Bi ELIZA ELENESTO KITUNDA


Mtajwa hapo juu anatafutwa na mume wake Bw. Jackson Kadwame baada ya kutoroka na watoto wawili Wilayani Iringa.

Kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa katika kituo cha Polisi kilicho karibu naye au kwa Bw. Jackson Kadwame namba 0752 354361 au 0772 054361.


Zawadi itatolewa kwa atakayefanikisha kupatikana kwake.
Taarifa ya kutoweka kwake imeripotiwa polisi na kupatiwa IR/ RB/ 5215/11.

Asante sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Anamtafutia nini mnyanyasaji mkubwa huyo, hadi mke anatoroka na watoto ujue kuna tatizo hapo, wanaume wababe ndio zao. Mimi wa kwangu karibu na mie nimtoroke na watoto wangu simwachii na nitamrusha live hapa ile wasomi wenzie wamwone!!!!

    ReplyDelete
  2. umejabarikiwa kwa kutuliwa mzigo na wewe unang'ang'ania kuurudisha.

    Mi wangu wakitoweka hata habari haitasikika.

    ReplyDelete
  3. WE MWENZETU IMEKUWAJE MPAKA MKE ANAKUKIMBIA. MTUNZE NA KUMPENDA MKEO

    ReplyDelete
  4. Jamani mama mpka atoroke, kuna kitu sorry ,lakini mmmmh huyu mama labda ameteseka sasa amechoka. kwenye picha anaonekana hana raha, jamani acheni kuwapiga wake zenu, na kuwatukana mnatesa watoto.

    ReplyDelete
  5. jamani mama wa watu anaonekana anamateso makubwa mno.kwanza mazingira yenyewe na mavazitu,anahaki ya kutoroka.nenda kabisa usiangalie nyuma.

    ReplyDelete
  6. Ni muda muafaka umefika sasa kwa wanawake kupigania haki/uhuru wao. Mijanaume mingine ni minyanyasaji sana, na mingine inafikia hata kutishia uhai wako ukionyesha ujasiri wa ku-walk out of marriage! Mamaa popote ulipo kama umeondoka kwa ajili hiyo yaani potea haswaaa wala usiangalie nyuma, kwanza kuangalia tuu ulivyo inaelekea jamaa alikuwa anakupa moto mkali. Ila kama umemkimbia kwa ajili ya mengine fikiria watoto kwanza! manake wanamuhitaji baba yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...