ANKAL!! 

Many Greetings from Tanzania –Burundi Border. Mwakeye! Mwalaye!

Above photo show a beacon at Manyovu along Kigoma Tanzania border. Behind is a wonderful landscape. The populated are (houses) on the right side is in Burundi while the left is on Tanzania side.
Salaam hapa ni Kiha wanasema “Mwakeye” na “Mwalaye”-  Za asubuhi na umelalaje. We reached the village after cruising the 55Km newly inaugurated road of Kigoma –Manyovu.
 The weather at Manyovu was cool and dry. What wonderful scenery driving in the beautiful land scape from Kigoma (700m a.s.l) to Manyovu (1450m s.sl.). The new infrastructure has completed transformed the socio-economy of the area to the better. 
One starts from dagaa (sardine)-oil palm economy at the shore of Lake Tanganyika to coffee, avocado and banana mix farming economy at Manyovu. The so called ZK political dominance is really inviting. ZITTO is written on the rocks along the road.  The sticking view is the contrasting land use scene on Tanzania and Burindi side. 
While the latter is densely populated, the other is not. E bwana ee yaani katika barabara mpya ya Manyovu unakutana na baiske zilosheheni  mananasi, mawese , ndizi mbivu makatapera nk. Ni kama Lushoto au Tukuyu Hakika mambo ya uchumi hapa sio mbaya. At the Manyovu market this morning the price of banana bunch was 6,000 Sh ,  nanasi 500Sh na Udongo Pemba 5,000Sh,
Another  eye catcher along the road is the factories for Udongo Pemba. Udongo Pemba ni ule unaoliwa na wamama wajawazito.  As mineral supplements, si unajua mifuta ya kichanga inahitaji kujengwa na calcium. In the absence of eggs etc. Kiroba ni sh 5,000.  This is a booming business for young men on the road side at Mkingo Village.
 The calcium rich soils are shipped to Mwandiga where they are converted into usable pellets/ vidole ready to be sold to other cities such as Mwanza and Dar es Salaam and even DRC and Burundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Hapo ndio nyumbani, nimefurahishwa mno!

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana mdau kwa ripoti yako ya kueleimisha. Hakika tunahitaji mambo kama haya sio wengine kuuza sura tu.

    ReplyDelete
  3. Mkuu, ahsante sana kwa nia yako njema ya kutuelimisha, lakini naomba nitoe mchango wangu wa senti mbili.

    1. Ungeeleweka vizuri sana kama ungetumia lugha ya kiswahili.

    2. Kula pemba kwa wanawake wenye mimba na hata wale wasio na mimba ni dalili za mtu kuwa na kiwango cha chini cha nutrient na lishe mbovu (malnutrition), mfano Iron dificiency anemia na zink dificiency. Na hiyo tabia ya kula pemba kwa lugha ya kitaalam inaitwa "pica". Na siyo pemba tu mtu anakula non-food materials (kama vumbi na udongo) na mara nyingi hutokea kwa watoto wadogo.

    ReplyDelete
  4. Asante mdau kwa taarifa hizi za kutia moyo.
    Ingekuwa ni jambo la msingi sana kama hawa wakulima wa matunda wangewekewa kiwanda japo kidogo cha kusindika matunda. Hii ingekuwa ni motisha kubwa.
    -----------------------------------
    Jamani Mheshimiwa Kabwe anaendelea vipi kule India? maana imekuwa jiiiiiiii!!!!!!

    ReplyDelete
  5. tuwekee pia picha za hiyo barabara mpya na vielelezo vingine vya kiuchumi ili tuweze kukuelewa zaidi

    ReplyDelete
  6. Mwakeyeneza!

    ReplyDelete
  7. Anonymous hapo juu kiwanda cha kusindika matunda ni jambo zuri, ila tuwaze kwanza nishati gani itatumika kuendeshea mitambo ya kusindika hayo matunda.

