Bi ELIZA ELENESTO KITUNDAMtajwa hapo juu anatafutwa na mume wake Bw. Jackson Kadwame baada ya kutoroka na watoto wawili Wilayani Iringa.
Kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa katika kituo cha Polisi kilicho karibu naye au kwa Bw. Jackson Kadwame namba 0752 354361 au 0772 054361.
Zawadi itatolewa kwa atakayefanikisha kupatikana kwake.
Taarifa ya kutoweka kwake imeripotiwa polisi na kupatiwa IR/ RB/ 5215/11.
Asante sana.


Anamtafutia nini mnyanyasaji mkubwa huyo, hadi mke anatoroka na watoto ujue kuna tatizo hapo, wanaume wababe ndio zao. Mimi wa kwangu karibu na mie nimtoroke na watoto wangu simwachii na nitamrusha live hapa ile wasomi wenzie wamwone!!!!
ReplyDeleteumejabarikiwa kwa kutuliwa mzigo na wewe unang'ang'ania kuurudisha.
ReplyDeleteMi wangu wakitoweka hata habari haitasikika.
WE MWENZETU IMEKUWAJE MPAKA MKE ANAKUKIMBIA. MTUNZE NA KUMPENDA MKEO
ReplyDeleteJamani mama mpka atoroke, kuna kitu sorry ,lakini mmmmh huyu mama labda ameteseka sasa amechoka. kwenye picha anaonekana hana raha, jamani acheni kuwapiga wake zenu, na kuwatukana mnatesa watoto.
ReplyDeletejamani mama wa watu anaonekana anamateso makubwa mno.kwanza mazingira yenyewe na mavazitu,anahaki ya kutoroka.nenda kabisa usiangalie nyuma.
ReplyDeleteNi muda muafaka umefika sasa kwa wanawake kupigania haki/uhuru wao. Mijanaume mingine ni minyanyasaji sana, na mingine inafikia hata kutishia uhai wako ukionyesha ujasiri wa ku-walk out of marriage! Mamaa popote ulipo kama umeondoka kwa ajili hiyo yaani potea haswaaa wala usiangalie nyuma, kwanza kuangalia tuu ulivyo inaelekea jamaa alikuwa anakupa moto mkali. Ila kama umemkimbia kwa ajili ya mengine fikiria watoto kwanza! manake wanamuhitaji baba yao.
ReplyDelete