Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa akibadilishana nyaraka za mkataba wa awali na Mkurugenzi mtendaji wa Tanzania Investment Bank baada ya kutia saini makubaliano ya awali ya manispaa ya Ilala kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la kisutu. Manispaa ya Ilala sio tu ndiyo ya kwanza kwa halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na TIB,Bali pia mradi huu utakuwa unamilikiwa kwa 100% na halmashauri tofauti na miradi ya ubia. Hii imekuja kuunga mkono jitihada za Rais wetu mpendwa Jakaya M Kikwete aliyeiongezea mtaji TIB kwa maendeleo ya nchi yetu. Ujenzi unategemewa kuanza mapema mwakani na mpango huu utaendelezwa kwenye masoko mengine kutimiza mpango wa meya Silaa wa kuwa na masoko makubwa na ya kisasa kama njia mojawapo ya kuondoa machinga mitaani,kukuza ajira na huduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Initiative nzuri na ya kuungwa mkono.Ni kuhakiki utekelezaji wa mradi kwa wakati na baada ya hapo kuhakikisha usimamiaji na ukarabati wa kitakachotokana na mradi huu vinazingatiwa.Kama kuna fikra kwamba sehemu ngumu ya kazi hii imepita basi ni makosa kwa maana kazi ngumu ipo mbele kwenye mradi huu.

    ReplyDelete
  2. Hivi ile benki ya jiji haina fedha? Kwanini hawa kukuopa kule, wame kopa TIB? Halafu nadhani kwa mfumo wa uchumi uliopo, si vyema kwa halmashauri kujiingiza moa kwa moja katika kuwekeza na kumiliki vitaga uchumi, na kujiingiza moja kwa moja katika biashara. Halamashauri zitafuta namna ya kuweza kuwezesha wafanya biashara waweze kukuza biashara zao kwa kuongeza ukwezaji ili kuongeza ajira. Tunarudi kule tulipotoka;yaani serikali na taasisi zake kumilika vitega uchumi. Sote tumeshudia matokeo yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...