Ankal Salamaleko!
Hongera kwa kupata shati jipya. Mie leo nna kajiswali ka-kizushi ambako naomba wadau watukufu wa Globu ya Jamii wanisaidie kulijibu, huenda majibu yakasababisha mambo kuwa mswano, hususan uopande wa kichwa chetu cha kiuendawazimu katika soka.
Ukizingatia kwamba kila Taifa Stars, Twiga Stars, Serengeti Boys na timu zote za michezo za Taifa zinarudi kapa siku nenda rudi, Swali: Je, endapo ungekuwa kiongozi wa juu katika Michezo ungelifanya nini ili tasnia hii iendelee?
Nawasilisha
Mdau wa Soka
Mpanda
Hongera kwa kupata shati jipya. Mie leo nna kajiswali ka-kizushi ambako naomba wadau watukufu wa Globu ya Jamii wanisaidie kulijibu, huenda majibu yakasababisha mambo kuwa mswano, hususan uopande wa kichwa chetu cha kiuendawazimu katika soka.
Ukizingatia kwamba kila Taifa Stars, Twiga Stars, Serengeti Boys na timu zote za michezo za Taifa zinarudi kapa siku nenda rudi, Swali: Je, endapo ungekuwa kiongozi wa juu katika Michezo ungelifanya nini ili tasnia hii iendelee?
Nawasilisha
Mdau wa Soka
Mpanda
Ningemtimua Maximo!
ReplyDeleteDuh kweli hilo swali ni gumu tena la kizushi.kwa upande wangu.ningemrudisha maximo,kwani ndiyo amejenga timu ambayo imeonyesha ushindani kwa vigogo wa soka duniani.kukabiliana na morocco kwao si mchezo.
ReplyDeleteNingesimamisha ushiriki wa kimataifa kwa miaka mitano, then niaandae timu mbalimbali. mfano Angola
ReplyDeletekwa kuanzia ningetumia wanamichezo waliopita kufundisha michezo kuanzia ngazi ya chekea kwa kugundua au kuangalia mtoto anapendelea mchezo gani husika basi tungeanzia hapo. lingine vyuo vya ualimu mahususi kwa michezo ili tupate walimu wenye viwango ktk mchezo husika. vile vile kuanzisha shule za vipaji maalum vya michezo, mbona inawezekana...
ReplyDeletena hii sio kitu ya miaka 5 au 10 ninayozungumzia hapa ni kitu cha kuanzia miaka 15 mpaka 30 ni mipango endelevu ndio inayotakiwa kwani kiongozi au wengi wetu hatutakuwepo tena ktk mfumo au maisha kwa jumla.
pia viwanja vya michezo mashuleni na sehemu nyinginezo viwepo kwa wingi....
WaTZ wenyewe ndio hawana malengo ya michezo. Angalia watani wetu wa jadi sasa wamemiliki mbio ndefu. Kila mkalenjini ana uelewa kuwa akikimbia anatajirika. Watu Africa magharibi mtoto wa kiume akikuwa tu anapiga soka kwa bidii ili aje kuchezea ligi za Ulaya. WaTZ hawana motisha yoyote kazi yao kusenganya na choyo tu basi.
ReplyDeleteJamani kuona hamuoni basi hata kuisi... Tanzania tumesema KILIMO KWANZA sasa sisi na soka wapi kwa wapi peleka wote shamba wakalime tupate misosi kwenye soka wanapoteza muda TU kampeni yetu yenyewe ya KILIMO KWANZA inatufunga
ReplyDeleteNingejaribu kuwahamasisha Wadau wote kwa pamoja na hasa kuanzia ktk Familia kutoa mchango wa dhati kuwajenga kiakili na kuwasupport watoto au ndugu zetu hili wafanikiwe kuwa wachezaji wa ukweli..hao kina Rooney,Beckham,Ronaldo,nk ni matunda ya jamii na wazazi wao kujitoa mwanga au kuwekeza kwao na ndio mavuno yake hivi sasa..Serikali tunaisingizia na wala hakuna sababu ya kubeba huu mzigo kama kwanza sisi wenyewe hatuna mchango wowote..
ReplyDeleteUnajua wachezaji wetu hawajafundishwa somo la uraia. Ningewafundisha somo hilo wangejifunza kuwa tayali kufa ili nchi isipate aibu. Kwa hiyo inatakiwa kucheza kufa na kupona. Hilo ni Moja
ReplyDeleteJambo la pili ningewapa pesa nyingi kwa ahadi.Ningewauliza wananangu mnaniahidi ushindi? wangejibu Ndio kama kawa. Mnataka sh ngapi ili mrudi na ushindi mzuri wangesema milioni kumi kumi ningewapa. Lakini wangerudi bila ushindi ningewaweka ndani(Lupango) miaka mitano na kazi ngumu na viboko kumi wanapoingia kisha kumi wakati wa kutoka.Ukifanya hivyo mala tatu tu ushindi ungeanza kupatikana.....Kizito!!
Mbona madictator Kama hitler walileta maendeleo Fulani kwa kutumia Nguvu na mabavu. Unatumwa kucheza mpira Kama mdau alivyosema hapo juu na unataja kiasi gani cha pesa upewe, ukishindwa lupango tu. Hivyo wataoweza wanachukua jukumu. Mbona north Korea kiongozi akishindwa kuongozam wizara aliopewa ni lupango tu. Au kifo. Mnakumbuka Nigeria waliposhindwa tu miaka ya 60 wachezaji walipelekwa front line vita ya biafra.
ReplyDelete