Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akitoa hotuba yake kwa wadau wa biashara ya anga visiwani Comoro. Hahaya ni miongoni mwa ruti mpya ambayo Boeing 737-300 iliyoletwa hivi karibuni inahudumia. Anaesikiliza ni Mkurugenzi wa Uchukuzi katika serikali ya Comoro Bw. Muhsin Salim. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Itsandra jijini Moroni Comoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Precision Air Bw. Alfonse Kioko (kushoto) akipongezana na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Utalii wa Comoro Bi. Kalathum Mahmoud katika hafla iliyoandaliwa na Precision Air hivi karibuni kwa ajili ya kuipongeza nchi hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha hadi kufikia Hahaya kuwa miongoni mwa ruti mpya ya shirika hilo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli maarufu ya Itsandra, Moroni Comoros. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Galaxy Wakala wa Precision Air Comoro Bw. Ali Nassor na Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Phil Mwakitawa.
Makamu Gavana wa nchi ya visiwa vya Comoro Madi Ahamada (kushoto) akikaribishwa na wafanyakazi wa shirika la ndege la Precision Air katika hafla iliyoandaliwa na shirika la ndege hiyo hivi karibuni jijini Moroni Comoro.
Wadau wa Precision Air wakijipendelea katika sekta ya mahakuli.
Kikundi cha ngoma za asili cha Sambolangade cha mjini Moroni Comoro kikionyesha umahiri wake wakati wa hafla hiyo iliyofana na Precision Air jijini Moroni Comoros.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...