    ReplyDelete
  8. Mdu hapo juu hufuatilii vyombo vya habari? Mh. Kabwe mbona ana wiki tangu arudi toka India.
    Ndio nyie mnaotegemea habari toka kwenye internet tuu wakati vyanzo vya habri vipo vingi tuu.

    ReplyDelete
  9. Anony Thu Nov 24, 07:52:00 AM 2011 wapi maneno kama tunaomba, tafadhali na kama kuna uwezekano?

    ReplyDelete
  10. Mtoa habari kuhusu kigoma, tafadhali kama ungeweza kutuwekea picha ya barabara ilivyo ili na sisi wanakigoma tuweze panuliwa mawazo kwa swala la kuwekeza ! jitahidi kama una uwezo na sisi tunaoishi mbali na upeo huo tuweze amshwa, ukweli mimi binafsi nilikuwa nimelala kama umetufungua macho. Kuna apportunities nyingi tu za sisis wana kigoma tunaoishi Ughaibuni kuja fanya mambo ya kisasa, Hongera kwa kutoa habari hiyo.

    Mdau marekani, original Mwanga Kigoma.

    ReplyDelete
  11. Vipi suala la umeme huko? mambo yanawezekana kwa sisi wadau kuja wekeza kwani mimi ni mkazi wa London kwa hivi sasa,je uwezekano wa kuweka mashine angalau za kuuzia juice na kuchomea chips.

    tufahamishe tuje turudi nyumbani tumechoka na huku weee acha tu.

    ReplyDelete
  12. Ngoja nitupe matope kidogo
    Mwakeyi mugabo, ulimo?
    Natoa pongezi kwa ujenzi wa barabara hiyo huko Manyovu.Lakini nisamehe nikiuliza barabara hiyo yule Muha kule Manyovu kijijini itamsaidia nini binafsi?Hizi barabara za lami ni nzuri sana kwa uendeshaji wa michuma ya waliojaliwa, na kwa usafirizaji wa bidhaa za matajiri, hivyo kuwawezesha kutunyang'anya zaidi hata kile kidogo tulicho nacho.Basi mimi ni Msegeju sina ng'ombe nawe una ngo'mbe zako naomba tuchanganye.Kwa wale wasiojua Kiswahili, nasema yaani, muheshimiwa Zitto na wengine wawasaidie hao jamaa vijijini wasimame kutoka kwenye vumbi, au wataendelea kuvaa milumba na kaniki milele.

    ReplyDelete
  13. jamani kasulu... umenikumbusha nyumbani.... jamani Mtabila na Muyovosi.

    cool place, udongo mwekundu na mvua full full october to may...kuna siku unakaa 2 or 3 days hujaona jua. da, hebu kuinuke zaidi kiuchumi from that new road connecting kigoma to burundi

    ReplyDelete
  14. mbona zitto ameisha rudi yupo hapa tanganyika?

    ReplyDelete
  15. Issa Michuzi hongera sana kwa kufika kwetu.Hali ndiyo hiyo uliyoiona ila hukufika kwenye maporormoko ya mto Mtunguruzi ambapo watoa umeme wa maji unaotumika katika hospitali ya Heri Mission ya Nyamasovu.Kuna mambo mengi sana pale tarafani Manyovu lakini hayawafikii watanzani kwa njia hii.jitahidi kwenda tena siku nyingine utajifunza mengi.Hongera sana na karibu tena kwetu.

    ReplyDelete
  16. yani hawa WAHA na waburundi hawana tafauti kabisa kwanza wameowana na kuzaliana saaana intermarriage ipo tu kwa sana ni basi kuna border imewatenganisha

    ReplyDelete
  17. Asanteni wadau kwa kunijuvya kuwa Zito yu nyumbani. Na Mwenyezi Mungu ashukuliwe.

    ReplyDelete
  18. Ikiwa unahitaji kuwekeza katika eneo hilo la Kigoma, wasiliana na tanzania.panorama@gmail.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...