhusu kupata waume au la. mnani-boa sana!

    ReplyDelete
  6. ............... Ankal nimeona hapo juu umegaiwa rizk na watu wa Pombe, ndio maana unawafagilia !........... kuna kesho ndugu yangu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...