MAREHEMU JOSEPHINE MASHAKA NYAGWASWA

Familia ya Askofu Mkuu Mstaafu Dr. M. P. Nyagwaswa wa Capri Point - Mwanza, inawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali wakati mama yetu mpendwa Josephine Mashaka Nyagwaswa alipolazwa katika Hospital ya Nairobi - Kenya hadi  kufanyiwa upasuaji mkubwa wa mgongo usiku wa tarehe 23/08/2011 na kutwaliwa mbinguni siku ya tarehe 24/08/2011 na kuzikwa tarehe 27/08/2011 katika makaburi ya Capripoint - Mwanza.

Shukrani zetu ziwaendee Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wote wa Nairobi Hospital na Lee Funeral Home kwa huduma zao kipindi chote ambacho Mama yetu amekuwa akilazwa hapo na hadi kutwaliwa kwake.

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote waliofika kutufariji na wale waliojaliwa kujumuika nasi siku ile ya kumpuzisha MAMA kwenye safari yake ya mwisho. Shukrani za pekee ziwaendee:-

1.   Mhe. Daniel  T. Arap Moi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya kwa faraja na kwa kulipa gharama zote za matibabu ya Mama.
2.   Baba Askofu Silas Yego, Askofu Mkuu wa AIC Kenya kwa faraja ya kiroho wakati tukiwa Nairobi.
3.   Wafanyakazi wa Methodist Guest Hse
4.   Uongozi wa Benki Kuu na wafanyakazi wake wote.
5.   Wawakilishi wote wa East African Revival Fellowship.
6.   Maaskofu, Wachungaji na viongozi wote waliowakilisha Makanisa na Mashirika mbalimbali walioshiriki katika msiba huu.
7.   Viongozi na Waumini wote wa AIC Makongoro.
8.   Viongozi na wahudumu wa Mwanza Airport kwa mapokezi na huduma nzuri.
10. Ndugu na marafiki wote kutoka makanisa, mashirika, jamii.

Hatuna neno la ziada la kusema ila mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atawalipa na kuwazidishia kwa mema yote mliyoyatenda kwa ajili yetu.

Sisi tulimpenda sana mama yetu, lakini Mungu amempenda zaidi.

“Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.” AMEN

 (Ayubu. 14: 1-2) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Pole sana, tunajua Mama hajafa bali amelala.

    ReplyDelete
  2. Auntie yangu, we loved you na tunakushukuru na kumshukuru Mungu kwa maisha yako hapa duniani na yote uliyotufunza kwa nyakati tulizokuwa nawe.
    Poleni wana na Baba Askofu. Mungu hutufunga jeraha zetu tukumbuke.

    ...Ina thamani kama nini machoni pa Mungu mauti ya mwenye haki wake. ( Zaburi 116:15)

    Namwa.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana: Baba Askofu msitaafu, ndugu zangu na wana AIC wote hapa TZ. Mama amemaliza kazi yake njema mwache akapumzike. Amina

    Nawafariji kwa kawimbo haka maarufu:

    Siiiku zetu zikiisha duniani, Twaenda kwa baba mbinguni.......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...