Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalongeris ( aliyenyosha mkono juu) akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya DC Mh Said Mwambungu ( kushoto
 Ulinzi ukiwa umeimarishwa Kongwa
 Watuhumiwa wa vibali vya mifugo hiyo
 Mkuu wa Wilaya Mh Saidi Mwambungu akihutubia wananchi
 Mwanakijiji wa Kongwa , Tarafa ya Mvuha , Wilaya ya Morogoro akiuliza mashwali kwa DC Said Mwambungu
Vijana wa kabila wa kimasai wa Kijiji cha Kongwa, wakimsikiliza Mkuu wa Wikaya ya Morogoro, Said Mwambungu.

Picha na Habari na John nditi
wa Globu ya Jamii, Morogoro

Septemba 3, mwaka huu katika eneo la Kijiji cha Kongwa, Tarafa ya Mvuha, Wilaya ya Morogoro, wananchi wa Kijiji hicho walilazimika kuwakamata wafugaji wa wavamizi kutoka Mikoa ya kanda ya Kati na Ziwa.
Wananchi hao waliazimika kuwakamata wafugaji hao baada ya kukutwa wakishwanga ng'ombe 125 walioshushwa eneo la Ubena , barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, wakati mifugo hiyo ikiwa na kibali cha kutoka Ofisa Mifugo Mkoa wa Dodoma kikionesha kuwa inasafirishwa kutoka Kizota Dodoma kwenda Pugu, Jijini Dar es Salaam, lakini kwa ujanja wao waliamua kushushia eneo hilo na kuingizwa katika Kijiji hicho.
Kibali hicho walichokutwa nacho kilitolewa Agosti 31, mwaka huu kikimtaja muhusika mkuu ambaye ni miliki wa mifugo hiyo ameruhusiwa kusafirisha kwenye magari mawili  kutoka Kizota kwenda Pugu.
Hivyo hasira za wananchi ziliwaangukia  vijana wawili waliokuwa wakishwanga mifugo hiyo na kulazimika kuitwa kwa askari kutoka Kituo cha Polisi Matombo.
Baadaye akawasili kijijini hapo Mkuu wa Wilaya , Mh Said Mwambungu akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kushugulikia sakata hilo, vijana hao wakaamriwa kuondosha mifugo yao na kuelekea kibari chao kinavyowataka 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...