MAREHEMU JOSEPHINE MASHAKA NYAGWASWA
Familia ya Askofu Mkuu Mstaafu Dr. M.
P. Nyagwaswa wa Capri Point - Mwanza, inawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na
mali wakati mama yetu mpendwa Josephine
Mashaka Nyagwaswa alipolazwa katika Hospital ya Nairobi - Kenya hadi kufanyiwa upasuaji mkubwa wa mgongo usiku wa
tarehe 23/08/2011 na kutwaliwa
mbinguni siku ya tarehe 24/08/2011 na
kuzikwa tarehe 27/08/2011 katika
makaburi ya Capripoint - Mwanza.
Shukrani zetu
ziwaendee Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wote wa Nairobi Hospital na Lee
Funeral Home kwa huduma zao kipindi chote ambacho Mama yetu amekuwa akilazwa
hapo na hadi kutwaliwa kwake.
Tunapenda kutoa
shukrani zetu za dhati kwa wale wote waliofika kutufariji na wale waliojaliwa
kujumuika nasi siku ile ya kumpuzisha MAMA kwenye safari yake ya mwisho.
Shukrani za pekee ziwaendee:-
1.
Mhe. Daniel T. Arap Moi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya
kwa faraja na kwa kulipa gharama zote za matibabu ya Mama.
2.
Baba Askofu Silas Yego, Askofu Mkuu wa
AIC Kenya kwa faraja ya kiroho wakati tukiwa Nairobi.
3.
Wafanyakazi wa Methodist Guest Hse
4.
Uongozi wa Benki Kuu na wafanyakazi
wake wote.
5.
Wawakilishi wote wa East African
Revival Fellowship.
6.
Maaskofu, Wachungaji na viongozi wote
waliowakilisha Makanisa na Mashirika mbalimbali walioshiriki katika msiba huu.
7.
Viongozi na Waumini wote wa AIC
Makongoro.
8.
Viongozi na wahudumu wa Mwanza Airport
kwa mapokezi na huduma nzuri.
10. Ndugu na marafiki
wote kutoka makanisa, mashirika, jamii.
Hatuna neno la ziada la kusema ila mwenyezi Mungu
mwingi wa rehema atawalipa na kuwazidishia kwa mema yote mliyoyatenda kwa ajili yetu.
Sisi tulimpenda sana mama yetu, lakini Mungu
amempenda zaidi.
“Bwana
Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.” AMEN
(Ayubu. 14: 1-2)
Pole sana, tunajua Mama hajafa bali amelala.
ReplyDeleteAuntie yangu, we loved you na tunakushukuru na kumshukuru Mungu kwa maisha yako hapa duniani na yote uliyotufunza kwa nyakati tulizokuwa nawe.
ReplyDeletePoleni wana na Baba Askofu. Mungu hutufunga jeraha zetu tukumbuke.
...Ina thamani kama nini machoni pa Mungu mauti ya mwenye haki wake. ( Zaburi 116:15)
Namwa.
Poleni sana: Baba Askofu msitaafu, ndugu zangu na wana AIC wote hapa TZ. Mama amemaliza kazi yake njema mwache akapumzike. Amina
ReplyDeleteNawafariji kwa kawimbo haka maarufu:
Siiiku zetu zikiisha duniani, Twaenda kwa baba mbinguni.......